Kwanini nguruwe hauzwi minadani kama mbuzi, kondoo, ng'ombe na kuku?

Kwanini nguruwe hauzwi minadani kama mbuzi, kondoo, ng'ombe na kuku?

wazee wa kazi wapo 'mlangali ulayasi' kama unaelekea ludewa njombe kila tar 16 ya kila mwezi, wao ni kuuza nyama ya nguruwe tu tena wanakata nyama nyekundu tu na ile nyama nyeupe wanayeyusha mafuta wanayauza kwenye chupa. Mnyama ni mtamu sana aisee...ni ku enjoy tu!.
Nikifika minadani kitu cha kwanza ni kutafuta chimbo la nyama ya nguruwe kabla ya shughuli zilizonipeleka 😛 😛
 
wazee wa kazi wapo 'mlangali ulayasi' kama unaelekea ludewa njombe kila tar 16 ya kila mwezi, wao ni kuuza nyama ya nguruwe tu tena wanakata nyama nyekundu tu na ile nyama nyeupe wanayeyusha mafuta wanayauza kwenye chupa. Mnyama ni mtamu sana aisee...ni ku enjoy tu!.
Nikifika minadani kitu cha kwanza ni kutafuta chimbo la nyama ya nguruwe kabla ya shughuli zilizonipeleka 😛 😛
Mhhh! Unaweka na "matosan" kwa pembeni au ivo ivo.
 
Jf saalam.

Wakuu tukitazama tu Kwa jicho la kawaida hata bila kuingiza dini/Imani zetu hapa napata ukakasi sana.

Ni kwanini Nguruwe pamoja na kupendwa sana na watu lakini sijawahi ona kwenye minada ya kawaida nguruwe nae anauzwa kama ilivyozoeleka kuona ng'ombe na punda wakiuzwa kwanini kwakwe ni tofauti?

Tangu nianze kutembelea minada mikubwa nakiri wazi sijawahi ona nguruwe minadani.

Ndio swali ninalo jiuliza ni kwamba hairuhusiwi nguruwe kuuzwa minadani?
Anzisha tu mnada wa nguruwe, wala nguruwe wengi sana, hukosi wala nguruwe.
 
Ni elimu mbovu TULIO NAYO KUHUSU UFUGAJI WA NGURUWE na hii imepelekea serikal kukoswa mapato mengi hasa ya uuzaj holela wakuto kuweka mazingira rafik ya kisoko hasa minada ka wanyama wengine,, MI NASHUKURU PAMOJA NA HILI ILA TUNAPIGA HELA MING SANAAA ss wafugaji wahitaji wana TUTAFUTA WENYEWE soko hali tuumizi vichwa ukilinganisha na wanyama wengine,, nitambue pia uwepo wa machinjio karibu kila mkoa na baadh ya wilaya sasa TUNACHINJA NA WANAKAGULIWA kwa mazingira rafik kabisaaa kidogo dogo TUNABADILIKA HUENDA SIKU ZA USON tutaona minada
Kama Kuna machinjio nguruwe Kwa Sasa afadhari Sasa siku si nyingi hakika tutaanza ona nguruwe minadani. Ahsantee sana Kwa jibu zuri la kina mkuu🙏🙏🙏
 
Halafu kwenye biashara ya kitimoto hai, mnunuzi na muuzaji wote wanafahamu ni kilo ngapi za nyama zilizopo hapo japokuwa mnyama bado anatembea i.e. yupo hai kwa kutumia "weigh band." Hakuna kudanganyana kama wafanyavyo wale jamaa almaarufu Galagaja kwenye ng'ombe na mbuzi.
Kuna mnada niliwahi uliza mbona kwenye list ya wanyama wanauzwa kwenye kibali hiki nguruwe hayupo nikaambiwa nguruwe hauzwi mnadani nilijiuliza sababu hasa ni nn Hadi asiuzwe. Leo nimepata majawabu!
 
Sah
Inakuwa hivyo kwa sababu takriban 98% ya mwili wake ni Consumable items. i.e. Kila kitu hapo mwilini kwake kinauzwa/kinatumika kuanzia kongoro, kichwa, utumbo, mafuta, n.k. wa hiyo faida ni kubwa. Kinachotupwa labda ni manyoya tuu kwani hakuna ngozi. Ngozi hutolewa na mafuta yake.
Sahihi mkuu
 
Sasa ikiwa nyama choma ya kitimoto unapata na wanapatikana hadi nanenane, sidhani kama wanahitaji kupatikana hadi mnadani. Wangu maisha ni mafupi na kuna mambo mengi hebu tujadili vipi tunaweza kuwarithisha kizazi kijacho Tanzania yenye matumaini.
Tukemee uchawa na ufisadi mkuu then katiba mpya na tume huru ya uchaguzi
 
Back
Top Bottom