Kwanini Nchi za Magharibi zinalenga kuzigawanya nchi nyingi za Afrika?

Kwanini Nchi za Magharibi zinalenga kuzigawanya nchi nyingi za Afrika?

Tz boy 4tino

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2014
Posts
1,598
Reaction score
1,822
Mpaka sasa, Jambo lilo wazi katika vita ya Ethiopia ni mkono wa nchi za magharibi katika mgogoro huo.

Baadhi ya viashiria vinavyoonyesha mkono wa nchi za magharibi katika vita hiyo:
  • matumizi ya magari ya FAO yaliyopeleka msaada wa vyakula na waasi wa TPLF.
  • Ushahidi wa Marekani na washirika wake kuwapa taarifa za kisatelite waasi , zinazo onyesha mahali walipo wanajeshi wa Ethiopia.
  • Social media ku ban akaunti za viongozi wa Ethiopia pamoja na wanaharakati wanaotetea nchi hiyo
  • Kuzidi kwa propaganda dhidi ya serikali Ethiopia kutoka vyombo vya habari vya magharibi
  • Uungaji mkono wa wazi, maadai ya kikundi cha waasi wa Tigray na nchi za magharibi
Swali ni je, kwa nini nchi za magharibi zimewekeza sana katika kupindua utawala wa Ethiopia , na kuunga mkono vikundi vyengine vya waasi vilivyo na lengo la kujitenga barani Afrika??.

Wachambuzi wengi wa mambo ya Afrika wanaamini nchi nyingi za Afrika zitagawanywa ndani ya miaka 5 ijayo, je ni nini haswa lengo kuu la nchi za magharibi katika hili??

 
Umesahau kuwa waziri mkuu alipapatikiwa na mabeberu alipoingia, yapo wapi sasa.
 
Kwa Ethiopia shida ni bwawa la umeme ambalo Egypt (chawa wa mabeberu) hataki lijengwe kwa hofu ya kupungua kwa kiwango cha maji huko kwako. Kwa maeneo mengine ya Afrika jibu liko wazi - ukitaka kuendelea kuwatawala watu au kuchukua rasilimali zao wagombanishe, watenge, wavuruge.
 
Ninacho kiona mimi huu ni mwendelezo wa nchi za magharibi kupiga vita vya chini chini dhidi ya ujio was Wachina barani Afrika - Wamerika suala hili wamelivalia njuga sana, hawapendi ukaribu wa Utawala wa Ethiopia na Uchina, kumbuka Wachina wamewekeza sana Ethiopia kiviwanda na miundo mbinu, Wachina vile vile ndio wanaojenga bwawa kubwa la kuzalisha Umeme barani Afrika nchini humo, kumbukeni Rais Trump aliwahi kuitishia Ethiopia kwamba atatuma ndege za kivita akishirikiana na Misri kubomoa Bwana hilo linalo jengwa na Wachina.

Jaribuni kufatilia mwenendo wa viongozi wa USA wanapo tembelea baadhi ya nchi za Kiafrika mara nyingi kauli zao ukijita zaidi kuwatisha tisha viongozi wa Afrika kuhusu ujio wa Wachina barani Afrika wanawashutumu kwa mambo mengi ikiwemu wizi wa mali asili pamoja na kutwisha nchi za Kiafrika mzigo wa madeni - cha ajabu wazungu hao hawasemi chochote kuhusu jinsi nchi za magharibi ( Ulaya na Amerika) walivyo pora Mali asili lukuki barani Afrika wakati wa utawaka wa kikoloni na kwenda kujenga/endeleza kwao giving nothing in return kuendeleza bara la Afrika, tofauti kabisa na Wachina ambao wanawasaidia Mataifa mengi ya Kiafrika kujiendeleza wenyewe - wazungu hilo hawalipendi kabisa.

Serikali ya Adis Ababa hisipo omba msaada wa kusaidiwa kijeshi na Uchina au Urusi basi Uongozi wa Taifa hilo utaondolewa madarakani kama yaliyo tokea huko Ukraine under guise of colour revolution hiki ndicho kinacho endelea huko Ethiopian kwa kuchochewa na vyombo vya kijasusi vya nchi za magharibi.
 
Mchawi wa waafrika ni waafrika wenyewe
.
Kama mmejua adui yenu anayewagombanisha ni mzungu kwanini msiungane na kusimama imara kuliko kuendelea kuuana kama kuku?

Huyo waziri mkuu alipokuwa anawachinja watigray kwa kushirikiana na majeshi ya eritrea mbona mlikaa kimya?

Hao watigray walichezea kichapo cha mbwa koko kutoka majeshi ya ethiopia na eritrea sasa hivi ndio wamejitutumua liwalo na liwe.
 
Umesahau kuwa waziri mkuu alipapatikiwa na mabeberu alipoingia, yapo wapi sasa
Waliamini wanaweza kumbadili na kumfanya kibaraka wao baada ya kumpa tunzo ya Nobel, hawakujua kuwa Abiy Ahmed ni kiongozi mwenye msimamo na hayupo teyari kuwauza watu wake kwa masilahi yake binafsi.
 
Kwa Ethiopia shida ni bwawa la umeme ambalo Egypt ( chawa wa mabeberu) hataki lijengwe kwa hofu ya kupungua kwa kiwango cha maji huko kwako. Kwa maeneo mengine ya Afrika jibu liko wazi - ukitaka kuendelea kuwatawala watu au kuchukua rasilimali zao wagombanishe, watenge , wavuruge.
Misri pia ana mkono wako katika mgogoro huu. Naona juzi Egypt walitoa ombi rasmi la kuomba African Union ihamishe makao makuu kutoka Addis Ababa to Cairo. Jambo ambalo liliibua maswali mengi.
 
Waliamini wanaweza kumbadili na kumfanya kibaraka wao baada ya kumpa tunzo ya Nobel, hawakujua kuwa Abiy Ahmed ni kiongozi mwenye msimamo na hayupo teyari kuwauza watu wake kwa masilahi yake binafsi.
Si hivyo bwashee, yeye alidhani kuitawala Ethiopia ni rahisi kidemokrasia! Kama mwanzo Samia alivyojichanganya. Mabavu hayaepukiki ona hata sie, migao ya maji na umeme vikerudi
 
Hivi kweli kabisa kama waafrika hatuwezi kukubali kuungana? tuwe na sauti 1, tuwe na soko 1, tuwe na uhuru wetu wakujipangia mambo yetu bila kuamuliwa? maana rasilimali tunazo sasa wapi tumeshindwa kujikwamua?

Kwnye huu mgogoro ukiangalia vizuri kbisa utaona sisi waafrika wenyewe hatujitambui wapi tunataka kwenda wapi tulipoko, inakuwaje Egypt badala ya kutafuta njia yakupatanisha yeye aseme ofisi zihamishiwe kwake? hakika kuna mahala hatupo sawa na hatujui tutatokaje hapo mahala.
 
Maskini Ethiopia inateketea hivi hivi tunaiona na hakuna viongozi wa kikanda wana lizungumzia hilo wako busy na mambo yao na kutembeza bakuli kwa wahisani wengine wakiwa ndio kiuongo kikubwa cha kuwamaliza wenzao.

Jana nimewasikiliza wachambuzi wa BBC wote wana shangaa hawa jamaa waliko pata silaha mpya na zenye uwezo wa juu kwa ghafla hivyo.
 
Mkuu ukisoma siasa za uchumi wa dunia ndio utatambua ni kwajinsi gani mabeberu wanachokifanya ilimradi kumaintain dominance na kunyonya nchi maskini.
sio wakati wote, hata sisi waafrika lazima tujitathmini. Kwa Nini utawala kabla yake ilikuwa salama. Kwa Nini yeye? Lazima na yeye ana mapungufu yake. Viongozi wa Afrika ni wabinafsi, akiwepo Abby mwenyewe. Kama tukiwa na nia ya dhati kuendeleza afrika. Bila kuangalia wala kupendelea basi Afrika itaendelea.
 
Hivi hawa viongozi wetu wa nchi za kiafrika hawaoni kuwa wana wajibu wa kukutana, kujadiliana, kukubaliana lolote na hata kutokubaliana lolote?

Hivi hiyo AU ipo kwa ajili ya nini hasa?

Hayo yanayo tokea Ethiopia hayawezi tokea nchi nyingine hapo baadaye?

Waafrika tutaendelea kusubiri na kutegemea wazungu hadi lini?

Kama kichocheo cha vita ni ushawishi wa Uchina labda hata hilo bwawa la umeme tutaendelea kunyanyasika na kulialia hadi lini?

Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
 
Sio rahisi Afrika na waafrika kuwa wamoja, tusiwasingizie wazungu sisi tumeumbwa na vinasaba vya kuchukiana. Ebu angalia tz tuko tyr bidhaa za china ziingie nchini lkn hatuko tyr bidhaa za kenya kuingia nchini, tunafanyiana figisu,sasa unajiuliza hivi Uchumi wa nchi zetu utakua vipi wakati nchi zetu zinachukiana? Yaani kwetu bora Mchina kuliko Mkenya, Mganda nk. Tunakuza chumi za Mashariki ya Mbali na Ulaya kuliko kukuza uchumi wa kikanda. Mwafrika ni mchawi wa kuzaliwa tusimsingizie mzungu.
 
Back
Top Bottom