Kwanini nguruwe hauzwi minadani kama mbuzi, kondoo, ng'ombe na kuku?

Jibu murua kabisa mkuu. Hivyo tutegemee miaka ijayo kuwaona na minadani Kwa hakika?
 
Ahsantee sana mkuu Kwa michango Yako
 
Tatizo ndugu zetu wana nongwa sana, watasusa kwenda mnadan kununua hata vitu vingine kisa tu Kuna nguruwe. We c unaona hata kuku tunawapa wachinje, maana ukichinja wewe hawali.

Tunawapenda sana ndugu zetu, Ila wana noma sana.
Kweli kabisa mkuu. Ila tunaomba na wao watuvumilie tu kama sisi tunavyo wavumilia kutuchinjia mifugo yetu.
 
N
Naungana na wewe mkuu 100% maana unaweza enda Kwa wafugaji zaidi3 wanakwambia hawauzi ama Wana wateja wao maalumu. Lakni kukiwa na soko lao sehemu huwezi koswa kabisa.
 
Huo mnada ungekuwa ni mbio mbio za kufukuza nguruwe maana hawajawahi tulia sehemu moja. Yaani ukiwa na hamu ya mbio unae sa mnada wa nguruwe mpaka jion umekimbia kilomita za kutosha.
Anaefuatia kwa kukosa utulivu ni mbuzi.
Mkuu wakitengewa maeneo mazuri wakawa na mabanda Yao kama tunavyoona kwenye nanenane mbona inawezekana kabisa? Angalia comment no12 mkuu
 
nenda minada ya mbulu kule manyara mkuu wa meza yupo kama kawa hii ni kwa viongozi haiwezi kuwa kila sehemu
Labda Hivi karibu nimewahi fika mnada wa Katesh sikuwaona Tena sio mara1 sikuwahi kuwaona mkuu.Lakini siwezi kupingana nawewe huenda Kwa Sasa wanauzika na ni jambo jema kabisa asibaguliwe na yeye ni mnyama kama wanyama wengine tu.
 
Muhimu sana mkuu. Mimi nikienda viwanja bila kitimoto basi out yangu haijakamilika kabisa!! Mkuu wa meza naweza kumfuta alipo zaidi ya km10 mkuu imenitokea mara kadhaa hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…