Kwanini Nchi za Magharibi zinalenga kuzigawanya nchi nyingi za Afrika?

Sisi wa afrika kwa ufupi upeo wetu wa kufikiri ni mdogo sana hivi kwanini tunapenda kuwabebesha mzigo wa lawama wazungu mfano ulio hai corona ,Libya ,Congo, Ethiopia nk tumezidi wa afrika tubadilike wa Tigray wana haki Yao kwa ufupi wasikilizwe
 
Nini kilisababisha wachinjwe Kama siyo uasi walioanzisha?
 
Waafrika Wana tabia ya kuwasema vibaya wazungu, ila hawataki kuzamia kwenda China, wanataka kwenda Kwa wazungu
 
Wakati huo wazungu hawakuona mpaka wakampa ahmed abiy tunzo ya amani ya nobel !!?
 
Waafrika Wana tabia ya kuwasema vibaya wazungu,ila hawataki kuzamia kwenda China, wanataka kwenda Kwa wazungu
Kwasababu hata haoWACHINA wenyewe nao hawajasalimika na GHILBA UNYAMA na UADUI unaofanywa na hao wapuuzi WAZUNGU
Simple tu kama huwezi kupambana nao ungana nao hata kinafiq tu yaani
 
Unafiki wa Waafrika mpaka lini?

Wakati wa Tigray wanauawa nchi zote za kiafrika zilikaa kimya. UN ilishindwa hata kupeleka madawa na vyakula. Sudan ikabebe mzigo wa wakimbizi Afrika kimyaa!

Leo Waziri mkuu analia kichapo, ndo nchi za Afrika na wachangiaji wenzetu wanajitokeza. Mbona walikaa kimya wakati watu wanafia njiani kukimbia kichapo cha majeshi ya serikali?

Jimbo lile lina serikali yake hivyo wangeachwa wajiendeshe pia ni eneo ambalo historia ya wahabeshi ilipo na utajiri wa kihistoria wote upo kule. Hii ndo sababu Addis haitaki kupoteza. Siongei kwa udini lakini ikumbukwe ile nchi ni ya ki Orthodox ila mtawala aliyepo ni Mislam na ndo sababu wakamaliza vita na Eletria sababu wale wote wana imani moja.

Kuhusu bwawa la mto nile, nadhani wote tunajua kuwa kupata nishati ya kujitosheleza ni haki ya kila nchi ndo maana Tanzania tumeweza kutiririsha maji ya ziwa Victoria kwenda mpaka Tabora bila kibali cha waarabu. Kasoro ni kwamba mikoa inayolinda vyanzo vya mto Nile kama Kagera, mara na Mwanza, maji imekuwa ni ndoto tangu tupate uhuru lakini Tabora na Shinyanga walishapeta. Vitu kama hivi ndo vinavyochochea kupiga kelele mpaka kujitoa muhanga kupigania haki zao. Kwa TZ haitatokea sababu sisi ni makondoo na tunaaminishwa kuwa ni kisiwa cha amani.
 
Umenena point tupu mkuu.
 
Wewe uwa ni propagandist, hakuna koment ya ukweli itatoka kinywani mwako.

Trump alisema: UENDA misri ikashambulia ilo bwawa, wewe hapa unabwabwaja eti alisema atatuma ndege kwenda kushambulia bwawa!

Shida ya Ethiopia ipo wazi ila kwasababu tushajijengea tabia ya kulaumu na kubebesha watu baki matatizo yetu ndiyo watu kama wewe wajuzi waku kutunga uwongo uwa ni comfort zone za mindsets za Waafrika wengi.
 
We jamaa ama unaandika uongo makusudi au hujui kinachoendelea Ethiopia.
 
Mkuu nipe mfano wa nchi ya kiafrika au nchi yoyote maskini ambayo imefanikiwa kwa kusimama yenyewe na kiongozi asiebebwa na mabeberu (akabakia hai)
 
Waafrika bado hatujawahi kua binadamu kamili, bado tuna safari ndefu sana. siku tukipata akili ya kujua nani ni adui wetu na tuishi nae vipi ndio tutakuja kupata ukombozi kamili wa fikra na uchumi.
 

Wazungu hatari sana.

Nawasubiri wayahudi/wamarekani weusi wa tandale, gongolamboto n.k waje waikane hii taarifa
 

Nikwambie kitu, jifunze ku- agree to disagree without offending anyone hilo LA kwanza, la pili ambalo ni very crucial usitukane watu ovyo,we leta hoja mbadala zenye substance - don't think tunashindwa kutumia abrasive languages za vijiweni - bottom line,is: jifunze kuheshimu binadamu wenzako hata kama mna maoni tofauti.

Kwa taarifa yako Trump na like mind wenzake, notably: Pompeo na John Bolton ni binadamu ambao walikuwa driven na inbuilt rabid hatred ya everything Chinese, mara ngapi Bolton alikuwa anatumwa na Trump barani Africa ku-preach viongozi wa Afrika kuhusu ubaya wa ujio wa Wachina barani Africa, mpaka sasa wazungu specifically Uncle SAM wako overly obsessed na Wachina!!

Now back to the main point - binafsi niliwahi kumsikia Donald Trump kwenye forum fulani hivi, akizungumzia ubaya wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Ethiopia linalo tokana na msaada wa Wachina kiufundi, kifedha na ujenzi, alisema/tishia kwa kusema anaweza kuisadia Misri kwa kuvurumisha cruise missiles za kubomoa bwawa la kuzalisha umeme nchini Ethiopia, sasa sijui kama alikuwa anatania au alikuwa serious, si unajua tena mtu mwenye alikuwa unpredictable kama Tsunami tidal waves.

Kusisitiza maoni yangu, sina shaka jana uliona kwenye TV maelfu ya waandamanaji katika mji mkuu wa Ethiopia yaani Adis Ababa, je, walikuwa wanashutumu Taifa gani kwamba ndilo linalo chochea na ku-finance vurugu zinazo endelea nchini Ethiopia - ni wazi tunashuhudia kwa maranyingine tena yaliyo tokea Ukraine ndio yanajirudia hivi sasa huko Ethiopia - na kusema kweli huo ndio mwanzo kwa kile kitakacho kuja kutokea hapo mbeleni barani Afrika kama Viongozi wa Kiafrika wasipo lishtukia hilo nchi nyingi za Kiafrika zitakubwa na migogoro ya kupandikizwa na kutumia mwanya/vurugu hizo kusimika madarakani viongozi ma puppet watakao support bara la Afrika kuwa recolonised kwa mara nyingine tena kwa kutumia mbinu mpya ie plan "B" ya kutisha tisha viongozi wa Afrika kuhusu ujio wa Wachina Barani Afrika.

Look - binafsi sikulazimishi ukubaliane na maoni yangu,we toa maoni mbadala na sio unaishia ku-trade inept tirade. CHEERS.
 
Chief, uenda approach yangu ya kukusahihisha inakukwaza ila hilo haliondoi ukweli kuwa we ni mjuzi wa kuweka chumvi katika komenti zako.
habari ya kuwa trump alisema atashambulia bwawa la Ethiopia haipo hata kwenye media zinazomchukia trump.

"
mimi nina weakness ya kutopenda kusikia uwongo, naweza nikamattack yoyote yule bila kujali itanisaidia nini.
 
"Kwanini nchi za Magharibi zinalenga kuzigawanya nchi za Afrika?"..
..Turudi Berlin Conference..
Ndio hao hao waliituwekea hiyo mipaka,nakusema hii Benin,Hii Chad,Hii Tanganyika, hii Rhodesia..nk
Kibaya zaidi hakukua na "mwakilishi" yeyote toka Afrika..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Misri pia ana mkono wako katika mgogoro huu. Naona juzi Egypt walitoa ombi rasmi la kuomba African Union ihamishe makao makuu kutoka Addis Ababa to Cairo. Jambo ambalo liliibua maswali mengi.
Wapuuuz wakubwa wale na wabaguzi..shenz zao..walishawah kuwaita waafrica mbwaa wa kusini mwa jangwa la sahara. Wale hawapaswii kuwa katika umoja wa africa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…