Kwanini Nchi za Magharibi zinalenga kuzigawanya nchi nyingi za Afrika?

Mbaazi zikikosa maua husingizia jua. Mawazo kama haya nimeyasikia tangu nikiwa shule ya msingi, sekondari na vyuo vikuu na sitaki niyasikie tena katika umri huu wa mtu mzima. Hii blame game haitatupeleka kokote. Kama tunajua nchi za magharibi zinatugawa au zina lengo la kutugawa Afrika, kwa nini tukubali kugawika? Tatizo ni wao au sisi?

Tusipojua tatizo letu liko wapi (tukiendelea kulitafuta tatizo kwa wengine) hatutaweza kuendelea/tutabakia kutawaliwa kifikira na materially. Tuondokane na kutafuta mchawi au kama tunamtafuta mchawi tumtafute withini us na siyo nje, tunapoteza muda bure!
 
Kwa TZ haitatokea sababu sisi ni makondoo na tunaaminishwa kuwa ni kisiwa cha ama [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848] kwaiyi Tz kutokupigana ni ukondoo
Unafiki wa Waafrika mpaka lini???

Wakati wa Tigray wanauawa nchi zote za kiafrika zilikaa kimya. UN ilishindwa hata kupeleka madawa na vyakula. Sudan ikabebe mzigo wa wakimbizi Afrika kimyaa!

Leo Waziri mkuu analia kichapo, ndo nchi za Afrika na wachangiaji wenzetu wanajitokeza. Mbona walikaa kimya wakati watu wanafia njiani kukimbia kichapo cha majeshi ya serikali?
Jimbo lile lina serikali yake hivyo wangeachwa wajiendeshe pia ni eneo ambalo historia ya wahabeshi ilipo na utajiri wa kihistoria wote upo kule. Hii ndo sababu Addis haitaki kupoteza. Siongei kwa udini lakini ikumbukwe ile nchi ni ya ki Orthodox ila mtawala aliyepo ni Mislam na ndo sababu wakamaliza vita na Eletria sababu wale wote wana imani moja.

Kuhusu bwawa la mto nile, nadhani wote tunajua kuwa kupata nishati ya kujitosheleza ni haki ya kila nchi ndo maana Tanzania tumeweza kutiririsha maji ya ziwa Victoria kwenda mpaka Tabora bila kibali cha waarabu. Kasoro ni kwamba mikoa inayolinda vyanzo vya mto Nile kama Kagera, mara na Mwanza, maji imekuwa ni ndoto tangu tupate uhuru lakini Tabora na Shinyanga walishapeta. Vitu kama hivi ndo vinavyochochea kupiga kelele mpaka kujitoa muhanga kupigania haki zao. Kwa TZ haitatokea sababu sisi ni makondoo na tunaaminishwa kuwa ni kisiwa cha amani.
 
Mpaka sasa, Jambo lilo wazi katika vita ya Ethiopia ni mkono wa nchi za magharibi katika mgogoro huo.

Baadhi ya viashiria vinavyoonyesha mkono wa nchi za magharibi katika vita hiyo:
  • matumizi ya magari ya FAO yaliyopeleka msaada wa vyakula na waasi wa TPLF.
  • Ushahidi wa Marekani na washirika wake kuwapa taarifa za kisatelite waasi , zinazo onyesha mahali walipo wanajeshi wa Ethiopia.
  • Social media ku ban akaunti za viongozi wa Ethiopia pamoja na wanaharakati wanaotetea nchi hiyo
  • Kuzidi kwa propaganda dhidi ya serikali Ethiopia kutoka vyombo vya habari vya magharibi
  • Uungaji mkono wa wazi, maadai ya kikundi cha waasi wa Tigray na nchi za magharibi
Swali ni je, kwa nini nchi za magharibi zimewekeza sana katika kupindua utawala wa Ethiopia , na kuunga mkono vikundi vyengine vya waasi vilivyo na lengo la kujitenga barani Afrika??.

Wachambuzi wengi wa mambo ya Afrika wanaamini nchi nyingi za Afrika zitagawanywa ndani ya miaka 5 ijayo, je ni nini haswa lengo kuu la nchi za magharibi katika hili??

DIVIDE AND RULE
 
Watigray endeleeni kuchapa kazi na huyo Abiy mkimpata hakikisheni mnapiga mboroh kabisa.
 
Nyinyi wenyewe mnajitengenezea migogoro na wananchi wenu na mnaanza kuwalaumu wazungu,,
 
Unafiki wa Waafrika mpaka lini???

Wakati wa Tigray wanauawa nchi zote za kiafrika zilikaa kimya. UN ilishindwa hata kupeleka madawa na vyakula. Sudan ikabebe mzigo wa wakimbizi Afrika kimyaa!

Leo Waziri mkuu analia kichapo, ndo nchi za Afrika na wachangiaji wenzetu wanajitokeza. Mbona walikaa kimya wakati watu wanafia njiani kukimbia kichapo cha majeshi ya serikali?
Jimbo lile lina serikali yake hivyo wangeachwa wajiendeshe pia ni eneo ambalo historia ya wahabeshi ilipo na utajiri wa kihistoria wote upo kule. Hii ndo sababu Addis haitaki kupoteza. Siongei kwa udini lakini ikumbukwe ile nchi ni ya ki Orthodox ila mtawala aliyepo ni Mislam na ndo sababu wakamaliza vita na Eletria sababu wale wote wana imani moja.

Kuhusu bwawa la mto nile, nadhani wote tunajua kuwa kupata nishati ya kujitosheleza ni haki ya kila nchi ndo maana Tanzania tumeweza kutiririsha maji ya ziwa Victoria kwenda mpaka Tabora bila kibali cha waarabu. Kasoro ni kwamba mikoa inayolinda vyanzo vya mto Nile kama Kagera, mara na Mwanza, maji imekuwa ni ndoto tangu tupate uhuru lakini Tabora na Shinyanga walishapeta. Vitu kama hivi ndo vinavyochochea kupiga kelele mpaka kujitoa muhanga kupigania haki zao. Kwa TZ haitatokea sababu sisi ni makondoo na tunaaminishwa kuwa ni kisiwa cha amani.
Abiy Ahmed sio Muislam n mkristo wa madhehebu ya kilokole
 
Sio rahisi Afrika na waafrika kuwa wamoja, tusiwasingizie wazungu sisi tumeumbwa na vinasaba vya kuchukiana. Ebu angalia tz tuko tyr bidhaa za china ziingie nchini lkn hatuko tyr bidhaa za kenya kuingia nchini, tunafanyiana figisu,sasa unajiuliza hivi Uchumi wa nchi zetu utakua vipi wakati nchi zetu zinachukiana? Yaani kwetu bora Mchina kuliko Mkenya, Mganda nk. Tunakuza chumi za Mashariki ya Mbali na Ulaya kuliko kukuza uchumi wa kikanda. Mwafrika ni mchawi wa kuzaliwa tusimsingizie mzungu.
Wakenya hawana adabu ndio maana tuwafanyia figisu. Wanakujaga humu na maneno ya dharau kuwa sisi hatuwezi fanya lolote kuwazidi wao wapo vema zaidi.

Wanatakiwa kuwa na adabu sana na taifa linalotumia bidhaa maana sisi ndo madon kwao why wanaleta dharau?!
 
Nyie mnajadili kishabiki sana Abey aliingia kichwakichwa tangiray na hakujua yapi yatakayotokea alikuwa na nafasi kubwa sana ya kumaliza huu mzozo Kwa njia ya mazungumzo toka mwanzo na Aya Mambo yasingefikia apa huwezi tatua mzozo WA ndani ya nchi Kwa kwendaa kupigana vita Kwa watu walioshika sehemu zote nyeti za nchii ni ujinga Tu alafu mnasema kuna mkono wa mzungu mzungu anaweza kuwepo Ila asilimia 90 huu mzozo aliukolezea Moto yeye mwenyewe Abey
 
Africa inateketezwa na waafrica wenyewe.
Think of madikteta wanavyowauwa wanavyowauwa wanaichi wao wenyewe?

Rais linachuki wazi wazi na kabila lingine?
Rais anachezea katiba atakavyo?
Shida ya Africa ni sisi wenyewe
 
Mpaka sasa, Jambo lilo wazi katika vita ya Ethiopia ni mkono wa nchi za magharibi katika mgogoro huo.

Baadhi ya viashiria vinavyoonyesha mkono wa nchi za magharibi katika vita hiyo:
  • matumizi ya magari ya FAO yaliyopeleka msaada wa vyakula na waasi wa TPLF.
  • Ushahidi wa Marekani na washirika wake kuwapa taarifa za kisatelite waasi , zinazo onyesha mahali walipo wanajeshi wa Ethiopia.
  • Social media ku ban akaunti za viongozi wa Ethiopia pamoja na wanaharakati wanaotetea nchi hiyo
  • Kuzidi kwa propaganda dhidi ya serikali Ethiopia kutoka vyombo vya habari vya magharibi
  • Uungaji mkono wa wazi, maadai ya kikundi cha waasi wa Tigray na nchi za magharibi
Swali ni je, kwa nini nchi za magharibi zimewekeza sana katika kupindua utawala wa Ethiopia , na kuunga mkono vikundi vyengine vya waasi vilivyo na lengo la kujitenga barani Afrika??.

Wachambuzi wengi wa mambo ya Afrika wanaamini nchi nyingi za Afrika zitagawanywa ndani ya miaka 5 ijayo, je ni nini haswa lengo kuu la nchi za magharibi katika hili??

Huu ni Ukosefu wa akili kudhani na kulaumu nchi za Magharibi!!Usiwe na dhana potofu kudhani kila kitu unahujumiwa!Jiulize kwanza!!Tusiwe kana nchi za kiarabu kudhani kila changamoto yao basi Israel inahusika!!Mchawi wa mwafrika ni mwafrika mwenzake tuache visingizio visivyokuwa na maana.
 
Na kwa nini kila anayeipinga serikali aitwe muasi, kwani lazima ukubaliane na serikali kwa kila kitu?
 
Huu ni Ukosefu wa akili kudhani na kulaumu nchi za Magharibi!!Usiwe na dhana potofu kudhani kila kitu unahujumiwa!Jiulize kwanza!!Tusiwe kana nchi za kiarabu kudhani kila changamoto yao basi Israel inahusika!!Mchawi wa mwafrika ni mwafrika mwenzake tuache visingizio visivyokuwa na maana.
Kuwa na akili ni kuamini kwamba hakuna mkono wa nchi za magharibi kwenye mzozo wa Ethiopia.

Labda nikuulize kwanini tweets za government supporters zilipoanza kutrend twitter wakafuta lakini za TPLF wakaziacha? Vilevile ni mara ngapi unasikia vyombo vyao vikitangaza kuhusu Maikadra Massacre au Kombolcha Massacre, jibu ni mara chache au hata wakitangaza wanatangaza kwamba "serikali ya Ethiopia imesema TPLF wameua watu kadhaa" wakati kwa serikali inageuzwa kwamba "serikali inaua raia wasio na hatia hata kama ni TPLF members". Hayo magari yaliyobeba chakula hadi leo hayajarudi sasa jiulize yameenda wapi

Hawa TPLF wanaungwa mkono na Marekani sababu wao ni mabepari na ipo hivyo tangu wanachukua nchi toka kwa wajamaa, bila shaka Marekani hajapenda ushirikiano wa China(wajamaa) na Ethiopia hasa kuhusu lile bwawa lakini pia uhusiano ulioanza wa Ethiopia na Eritrea(kumbuka Eritrea sio mabepari lakini pia wana vikwazo lukuki toka Marekani). TPLF ni silaha ya Marekani kwa Abiy.

Meles Zenawi alikuwa anapanga mipango na Marekani jinsi ya kuiadhibu Eritrea kwa kuiwekea vikwazo na kupandikiza waasi lakini leo hii Abiy amewageuza marafiki kinyume na matakwa ya Marekani. Ushahidi huu hapa; paragraph 6 & 7(wikileaks cable)
Cable: 09ADDISABABA2817_a

Patrice Lumumba kauliwa na CIA na ipo wazi tu, mapinduzi ya Mali na Guinea unajua nini kipo nyuma yake au unaamini hizi stori ya mapinduzi yamefanyika kuleta demokrasia? Vitu havitokei kwa bahati mbaya tu.

Hata huko Middle East Israel, Marekani na Nato wamehusika kuharibu zile nchi ila hiyo ni topic ya siku nyingine.
 
Kwa Ethiopia shida ni bwawa la umeme ambalo Egypt (chawa wa mabeberu) hataki lijengwe kwa hofu ya kupungua kwa kiwango cha maji huko kwako. Kwa maeneo mengine ya Afrika jibu liko wazi - ukitaka kuendelea kuwatawala watu au kuchukua rasilimali zao wagombanishe, watenge, wavuruge.

Kumbuka Al Sisi ni myahudi na anapata nguvu kutoka kwa matajiri wakubwa na viongozi wenye asili hiyo huko USA
Naona uko sahihi kabisa
 
Kadri waafrika tutakavyo zidi kutafuta mchawi kwa matatizo yetu ndivyo tutakavyo endelea kuwa mafukara.

Tuna viongozi wa hovyo ambao hawapo popote duniani ila Afrika tu sasa kwa nini tusiwe hivi tulivyo. Kila uchao wazungu, wazungu wakati wazungu wenyewe wako makwao huko.

Wakati mataifa mengi ya Afrika yanapewa uhuru kuna wazungu walitabiri kuwa hawa kamwe hawataweza kujitawala na ndicho kilichotokea.
 
Mpaka sasa, Jambo lilo wazi katika vita ya Ethiopia ni mkono wa nchi za magharibi katika mgogoro huo.

Baadhi ya viashiria vinavyoonyesha mkono wa nchi za magharibi katika vita hiyo:
  • matumizi ya magari ya FAO yaliyopeleka msaada wa vyakula na waasi wa TPLF.
  • Ushahidi wa Marekani na washirika wake kuwapa taarifa za kisatelite waasi , zinazo onyesha mahali walipo wanajeshi wa Ethiopia.
  • Social media ku ban akaunti za viongozi wa Ethiopia pamoja na wanaharakati wanaotetea nchi hiyo
  • Kuzidi kwa propaganda dhidi ya serikali Ethiopia kutoka vyombo vya habari vya magharibi
  • Uungaji mkono wa wazi, maadai ya kikundi cha waasi wa Tigray na nchi za magharibi
Swali ni je, kwa nini nchi za magharibi zimewekeza sana katika kupindua utawala wa Ethiopia , na kuunga mkono vikundi vyengine vya waasi vilivyo na lengo la kujitenga barani Afrika??.

Wachambuzi wengi wa mambo ya Afrika wanaamini nchi nyingi za Afrika zitagawanywa ndani ya miaka 5 ijayo, je ni nini haswa lengo kuu la nchi za magharibi katika hili??

Ukabila/ ukanda ndio unaoitesa Ethiopia hakuna mkono wa mtu hapo.
 
Hivi kweli kabisa kama waafrika hatuwezi kukubali kuungana? tuwe na sauti 1, tuwe na soko 1, tuwe na uhuru wetu wakujipangia mambo yetu bila kuamuliwa? maana rasilimali tunazo sasa wapi tumeshindwa kujikwamua?

Kwnye huu mgogoro ukiangalia vizuri kbisa utaona sisi waafrika wenyewe hatujitambui wapi tunataka kwenda wapi tulipoko, inakuwaje Egypt badala ya kutafuta njia yakupatanisha yeye aseme ofisi zihamishiwe kwake? hakika kuna mahala hatupo sawa na hatujui tutatokaje hapo mahala.
Tatizo lilianza walipo gawa mipaka ya Nchi na kuweka Nchi za kiarabu kuwa pamoja na Nchi za Kiafrika asili.chochote kitakachofanyika na nchi za kiafrika jua fika Algeria,Egypt, Morocco, Libya na Tunisia watakuwa wanawachora.
 
Back
Top Bottom