Wakiingia vitani moja kwa moja, inaweza kusababisha janga la Dunia. Fahamu kuwa Russia ana silaha za nuklia, na Putin ni Rais dikteta ambaye ameua wapinzani wake wengi na amewaweka ndani wapinzani wake wengi.
Mtu katili hawezi kuona shida kuangamiza Dunia. Madikteta sifa moja kubwa waliyo nayo ni kutokubali kushindwa. Putin ana uhakika kuwa hayo mataifa ya Magharibi yakiingia vitani dhidi yake, lazima watampiga, na silaha pekee atakayoitegemea ni nuklia. Ndiyo maana mataifa haya ya Magharibi wameamua kutoa usaidizi wa silaha kwa Ukraine, na siyo wao kuingia vitani moja kwa moja dhidi ya Russia. Wanataka wamwangamize taratibu bila ya kuwepo kwa janga la Dunia. Nchi pekee imayoumizwa zaidi ni Ukraine maana uhai wa watu hauna mbadala.
Lakini kwa vyovyote vile, vita hii itaiumiza sana Urusi kwa miaka mingi. Haya mataifa ya Magharibi yanatoa ziada kuisaidia Ukraine, Russia anatumia kile ambacho kinahitajika sana kwaajili ya maendeleo ya watu wake. Angalia makampuni yalivyo mengi yaliyoondoka Russia, vijana wengi wenye ujuzi walivyomimbia Russia, silaha nyingi anazoendelea kuzitumia, n.k.