Kwanini nilisema kama ukiwa na fomula hii utaishia kuteseka kiuchumi?

Kwanini nilisema kama ukiwa na fomula hii utaishia kuteseka kiuchumi?

Wiki iliyopita nili post uzi unaozungumzia ni jinsi gani utakuwa Middle Class, yaani kuteseka ki –uchumi, kama ndio kwanza unaanza maisha na unafuata fumula ya walio wengi, yaani kununua gari then kujenga nyumba.

Ebu tuanze uchambuzi.

Kwa upande wa gari.

Bei ya chini kabisa ya gari used ni Tsh Milioni 5 au 6 mfano Vitz. Tuweke kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya mafuta kwa siku ambapo utatumia lita 5 hadi 6. Kwa siku utatumia 6X2,250=13,500/- kwa siku. Kwa mwezi itakuwa 13,500X30=405,000/-

Kwa mwaka 405,000X12-=4,860,000. Ukiweka Service na gharama zinginezo kama road license, bima, oil nk inafika milioni sita hadi saba kwa mwaka. Milioni saba ni sawasawa na kusomesha watoto 5 katika English medium school . Piga hiyo hesabu kwa miaka 5 utapata habari yako, na ndani ya miaka kama ingekuwa ni biashara ingekuwa mbali, au kukitokea makosa itakufa pia

Kwa upande wa Nyumba.

Nyumba ya kuishi utatumia milioni 40 au 50 kujenga nyumba ambayo itakusaidia ku serve kodi ya 150,000 kwa mwezi wakati kwa kutumia M40 ungetengeneza asset inayozalisha M1.5 kwa mwezi.

Nyumba ya kupangisha ni Idea nzuri lakini tathmini inaonesha nyumba ya kupangisha inatumia miaka 10 hadi 15 kurudisha hela, inategemea na mahali ilipo.

Kwa mambo kama haya ndiyo maana utakuta mtu kila mara analia kuwa haoni hela yake inakwenda wapi, lakini kasahau kuwa anahudumia gari.

Watu wengi hatuna utamaduni wa kuweka kumbukumbu ndiyo maana siku ile watu walisema maisha hayana fumula, wengine wakasema nanunua ndinga kwanza mambo mengine baadae.

Tatizo liko hivi ukianza na gari, uje nyumba then uhamie kwenye business itakuwa ni too late kwako hasa ki umri, uzoefu unaonesha kwa watanzania waliowengi tunajenga nyumba kwa taratibu sana kutokana na kipato, leo unapata laki 1 unanunua bati 9, mwezi ujao siment mifuko 5.

NB: Mimi naona ni bora ukawekeza kwenye vitu vinavyozalisha kwanza then Gari na Nyumba vitakuja baadae, yaani vi hudumiwe na biashara zako, lakini siyo mshahara wako.

Hayo ni maoni, vinginevyo kila mtu ana malengo yake

Well said mkuu simple analysis and clear...I short the number one priority when get job is to build business(asset) and not buying liability(things that cost you like car).
Hii ni formuala rahisi sana lakini kama ulivyosema watu wengi bado kuna maisha ya kukalili ndo maana walio wengi wako broke every month.
 
Formula ya maisha ipo ndugu, ndiyo maana huwa tunaanza na elimu then kutafuta pesa kunafuata. Kufanikiwa bila kujua hata kusoma A ni nadra sana. Pia ndio maana kuna somo la maarifa ya jamii, hiki nilichokiandika ni maarifa ya jamii pia

Mkuu mada yako ni sahihi kabisa,Mtu yeyote anayetaka kufanikiwa kiuchumi lazima afuate formula.
Mtu na vihela vya kudunduriza anajenga nyumba ati anakwepa kodi au awe na kwake tu au ananunua gari ati anataka usafiri haijakaa kiuchumi kabisa na hili ni tatizo kwa wtz wengi ahlafu tunabaki kulia maisha magumu mishahara midogo, unakuta mtu ati anaaza kukopa gari ya kutembelea au nyumba.

Mtu yeyote anayetaka kua na maisha bora na mafanikio ya kiuchumi kipaumbele cha kwaza ni elimu sio mpaka chuo kikuu, mtu ajue tu namna ya kumaster mzingira.
Baada ya hapo ni lazima atafute namna gani aweza kutengeneza hela hapa ndio kwene gap kati ya wachagga na makabila mengine mengi tz.
 
Ndiyo maana nilisema kwenye conclusion kuwa mwisho wa siku kila mtu ana mipango yake, wewe kama hauna idea ya ujasiriamali soma then pita, waachie wenye interest. Ndiyo maana kwenye hii forum kuna watu wanakuja na idea zao za kufuga bata, wengine machungwa

Mkuu

Kama ungelijua investment katika nyumba, basi hata hio biashara ungeona cha mtoto tu. Nyumba ni asset ambayo every single day inapanda thamani hasa maeneo ambayo yametolewa na serikali, yamepimwa, kama leo unajenga nyumba ya milioni 40 baada ya miaka 5 unauza milioni 80-500 hapa dar es salaam, karibu kuna rafiki yangu tulikutana Dar, alikuwa anaishi nje, alinambia Dar nimefika, asset ya nyumba ni mipango tosha ya kutokea kimaisha.
Hilo naamini, kwa gari nitakubaliana na wewe, kama mtu bado anaanza maisha.
 
Kuuliza c ujinga kila nikikatiza humu nakuta na hili neno Becky ndio nn?tens hasa kama MTU amekasirika na post husika
 
Mkuu umemaliza kila kitu. kuna tofauti kubwa sana kati ya maisha ya Bongo na America au na nchi zilizoendelea.
So, mtu anapoleta formula za America ili ziwe applied Bongo anakuwa anakosea sana.
Wenzetu nchi zilizoendela like america ambapo formular kama hii ya mleta mada iliko kopiwa, kuna nyumba nyiingi sana za National housing, Serikali ina apartments za kutosha za kupangisha raia wake tena kwa cheap kabisa.
Hapa kwetu kuna nyumba ngapi za National housing? zina'accomodate asilimia ngapi za raia?

Imagine mtu mwenye familia ya watoto wawili tuu wa kike na kiume, atahitaji kupanga nyumba angalau ya vyumba vitatu.
Mjini Dar kwa mfano nyumba ya vyumba vitatu inapangishwa si chini ya wastani wa TSh 350,000/= kwa maeneo ya kawaida kabisa.
350,000/- X 12 = ni TSH. 4,200,000/-
kwa mwaka utatakiwa kulipa 4.2M kwenye nyumba ya kupanga.
kwa miaka mitano: 4,200,000/= X 5 = 21,000,000/- mpangaji atalipa 21M.
Kwanini usijenge nyumba yako?

Kwenye issue ya gari, the guy has a point. nakubaliana na mtoa mada kwenye kipengele cha gari lakini sio nyumba ambayo ni one of the three basic needs, other basic needs iclude, Food and clothes.

mkuu tatizo watu wamekalili maisha..kwamba ni lazima ujenge kwanza ndo uanze weka miladi...hii iko sana kwa wafanyakaz..kujenga ni kitu kizuri sana..but wengi wanataabika sana mpka kumaliza..kwa mfano mtu anachukua mkopo wa mil 10 anaenda kujenga,nyumba inafika kwenye lenta haijaisha..so bdo analipa kod kwa land lord na mshahara unakatwa hapo anaanza ishi maisha ya shida sana kukopa haikuishi..kwa mtu kama hyu ni bora hyo 10m angekuwa smart kucreate some bisness then profit ya hapo ndo ujenzi uanze...hii ndo naona ideal poa wengi wanakoseaga hapa.
 
Mkuu

Kama ungelijua investment katika nyumba, basi hata hio biashara ungeona cha mtoto tu. Nyumba ni asset ambayo every single day inapanda thamani hasa maeneo ambayo yametolewa na serikali, yamepimwa, kama leo unajenga nyumba ya milioni 40 baada ya miaka 5 unauza milioni 80-500 hapa dar es salaam, karibu kuna rafiki yangu tulikutana Dar, alikuwa anaishi nje, alinambia Dar nimefika, asset ya nyumba ni mipango tosha ya kutokea kimaisha.
Hilo naamini, kwa gari nitakubaliana na wewe, kama mtu bado anaanza maisha.

Yes nyumba ni nzuri lakini hujamwelewa mtoa mada. Yeye anasema kwani ujinge nyumba halafu unaendelea kuwa hoi kiuchumi? Kwanini hiyo hela usingeizungusha ipatikane extra ujenge nyumba na bado ubaki na hela nyingi ambayo ieendelee kujiongeza na kukupa stable income?
 
Mkuu,mawazo yako ndio ya kwangu,watu wengi ukiwaambia hvyo wanakuona wewe ni wa ajabu lakini kiuhalisia huo uliousema ndio ukweli wenyewe,haiwezekani ukaizike hela yako ya mkopo kwenye nyumba halafu uishi kwa tabu na kubangaiza,wakati ile fedha ya mkopo ungeweza kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ambayo faida yake ndiyo ikufanye ujenge wakati huo huo mtaja wa biashara bado unao
 
Wiki iliyopita nili post uzi unaozungumzia ni jinsi gani utakuwa Middle Class, yaani kuteseka ki –uchumi, kama ndio kwanza unaanza maisha na unafuata fumula ya walio wengi, yaani kununua gari then kujenga nyumba.

Ebu tuanze uchambuzi.

Kwa upande wa gari.

Bei ya chini kabisa ya gari used ni Tsh Milioni 5 au 6 mfano Vitz. Tuweke kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya mafuta kwa siku ambapo utatumia lita 5 hadi 6. Kwa siku utatumia 6X2,250=13,500/- kwa siku. Kwa mwezi itakuwa 13,500X30=405,000/-

Kwa mwaka 405,000X12-=4,860,000. Ukiweka Service na gharama zinginezo kama road license, bima, oil nk inafika milioni sita hadi saba kwa mwaka. Milioni saba ni sawasawa na kusomesha watoto 5 katika English medium school . Piga hiyo hesabu kwa miaka 5 utapata habari yako, na ndani ya miaka kama ingekuwa ni biashara ingekuwa mbali, au kukitokea makosa itakufa pia

Kwa upande wa Nyumba.

Nyumba ya kuishi utatumia milioni 40 au 50 kujenga nyumba ambayo itakusaidia ku serve kodi ya 150,000 kwa mwezi wakati kwa kutumia M40 ungetengeneza asset inayozalisha M1.5 kwa mwezi.

Nyumba ya kupangisha ni Idea nzuri lakini tathmini inaonesha nyumba ya kupangisha inatumia miaka 10 hadi 15 kurudisha hela, inategemea na mahali ilipo.

Kwa mambo kama haya ndiyo maana utakuta mtu kila mara analia kuwa haoni hela yake inakwenda wapi, lakini kasahau kuwa anahudumia gari.

Watu wengi hatuna utamaduni wa kuweka kumbukumbu ndiyo maana siku ile watu walisema maisha hayana fumula, wengine wakasema nanunua ndinga kwanza mambo mengine baadae.

Tatizo liko hivi ukianza na gari, uje nyumba then uhamie kwenye business itakuwa ni too late kwako hasa ki umri, uzoefu unaonesha kwa watanzania waliowengi tunajenga nyumba kwa taratibu sana kutokana na kipato, leo unapata laki 1 unanunua bati 9, mwezi ujao siment mifuko 5.

NB: Mimi naona ni bora ukawekeza kwenye vitu vinavyozalisha kwanza then Gari na Nyumba vitakuja baadae, yaani vi hudumiwe na biashara zako, lakini siyo mshahara wako.

Hayo ni maoni, vinginevyo kila mtu ana malengo yake

ki ukweli ni jambo LA busara sana kuanza kuwa na investment yenye kukupa faida katika muda mfupi
 
mleta mada uko vizuri. uchambuzi wako uko vizuri.
kuna kitu wachangiaji hapa wanachanganya kuhusu gari, mleta mada ameonya kununua gari na kutegemea kulihudumia kwa fixed income, probably mshahara tu. kwa kweli itakusumbua, lakini kama una mradi wowote hata kama ni home based project kama ufugaji kuku, iko vizuri.

binafsi nilinunua gari, kwa sababu nilikuwa natumia fedha nyingi katika matumizi ya tax, binafsi mbali na safari za kazini, huwa napenda kutembea na familia yangu, hivyo kwa kununua gari najiona nime-save pesa kwa matumizi ya public transport. kimbembe huwa kinakuja, tairi zimeisha, service na makaratasi, sema nina other source of income, vinginevyo, ni kuongeza umaskini kama mleta mada anavyotanabaisha.

nilijenga nyumba yangu kwa miaka 5, kidogo kidogo, hivyo ni kweli kuwa hata ukimkuta mtu ana nyumba ya ml 50, ni wachache sana waliokuwa nazo zote kwa wakati mmoja. lakini wazo la mtoa mada katika ujenzi wa nyumba liko vizuri, tujiulize kwa nini wahindi wanashupaa kukaa nyumba za msajili/NHC, wanajua. kwa kulitambua hilo ndo maana nimesitisha mpango wa ujenzi wa nyumba niliyodhani ya kisasa ya kuishi, kwani ninayotaja hapa kujenga, nilijenga nikisema hii ni ya kuanzia maisha tu. lakini hiyo ya kuanzia pia imenisaidia kuwa huru zaidi na kupunguza gharama za kodi kwani hata nikiwa peke yangu huwa sitaki kubanwa, nilikuwa nimepanga nyumba nzima, kwa sasa na familia yangu extended, ndo kabisaaaa.

hivyo mada iko vizuri, ukiona hai-apply kwako, kwa wengine ni somo tosha, lakini hata kama unadhani haiko vizuri, hutakosa cha kujifunza, for a reasonable person.
 
Mkuu

Kama ungelijua investment katika nyumba, basi hata hio biashara ungeona cha mtoto tu. Nyumba ni asset ambayo every single day inapanda thamani hasa maeneo ambayo yametolewa na serikali, yamepimwa, kama leo unajenga nyumba ya milioni 40 baada ya miaka 5 unauza milioni 80-500 hapa dar es salaam, karibu kuna rafiki yangu tulikutana Dar, alikuwa anaishi nje, alinambia Dar nimefika, asset ya nyumba ni mipango tosha ya kutokea kimaisha.
Hilo naamini, kwa gari nitakubaliana na wewe, kama mtu bado anaanza maisha.

Dah uji*a ni shida sana why unajenga nyumba kwa 50 million ili ikurudishie fedha yako baada ya miaka mitano Kwanini usiagize Costa 2 kutoka japani ambapo kwa siku zinarudisha 150,000 ×2 =300,000/=

300,000 ×30=9,0000,000M

9,000,000×12=108M

108M unatoa operating expnse kama 25Million Unabakiwa na 83 million unaagiza costa 4 sasa kwa siku utakua unaingiza laki 800,000×30 Kwa mwezi ni 24,000,000 pesa yako inarudi baada ya miezi 6 then unaanza kupiga faidaaaa! 24M ×12=268M

268M×5=1.3Billion operating expense ni 500million So faida ni 800Million
 
Ivi ukijenga Nyumba ikakamilika kisha ukaiuza faida yake si itakuwa kubwa sana kuliko kufanya Biashara anayoizungumzia mtoa mada?

tatizo hii nchi tunaishi wabongo, nani atakubali toa 50 or 70 mil angalia anajua akiokoteza bati na cement naye atajenga.

ili ufanye biashara hiyo nunua viwanja prime area ,then jenga nyumba ya kisasa kuwatafuta high income people. sijui kama garama zake utazimudu?
 
Mkuu@AllenSnr coaster kwa milioni 25? kwa mtu au hizi za kuagiza japan? ninavyojua hiyo milioni 25 ni bei ya hiace..
 
Dah uji*a ni shida sana why unajenga nyumba kwa 50 million ili ikurudishie fedha yako baada ya miaka mitano Kwanini usiagize Costa 2 kutoka japani ambapo kwa siku zinarudisha 150,000 ×2 =300,000/=

300,000 ×30=9,0000,000M

9,000,000×12=108M

108M unatoa operating expnse kama 25Million Unabakiwa na 83 million unaagiza costa 4 sasa kwa siku utakua unaingiza laki 800,000×30 Kwa mwezi ni 24,000,000 pesa yako inarudi baada ya miezi 6 then unaanza kupiga faidaaaa! 24M ×12=268M

268M×5=1.3Billion operating expense ni 500million So faida ni 800Million

Is it so simple to become a millionaire?
 
Unatakiwa kiinvest kimkakati then buy a means of transport lastly house....
 
Acheni uwoga nyie madogo mi nilianza kabiashara kadogo then uwanja saivi Nina gari Nyumba na biashara ila sikuiga formula zenu
 
Back
Top Bottom