Kwanini nilisema kama ukiwa na fomula hii utaishia kuteseka kiuchumi?

Nkobe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
2,204
Reaction score
3,277
Wiki iliyopita nili post uzi unaozungumzia ni jinsi gani utakuwa Middle Class, yaani kuteseka ki –uchumi, kama ndio kwanza unaanza maisha na unafuata fumula ya walio wengi, yaani kununua gari then kujenga nyumba.

Ebu tuanze uchambuzi.

Kwa upande wa gari.

Bei ya chini kabisa ya gari used ni Tsh Milioni 5 au 6 mfano Vitz. Tuweke kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya mafuta kwa siku ambapo utatumia lita 5 hadi 6. Kwa siku utatumia 6X2,250=13,500/- kwa siku. Kwa mwezi itakuwa 13,500X30=405,000/-

Kwa mwaka 405,000X12-=4,860,000. Ukiweka Service na gharama zinginezo kama road license, bima, oil nk inafika milioni sita hadi saba kwa mwaka. Milioni saba ni sawasawa na kusomesha watoto 5 katika English medium school . Piga hiyo hesabu kwa miaka 5 utapata habari yako, na ndani ya miaka kama ingekuwa ni biashara ingekuwa mbali, au kukitokea makosa itakufa pia

Kwa upande wa Nyumba.

Nyumba ya kuishi utatumia milioni 40 au 50 kujenga nyumba ambayo itakusaidia ku serve kodi ya 150,000 kwa mwezi wakati kwa kutumia M40 ungetengeneza asset inayozalisha M1.5 kwa mwezi.

Nyumba ya kupangisha ni Idea nzuri lakini tathmini inaonesha nyumba ya kupangisha inatumia miaka 10 hadi 15 kurudisha hela, inategemea na mahali ilipo.

Kwa mambo kama haya ndiyo maana utakuta mtu kila mara analia kuwa haoni hela yake inakwenda wapi, lakini kasahau kuwa anahudumia gari.

Watu wengi hatuna utamaduni wa kuweka kumbukumbu ndiyo maana siku ile watu walisema maisha hayana fumula, wengine wakasema nanunua ndinga kwanza mambo mengine baadae.

Tatizo liko hivi ukianza na gari, uje nyumba then uhamie kwenye business itakuwa ni too late kwako hasa ki umri, uzoefu unaonesha kwa watanzania waliowengi tunajenga nyumba kwa taratibu sana kutokana na kipato, leo unapata laki 1 unanunua bati 9, mwezi ujao siment mifuko 5.

NB: Mimi naona ni bora ukawekeza kwenye vitu vinavyozalisha kwanza then Gari na Nyumba vitakuja baadae, yaani vi hudumiwe na biashara zako, lakini siyo mshahara wako.

Hayo ni maoni, vinginevyo kila mtu ana malengo yake
 
I agree with you bro,ukipanga nyumba hutakuwa na maumivu ya sijui kitasa kimeharibika mara bomba ,mara rangi.tatizo letu sisi watanzania wengi tunaenda kwa kuiga mno,kila mtu anataka kuwa kama fulani in a blink of an eye,huwa hatuna utamaduni wa kuangalia huyu ameanzaje mpaka kafika hapa ambapo mimi mdebwedo na nataka kujicompare naye.
 
Mimi nakubaliana na wewe mkuu,ila inategemea unaishi mkoa gani,kwa mkoa kama Dar gari ni kitu cha lazima aisee otherwise hata ufuatiliaji wa miradi yako utakuwa mgumu.Jambo la kuzumgumzia hapo kwenye gari ni kuhusu kununua gari ambalo ni economy na si kutaka sifa kununua gari la CC nyingi na luxury wakati huna kipato cha ziada.

Ukianza biashara ukiwa kijana unajifunza mengi sana kuliko kusubiri mpaka umalize kujenga japo si kila mtu atajenga nyumba kwa muda mrefu,kama hela ipo jenga fasta umalize then uingie kwenye biashara mazima ukiwa kwako stress free.
 
hahahaha jamani kuna mtu alisema vizuuuri kabisa on this....MAISHA HAYANA FORMULA.

wengine wana hela kibao wameachiwa za uridhi,
wengine wanaishi wakijua kifo kiko mahali popote,so wana spend kwa raha zao.
wengine wanaishi waki focus kutimiza ndoto zao,once wakizitimiza baaaas hawana haja ya kumiliki dunia nzima ( mimi mmoja wapo), wengine wameridhika na wanachokifanya na wako happy

ndugu usidhani kila mtu anataka kuwa na hela kama bill gates...mimi ndoto yangu kujenga nyumba yangu yenye gorofa moja na kununua Celica (2-doors - sport) ...kwaiyo ujue nikishamiliki celica ..maisha yangu hapa duniani 50% ni success...

life should be very simple....kama kila mtu angesoma philosophy...mfano..hata uwe na ela za kununua mikate 10,tumbo lako halimalizi slace 5...gari lina seats 5,kila siku unakalia seat 1 etc etc ....focus on being happy..stop trying teaching people how to live..you cant.
 

Ndiyo maana nilisema kwenye conclusion kuwa mwisho wa siku kila mtu ana mipango yake, wewe kama hauna idea ya ujasiriamali soma then pita, waachie wenye interest. Ndiyo maana kwenye hii forum kuna watu wanakuja na idea zao za kufuga bata, wengine machungwa
 
Ulichokosea kwenye ule uzi ulichanganya maisha ya bongo na mbele

Na huu mapungufu moja una assume wanaojenga wanakuwa na hela ya kukamilisha nyumba at per.usidanganye.wanaanza msingi hawana hela za nondo ya lenta.kama kukamilika nyumba ita cost 40 milioni basi jua hawana kiasi hicho wakati wanaanza.hivyo ku forgore nyumba na kufanya biashara ya 40 milion haipo.ujenzi wengi ni kwa kudunduliza

Pili gari usichukulie cost mafuta na car service tu na upande mwingine daladala/bajaji ile kuchelewa mishe zako,kukosa kufanya mambo mengi kwa kuzuiwa na usafiri na kero nyingine za ' public transport' nayo ni cost.gharama si fedha tu jiulize cost-benefit analysis mchumi Nkobe
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hapo kwenye red sidhani kama ni kweli, maana si wote wanaishi kwenye nyumba zao na si wote hawana nyumba,Watanzania wangekuwa wanaiga wengi tungekuwa na mfumo mmoja wa maisha, pia ujue sio kila mtu anaweza kufanya biashara ana sio kila mtu anaweza jenga, ninacho amini mimi ni kuwa matumizi sahihi ya fedha ni kufanya kitu unachoweza kufanya na kikakamilika
 
wewe unazungumza kiuhalisia kabisa, mtoa mada anadhani nyumba ya 40M hela ilitolewa mara moja, pili anashindwa kujua sio kila mtu anamuda wa kusimamia hiyo miradi, tatu sio kila mtu anaweza kufanya hizo biashara,
 
Mkuu umemaliza kila kitu. kuna tofauti kubwa sana kati ya maisha ya Bongo na America au na nchi zilizoendelea.
So, mtu anapoleta formula za America ili ziwe applied Bongo anakuwa anakosea sana.
Wenzetu nchi zilizoendela like america ambapo formular kama hii ya mleta mada iliko kopiwa, kuna nyumba nyiingi sana za National housing, Serikali ina apartments za kutosha za kupangisha raia wake tena kwa cheap kabisa.
Hapa kwetu kuna nyumba ngapi za National housing? zina'accomodate asilimia ngapi za raia?

Imagine mtu mwenye familia ya watoto wawili tuu wa kike na kiume, atahitaji kupanga nyumba angalau ya vyumba vitatu.
Mjini Dar kwa mfano nyumba ya vyumba vitatu inapangishwa si chini ya wastani wa TSh 350,000/= kwa maeneo ya kawaida kabisa.
350,000/- X 12 = ni TSH. 4,200,000/-
kwa mwaka utatakiwa kulipa 4.2M kwenye nyumba ya kupanga.
kwa miaka mitano: 4,200,000/= X 5 = 21,000,000/- mpangaji atalipa 21M.
Kwanini usijenge nyumba yako?

Kwenye issue ya gari, the guy has a point. nakubaliana na mtoa mada kwenye kipengele cha gari lakini sio nyumba ambayo ni one of the three basic needs, other basic needs iclude, Food and clothes.
 
Nkobe umeongea point, unajua ni watu wachache wanayaona hayo, ulichokiandika hapo ndio kinachotutofautisha ki uchumi kati ya family moja na nyingine, ulichokiandika hicho ndicho kinachotofautisha wachaga na makabila mengine ki uchumi.

Tatizo ni aina ya elimu tunayopewa tangu tukiwa utotoni, wasomi wengi wanaona wako na security kwa kuishi kwenye nyumba zao wenyewe, msomi umwambii kitu mbele ya nyumba yake, wanahisi wako secured lakini ki ukweli wako hatarini kwa maana inamlazimu aishi kwa kumtukuza boss ili kibarua kiendelee
 

mkuu nakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa sana. Hapo kwenye gari bado inategemea vitu vingi. Moja eneo mtu analoishi. Kwa dar gari ni basic need hasa kwa kuzingatia gharama za nauli( hasa kama safari ni za kuunga unga) hatari ya kuibiwa vitu kama cm na mikoba au pochi, utanashati(ukizingatia kuna kukanyagwa,kukimbilia gari kwahiyo jasho etc),na kubwa zaidi MUDA unaopotea barabarani kwa kuwa abiria hana mamlaka ya kukontroo spid na mambo mengine barabarani. Ila hapa ni muhimu kuangalia aina ya gari ya kununua.

Ishu nyingine ni kwamba biashara sio rahisi kama jamaa anavyo ashum. Ni rahisi sana kupoteza fedha kwenye biashara ( sio uoga tunaongea kwa uzoefu) kuliko kwenye ujenzi. Sasa ukizingatia pesa zenyewe za kuunga unga,then frame tu kodi ya mwezi 300000,mwaka 3.6m na unatakiwa ulipe cash,then uweke mtaji bado ulipe mfanyakazi,dah atlist kiwango cha chini sana uwe na 15 to 20m, zinapatikana wapi hizo?

Ila ukija kwenye nyumba kila mwezi unaweza fanya kitu fulani .Mfano take home sh 470,ni rahisi kutoa lori moja la mchanga kila mwezi ( 130 to 150 kwa lori moja-moshi) so baada ya kama mwaka au miwili hivi unakuta vifaa vya ujenzi vimekamilika.( na nyumba kwa familia za kibongo, ni muhimu sana mkuu)

Ila mleta mada ana hoja nzuri sema mazingira ya kibongo..............
 
kwa nini nitafute hela niishi maisha magumu,,natakiwa nimiliki mjengo then gar badae ndio nianze kuwekeza
 
Umesema ya moyoni kwa vyovyote vile yanatuhusu na wengi wetu Maarifa haya ndio tunayoyataka ili kujenga jamii iliyo Bora na Imara.
 
Ivi ukijenga Nyumba ikakamilika kisha ukaiuza faida yake si itakuwa kubwa sana kuliko kufanya Biashara anayoizungumzia mtoa mada?
 
Bado nawaza kuhusu hili jambo, lakini mwisho wa siku itategemea na mazingira na opportunities ulizonazo, kiwango ambacho unaweza ku-afford ku-take risk, flow ya income yako, alternatives ulizonazo nk.
 
Wazo lako ni zuri lakini nikuulize, unaelezea uzoefu au ni theory unayoijenga? Naamini kuwa ni vizuri kuanza na kuingiza fedha kwenye uzalishaji ili utengeneze pesa. Hata hivyo wazo hilo lina faida na changamoto zake. Faida ni pale biashara yako inapoweza kuzalisha faida na kukua. Hapo utakuwa hujapoteza muda. Lakini changamoto ni biashara hiyo unawekeza fedha kibao then inakata. Huna nyumba na kodi ya pango inakukaba. Ushauri. Ukiwa kijana hasa Dar. Kimbilia kununua kiwanja jenga two rooms faster then jikite kwenye uwekezaji. Ukifanikiwa ni vema ukianguka uko kwako. Nazungumzia uzoefu wa dar. Niliwekeza mara mbili bila mafaniko nikaamua kujenga sasa nina biashara yangu nzuri tu, gari, watoto shule wanaenda.
 

kwa hyo mkuu we umeona kujenga nyumba ya ghorofa ndyo umemaliza maisha .....watoto wanadaiwa ada shuleni utawalipia hyo nyumba?? Vp ukiumwa utalipa bill ya hospital kwa hyo nyumba ??? Suala la kuwa na hela nyingi ktk dunia ya sasa haliepukiki ili kujihakikisha maisha bora cku zote ni lazima uwe na uhakika wa kuwa na fedha na cyo nyunba nzuri ....msijipe moyo kiivo kuwa na nyumba ni sehem ndogo ktk maisha cyo inakuwa ndyo mwisho wa maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…