Kwanini nilisema kama ukiwa na fomula hii utaishia kuteseka kiuchumi?

Kwanini nilisema kama ukiwa na fomula hii utaishia kuteseka kiuchumi?

Mim nilianza kununua kiwanja 2009 kwa 8.5m (hapo gari ningeweza nunua).sasa hivi eneo kama ili linauzwa 50m.Nimejenga na ninaishi na familia sitakaa nikajuta kwa kuanza kujenga kwa sbb za kijamii na kiuchumi.Kiuchumi tuna miradi ambayo ni home based project.1 kuku (wa mayai,nyama,chotara na wa kienyeji)2.mradi wa kusambaza maji na 3. flemu za kupangisha.Labaour force niliyoiajiri kwa kazi za ndani wanadeal na biashara pia.sina tax,rent,na zaidi close supervion ipo. Naweza kupata loan kupitia projects hiz
 
Anyway topic hii ina mambo mengi ambayo ni variable from mtu na mtu,1.mazingira 2.Ability to take calculated risk 3.business knowledge 4.kipaumbele cha mtu kutokana na changamoto aliyonayo.5.opportunity available.n.k.but kwa mtizamo wangu, cash flow is first thing,yaani kufanya vitu ambayo vitaongeza mzunguko wangu wa fedha kwanza,na hapa ndo tunapotofautiana,mwingine anaona aanze na biashara bcz anaujuzi na uzoefu fulani kwake risk is very low,but some people bcz hana ujuzi na uzoefu wa biashara the best ni kutumia mshahara kujenga na kuridhika na kidogo,but financial freedom start with investment that will insure positive cash floww then spending but not all can afford this.
 
Kwa harakaharaka kama hujaingia katika majukumu ya familia ni vizuri sana kufuata ushauri wa hii thread. Ukiingia katika majukumu ya familia tena nyie ndio tegemezi inakuwa ngumu maana ikitokea la kutokea na huna nyumba watoto watapata shida sana. Hivyo, mawazo kama haya yanatakiwa yawe tunakuwa nayo ili kuweza kupanga maisha yetu ya baadae.
 
Ndiyo maana nilisema kwenye conclusion kuwa mwisho wa siku kila mtu ana mipango yake, wewe kama hauna idea ya ujasiriamali soma then pita, waachie wenye interest. Ndiyo maana kwenye hii forum kuna watu wanakuja na idea zao za kufuga bata, wengine machungwa

Huwezi kuridhika na maisha kwa Cecil two doors... After couple of years Cecil two doors is nothing uta taman another stuffs which means huja ridhika
 
Waoga wanaanza kujenga nyumba kwanza wasio waoga wanajikita kwenye biashara maana hao waoga waliojenga nyumba hawana ubavu wa kukopa benki mikopo kwa kutumia nyumba zao wanaogopa watafeli kurudisha mikopo hivyo nyumba zao kuuzwa, nyumba ni secured investment for the weak sababu licha ya kuappreciate value annually wenye nyumba hawana ubavu wa kuziuza ili kutengeneza capital kama hamna higher risk hakuna higher return,kujenga nyumba hakuna risk, kujenga nyumba ni kuzika hela huwezi kuta mhindi anajenga nyumba salasala hata siku moja sababu hakuna faida
 
CMBO is happy when.....

Akaunti yangu inaongezeka hela kila mwezi (saving) HOW ?

Ku multply investment na biashara ndogo ndogo ili kila mwezi saving iwe kubwa na sio kupungua, mfano mwezi huu nimesave 1m next month atleast 1.5m.

I believe kwenye kununua mashamba, that the only reason pesa yangu huwa inatoka kwenye account, sababu nyingine ni kufungua biashara nyingine.. Naamini shamba la heka moja mnapopaita porini in 5 yrs the ordinary person kununua ni issue,
How does it feel unanunua shamba la heka moja 1m kwa only 4m then in less than 5 yrs anakuja mtu anataka kukupa 100m umegoma anaongeza inakuwa 150m, what will it be ukiwa mbishi kwa 10 yrs?
Sina nyumba nimepanga and i think am happy mana i am my own boss after three yrs ya kukimbilia posta alfajiri na mikataba ya mwaka mmoja mmoja.
Ila kama umeajiriwa na upo happy huna mpango na biashara na your family is happy, then u are living fine too
 
Kujenga tu nyumba ya kushi mwenyewe wakti huna vyanzo vya uhakika wa mapato ni kama kununua liability. Nyumba labda jenga kwa madhumuni ya kupangisha kama ndo bado unatafuta maisha. Na kabla hujajenga nyumba ya kupangisha inabidi uangalie mahitaji ya soko katika eneo hilo maana hayo ndo yataonyesha return itakuwaje. Kujenmga nyumba ya milioni mia halafu unaipangisha kwa laki tatu na hamsini kwa mwezi huooo ni ujuhaaa ulipitilizaa:becky:
 
Mods Tafadhari usiunganishe uzi huu ili tufanye uchambuzi wa ki uchumi hapa na wadau.
Wiki iliyopita nili post uzi unaozungumzia ni jinsi gani utakuwa Middle Class, yaani kuteseka ki –uchumi ,kama ndio kwanza unaanza maisha na unafuata fumula ya walio wengi, yaani kununua gari then kujenga nyumba

Ebu tuanze uchambuzi.

Kwa upande wa gari.

Bei ya chini kabisa ya gari used ni Tsh Milioni 5 au 6 mafano Vitz.
Tuweke kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya mafuta kwa siku ambapo utatumia lita 5 hadi 6. Kwa siku utatumia 6X2,250=13,500/- kwa siku. Kwa mwezi itakuwa 13,500X30=405,000/-

Kwa mwaka 405,000X12-=4,860,000. Ukiweka Service na gharama zinginezo kama road license, bima, oil nk inafika milioni sita hadi saba kwa mwaka. Milioni saba ni sawasawa na kusomesha watoto 5 katika English medium school . Piga hiyo hesabu kwa miaka 5 utapata habari yako, na ndani ya miaka kama ingekuwa ni biashara ingekuwa mbali, au kukitokea makosa itakufa pia

Kwa upande wa Nyumba.

Nyumba ya kuishi utatumia milioni 40 au 50 kujenga nyumba ambayo itakusaidia ku serve kodi ya 150,000 kwa mwezi wakati kwa kutumia M40 ungetengeneza asset inayozalisha M1.5 kwa mwezi.
Nyumba ya kupangisha ni Idea nzuri lakini tathmini inaonesha nyumba ya kupangisha inatumia miaka 10 hadi 15 kurudisha hela, inategemea na mahali ilipo.
Kwa mambo kama haya ndiyo maana utakuta mtu kila mara analia kuwa haoni hela yake inakwenda wapi, lakini kasahau kuwa anahudumia gari.

Watu wengi hatuna utamaduni wa kuweka kumbukumbu ndiyo maana siku ile watu walisema maisha hayana fumula, wengine wakasema nanunua ndinga kwanza mambo mengine baadae. Tatizo liko hivi ukianza na gari, uje nyumba then uhamie kwenye business itakuwa ni too late kwako hasa ki umri, uzoefu unaonesha kwa watanzania waliowengi tunajenga nyumba kwa taratibu sana kutokana na kipata, leo unapata laki 1 unanunua bati 9, mwezi ujao siment mifuko 5.

NB: Mimi naona ni bora ukawekeza kwenye vitu vinavyozalisha kwanza then Gari na Nyumba vitakuja baadae, yaani vi hudumiwe na biashara zako, lakini siyo mshahara wako.

Hayo ni maoni, vinginevyo kila mtu ana malengo yake

Ngoja nijikite kwenye nyumba kwanza.
Kuna investment za aina nyingi,investment ya kwenye nyumba ni for security. unaweza hiyo nyumba ukaenda kuombea mkopo benki na siju hizi bank wanakubali hata squatters.
Na unazungumzia 40m ya nyumba kua ukiweka kwenye buashara utapata 1.5m kwa mwezi sasa naomba unijibu ni watu wangapi wanakua na hiyo 40m cash kwa ajili ya kujenga nyumba???Hela inayokusanywa kidogo kidogo ni bora iwekwe kwenye investment kama nyumba moja kwa moja sababu ukisubiri ifike 40m kwa ajili ya biashara kamwe haitafika.
 
Mimi nakubaliana na wewe mkuu,ila inategemea unaishi mkoa gani,kwa mkoa kama Dar gari ni kitu cha lazima aisee otherwise hata ufuatiliaji wa miradi yako utakuwa mgumu.Jambo la kuzumgumzia hapo kwenye gari ni kuhusu kununua gari ambalo ni economy na si kutaka sifa kununua gari la CC nyingi na luxury wakati huna kipato cha ziada.

Ukianza biashara ukiwa kijana unajifunza mengi sana kuliko kusubiri mpaka umalize kujenga japo si kila mtu atajenga nyumba kwa muda mrefu,kama hela ipo jenga fasta umalize then uingie kwenye biashara mazima ukiwa kwako stress free.
Paragraph number 1 pumba tupu, hope utakuwa na vitz...............

Paragraph number two well said..........
 
Anyway topic hii ina mambo mengi ambayo ni variable from mtu na mtu,1.mazingira 2.Ability to take calculated risk 3.business knowledge 4.kipaumbele cha mtu kutokana na changamoto aliyonayo.5.opportunity available.n.k.but kwa mtizamo wangu, cash flow is first thing,yaani kufanya vitu ambayo vitaongeza mzunguko wangu wa fedha kwanza,na hapa ndo tunapotofautiana,mwingine anaona aanze na biashara bcz anaujuzi na uzoefu fulani kwake risk is very low,but some people bcz hana ujuzi na uzoefu wa biashara the best ni kutumia mshahara kujenga na kuridhika na kidogo,but financial freedom start with investment that will insure positive cash floww then spending but not all can afford this.

This is the best reply.

Kufanya hayo maamuzi inategemea na;
1. Mazingira
2. Uwezo wa mtu/kipato
3. Msukumo wa ndani
4.
 
Asante kitulo kwa comment yako nzuri,inatupasa tufikiri vizuri ndani na nje ya box,Maana ya uchumi ni kutumia rasilimali ulizonazo kuongeza vitegauchumi/vitega pesa,kwa mtizamo wangu swali la msingi ni hili,kwa nini unanunua gari au kujenga nyumba? je kwa kununua gari au kujenga nyumba kutakufanya usave/upunguze matumizi yako kwa kiasi gani?.Kwa huyo jamaa yako wa songea,mimi namuona ni mchumi,alisave kodi ya nyumba pia kupitia nyumba aliongeza mapato this is what we taking about,kununua gari au kujenga nyumba kwanza is not any issue,hoja hapa ni kwamba nyumba au gari vitakuingizia mapato kwa kiasi gani?.MAFANIKIO YA KIUCHUMI, IS NOT STRUGGLING TO GATE WHAT WE HAVEN'T BUT IT IS STRUGGLING TO USE WHAT WE HAVE.
 
Malenga wetu,unachosema ni kweli,ktk land na nyumba,kuna appreciation every year,lakini kumbuka appreciation value is non cash iteam unaweza kuwauliza wahasibu wanafahamu,so kama una nyumba appreciation value haiingii mfukoni wako mpaka uuze nyumba/land so unaweza ukawa na nyumba/land but mfukoni huna pesa na shida nyingi zinataka pesa.kwa upande wa kodi ya nyumba kila mwaka kodi inapanda but investment za nyumba zinachukua muda mrefu sana 10-15 yrs to return investment capital unless uwe na nyumba nyingi za biashara na makazi.But kwa watu ambao bado hatuna ujuzi wa biashara na uwekezaji kujenga nyumba is bliliant idea.But if your are risk taker,short term investment ni nzuri kwa mtu ambaye ana mtaji mdogo na ana mahitaji makubwa ya pesa ndani ya muda mfupi.
 
Mtoa mada umeeleza vizuri sana, that are ideas of a matured person.
 
Back
Top Bottom