Kwanini nguruwe hauzwi minadani kama mbuzi, kondoo, ng'ombe na kuku?

Kwanini nguruwe hauzwi minadani kama mbuzi, kondoo, ng'ombe na kuku?

Your lost
Wale hawana cha sokoni wananunuliwa moja kwa moja mabandani jinsi walivyo na thamani
Hawapatikani kwa wingi ndio maana, kama wangekuwa wanafugwa kwa kama ng'ombe au mbuzi au kuku sidhani kama wangekuwa adimu.
Ila mavi yao yananuka hatari kwa hiyo kufuga maeneo ya mijini ni shida.
 
Sio kweli, katafiti vizuri ukipata muda
Utafiti simple kabisa.
We pita mitaa ya Mbeya huko Iyunga, Uyole... ni mabanda ya kuuza nguruwe chini inapita mifereji ya majitaka. Huhitaji leseni.
Lkn jirani tu Bucha za nyama ng'ombe lazima uwe na leseni, ukaguzi wa mara kwa mara kuhakikisha usafi unazingatiwa
 
Nchi ina waislam na waislam hawapendi nguruwe ndio maana hauzwi minadani kama wanyama wengine. Ila hapohapo mnadani utakuta kuna eneo nyama za nguruwe zinauzwa na kuliwa hadharani
Kabisa,nilenda mnada mmoja karagwe,nilikuta kuna mtaa mzima ni wakuuzq na kukaanga nyama ya nguruwe,kitimoto inaliwa mitaa ile sio mchezo na bia za kutosha.
 
Jf saalam.

Wakuu tukitazama tu Kwa jicho la kawaida hata bila kuingiza dini/Imani zetu hapa napata ukakasi sana.

Ni kwanini Nguruwe pamoja na kupendwa sana na watu lakini sijawahi ona kwenye minada ya kawaida nguruwe nae anauzwa kama ilivyozoeleka kuona ng'ombe na punda wakiuzwa kwanini kwakwe ni tofauti?

Tangu nianze kutembelea minada mikubwa nakiri wazi sijawahi ona nguruwe minadani.

Ndio swali ninalo jiuliza ni kwamba hairuhusiwi nguruwe kuuzwa minadani?View attachment 3140160
Tembea ujionee, acha kujifungia magetoni
 
Attachments

  • 20241103_143845.jpg
    20241103_143845.jpg
    138.4 KB · Views: 2
Jf saalam.

Wakuu tukitazama tu Kwa jicho la kawaida hata bila kuingiza dini/Imani zetu hapa napata ukakasi sana.

Ni kwanini Nguruwe pamoja na kupendwa sana na watu lakini sijawahi ona kwenye minada ya kawaida nguruwe nae anauzwa kama ilivyozoeleka kuona ng'ombe na punda wakiuzwa kwanini kwakwe ni tofauti?

Tangu nianze kutembelea minada mikubwa nakiri wazi sijawahi ona nguruwe minadani.

Ndio swali ninalo jiuliza ni kwamba hairuhusiwi nguruwe kuuzwa minadani?View attachment 3140160
Nguruwe ni kama iphone inauzika akiwa bandani.
 
Back
Top Bottom