Kwanini ni nadra sana kusikia tuhuma za rushwa kwa Rais au waziri Marekani?

Kwanini ni nadra sana kusikia tuhuma za rushwa kwa Rais au waziri Marekani?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Hivi Marais na mawaziri wa Marekani huwa hawajihusishi na vitendo vya rushwa wakiwa madarakani au wanafanya kijanja sana? Huwa nasikia viongozi hawa wakitajwa kwenye skendo mbalimbali lakini ni nadra sana na sijawahi kusikia kabisa Rais au waziri Marekani anatuhumiwa kwa rushwa zinazohusu pesa za wa Marekani. Njoo Africa sasa, ni kama kunywa maji tu!
 
Hivi Marais na mawaziri wa Marekani huwa hawajihusishi na vitendo vya rushwa wakiwa madarakani au wanafanya kijanja sana? Huwa nasikia viongozi hawa wakitajwa kwenye skendo mbalimbali lakini ni nadra sana na sijawahi kusikia kabisa Rais au waziri Marekani anatuhumiwa kwa rushwa zinazohusu pesa za wa Marekani.
Taasisi zao ziko huru, mfano FBI Rais hana mamlaka yoyote ya kuwaingilia utendaji wao

Kwa kifupi Marekani hakuna vimemo.
 
information nyingi za miradi na uwekezaji ziko wazi yaana kuna transparency kwa hiyo sio rahisi sana kuzunguka chini ya meza au kufungua boneti kupeana miradi sijui chukua fukwe wa kilwa kwa dola milioni 20 kwenye deal za carbon.
 
Marekani inaongozwa na serikari mbili: Inavyoonekana na isiyoonekana.... Sijui nilitaka kuongea nini, anyway...
 
Viongozi wa wenzetu naonaga kesi zao kubwa ni kukwepa kulipa kodi na unyanyasaji wa wanawake/kingono.
 
Hivi Marais na mawaziri wa Marekani huwa hawajihusishi na vitendo vya rushwa wakiwa madarakani au wanafanya kijanja sana? Huwa nasikia viongozi hawa wakitajwa kwenye skendo mbalimbali lakini ni nadra sana na sijawahi kusikia kabisa Rais au waziri Marekani anatuhumiwa kwa rushwa zinazohusu pesa za wa Marekani. Njoo Africa sasa, ni kama kunywa maji tu!
1. Katiba yao ni nzuri, Hakuna mtu hata mmoja ambaye yupo juu ya Sheria. Completely, no one is above the law.
2. Kuna Demokrasia Pana na Uwazi (Transparency).
3. Serikali zao zinaendeshwa kwa Mifumo ya kitaasisi, Siyo Uamuzi wa mtu mmoja tu peke yake. Maamuzi mengi yanafanywa kwa mfumo wa ushirikishaji wa Watu zaidi ya mmoja kwa mtindo wa Akidi (Quorum).
Mtu mmoja tu peke yake kwa Cheo chake hawezi kufanya Uamuzi ambao ni halali pasipo kuwashirikisha Watu wengine kadhaa. Checks and balances systems.
 
Taasisi zao ziko huru, mfano FBI Rais hana mamlaka yoyote ya kuwaingilia utendaji wao

Kwa kifupi Marekani hakuna vimemo.
Marekani na nchi za Ulaya sio maumbwa kama maafrika na maccm! Majitu yanaiba halafu yanajisifu!
 
Back
Top Bottom