Mods Tafadhari usiunganishe uzi huu ili tufanye uchambuzi wa ki uchumi hapa na wadau.
Wiki iliyopita nili post uzi unaozungumzia ni jinsi gani utakuwa Middle Class, yaani kuteseka ki uchumi ,kama ndio kwanza unaanza maisha na unafuata fumula ya walio wengi, yaani kununua gari then kujenga nyumba
Ebu tuanze uchambuzi.
Kwa upande wa gari.
Bei ya chini kabisa ya gari used ni Tsh Milioni 5 au 6 mafano Vitz.
Tuweke kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya mafuta kwa siku ambapo utatumia lita 5 hadi 6. Kwa siku utatumia 6X2,250=13,500/- kwa siku. Kwa mwezi itakuwa 13,500X30=405,000/-
Kwa mwaka 405,000X12-=4,860,000. Ukiweka Service na gharama zinginezo kama road license, bima, oil nk inafika milioni sita hadi saba kwa mwaka. Milioni saba ni sawasawa na kusomesha watoto 5 katika English medium school . Piga hiyo hesabu kwa miaka 5 utapata habari yako, na ndani ya miaka kama ingekuwa ni biashara ingekuwa mbali, au kukitokea makosa itakufa pia
Kwa upande wa Nyumba.
Nyumba ya kuishi utatumia milioni 40 au 50 kujenga nyumba ambayo itakusaidia ku serve kodi ya 150,000 kwa mwezi wakati kwa kutumia M40 ungetengeneza asset inayozalisha M1.5 kwa mwezi.
Nyumba ya kupangisha ni Idea nzuri lakini tathmini inaonesha nyumba ya kupangisha inatumia miaka 10 hadi 15 kurudisha hela, inategemea na mahali ilipo.
Kwa mambo kama haya ndiyo maana utakuta mtu kila mara analia kuwa haoni hela yake inakwenda wapi, lakini kasahau kuwa anahudumia gari.
Watu wengi hatuna utamaduni wa kuweka kumbukumbu ndiyo maana siku ile watu walisema maisha hayana fumula, wengine wakasema nanunua ndinga kwanza mambo mengine baadae. Tatizo liko hivi ukianza na gari, uje nyumba then uhamie kwenye business itakuwa ni too late kwako hasa ki umri, uzoefu unaonesha kwa watanzania waliowengi tunajenga nyumba kwa taratibu sana kutokana na kipata, leo unapata laki 1 unanunua bati 9, mwezi ujao siment mifuko 5.
NB: Mimi naona ni bora ukawekeza kwenye vitu vinavyozalisha kwanza then Gari na Nyumba vitakuja baadae, yaani vi hudumiwe na biashara zako, lakini siyo mshahara wako.
Hayo ni maoni, vinginevyo kila mtu ana malengo yake