Kwanini ni Mbowe na sio Lissu na kwanini CHADEMA haifi?

Mm nilitegemea NYERERE kwa exposure yako kubwa hiyo, ungefanya analysis vizuri kabisa mazuri na mabaya ya lisu na mbowe hivyo hivyo, I'li kuwachia wanachadema wachague wao, nimesikitika sana ww kuonesha uchawa wako hapa, ivi wewe ndio ulie chukua tunzo za uwandishi bora afrika? Sijajua vigezo wanavyotumia. Mm nilitegemea ww utoe mwanga kwa watanzania juu cha ya nani ni bora Kati ya lisu na mbowe? Ulichokifanya umeonyesha ushabiki (uchawa) na sio mwandishi wa kutoa elimu. Frankly speaking l disvalued u. Japo na ww ni maoni Yako na unabenefiti kutoka kwa Mbowe.
 
Akikujibu niite
 
Mkuu alafu huyu eti ni mwandishi,amekuwa biased, kamsema lisu mabaya yake,tu bila kusema na ya Mbowe, audui wa taifa hili vijana wa chadema pia hafai, kabisa chawa
Huyo siyo kijana wa Chadema ni mwehu fulani pandikizi la Mbowe!
 
Mkuu mm pia nimeumia sana kuona mwandishi ambae anasifika afrika anakuwa biased ,kasema mabaya ya lisu na mazuri ya Mbowe? Afrika people tunashida kichwani ,ivi wanatumia vigezo gani kuchagua wandishi bora? Kama huyu NYERERE ndio mwandishi bora wa afrika twice basi wote humu jamii forum ni wandishi bora sanaaaaaaaaa
 
Hapo ndipo mnapokosea. Lissu hakusimama peke yake kum face JPM. Wakina Mbowe, Halima, Lema, Heche, Mnyika n.k. wote walipambana kikamilifu dhidi ya serikali ya JPM. Walipigwa, walitupwa rumande na walifungwa lakini waliendelea mpambano. Kuna Husna Amri Said na wenzake wa Chato ambae bila kujali kuwa pale ni kwa JPM walipambana kunyanyua bendera ya Chadema. Na wengi zaidi ambao bado wamo wanapambania chama na taifa lao. Wote hawa kwako ni bure, umemuona Lissu peke yake? Mnamuonaje Lissu shujaa kwa kupigwa na kusurvive risasi bila kutambua mchango mkubwa wa wanachama wenzake ambao walikataa kumpeleka kwenye hospitali za serikali na kumrusha kwa ndege kwenda Nairobi. Ni haki yenu kumpigia debe Lissu lakini hamna haki ya kufuta mchango mkubwa wa Mbowe na wenzake.

Amandla...
 
Kwa makala yako inaonyesha Chadema ni chama hakipo makini kwani walisimamisha mgombea wa urais asiye na uwezo hata wa kuingiza chama halafu wakasingizia Magufuli kaiba kura.
Kama Mbowe kaongoza chama miaka zaidi ya 20 na bado chama kinaendeshwa kwa kutegemea pesa za mfukoni mwa mtu Basi hafai.
Abdu ameanza kujulikana baada ya mama yake kuwa rais, Kama. Mbowe ana uwezo wa kuwasiliana na rais kwanini amtumie Abdu kushugulikia maswala ya mafao ya Lissu inaonyesha hata mngeingia madarakani James ndio angekuwa anavyofanya haya ya Abdu
 
Ninavyoelewa uhitaji mkubwa wa Rais mpya ni kuunda mpya mfumo wa utawala na dola katika nchi yetu. Kazi hiyo Lissu angeiweza sana. Lakini hilo hitaji haliko Chadema. Chadema kinahitaji kiongozi mpambanaji lakini mwenye uwezo pia wa kuhakikisha survival ya chama chake. Hiyo kazi Lissu haiwezi.

Amandla...
 
Wewe sio mpiga kura CDM ,
Wacha kila mtu auze sera zake...

Kama unampenda TL sawa na wapo wanaompenda FAM...
Hoja zake dhidi ya TL ndio hizo zako ni zipi?
 
Sisi ndiyo Watanzania eti. Tunajuana, wote ni wale wale. Tofauti hawa wako Mboga mboga, hawa zambazarau na wale wako kwenye Soccos.
Mchukue mtu wa mboga mboga mpeleke Saccos atakushangaza, hivyo hivyo Mtu wa Sacoss mpeleke mboga mboga akushangaze. Tatizo siyo mifumo, tatizo ni sisi watanzania wenyewe.
 
Soma uelewe..si mara zote kushiriki uchaguzi ni lengo ni kushinda hiyo nafasi, lengo linaweza kuwa kukijenga chama zaidi kuliko kushinda nafasi mnayogombea!
 
Kwa maana nyingine CHADEMA hahihtaji mfumo mpya wa kiutawala ila nchi ndo inahitaji? Nchi hahitaji kiongozi mwenye kuhakikisha survival ya wananchi?

Vilevile kwa maana nyingine, ukiwa mwanachama wa CHADEMA kwako nchi haina maana bali chama?
Chadema haina dola. Mwenyekiti wa Chadema hateui IGP, wakurugenzi wa Halmashauri, Tume ya Uchaguzi, n.k. Hawa wote tumeona jinsi wanavyoweza kutumika vibaya kama Rais hayuko makini. Na mabadiliko katika taasisi hizo yataletwa na Rais peke yake.
Ukiwa mwanachama wa chama chochote cha msingi zaidi ni chama kuliko nchi kwa sababu katika muundo wetu nafasi yako katika chama ndio inayokuwezesha kuleta impact katika serikali. Kwa kifupi, hauwezi kushika nafasi yeyote ya kiutawala ( Rais, Spika n.k.) bila kuwa mwanachama wa chama.

Amandla...
 
We nawe poyoyo kweli, unataka kufananisha mfumo wa chama kimoja kipindi hiko na sasa,
Hata chama changu pendwa ccm kila miaka kumi tunabadilisha mwenyekiti
Mnabadilisha kwa sababu tu ameingia Rais mpya na si vinginevyo.

Amandla...
 
Well said. Chadema ni Mbowe na mbowe ni chadema......
Mimi nilishasema Tundu lissu ni mzuri ila hayuko financially stable. Hana tofauti na Lipumba, marehemu Mrema, Mbatia, Zitto na kadhalika.
Hata wanamapinduzi wengi ulimwenguni ukiwasoma walikuwa kwanza wanahakikisha Wana nguvu ya kiuchumi kufinance hayo mapinduzi. Sio wote pangu pakavu halafu mnaongozana. Mtafika wapi.
Aanzishe chama chake halafu aone kama ni rahisi. Useless
 
🤣🤣🤣🤣 Lisu amekua nduli tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…