Kwanini niuze simu?

Kwanini niuze simu?

mathsjery

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Posts
2,249
Reaction score
1,813
Kumekuwa na mawazo mengi yanayotolewa hapa jukwaani na baadhi ya wadau kwa watu wenye uhitaji wa aina hiyo.

Moja ya wazo huwa najiuliza sana ni kwanini linatolewa sana ni hili.

Uza simu.

Uza simu kanunue karanga tembeza vyuoni na saiti.

Uza simu kanunue mitumba na viatu pale sijui wapi saa 12 asubuhi viatu ni 2000tsh/pair

Nakadhalika na kadhalika.

Swali langu je ni kweli kuuza simu ndo suluhisho?
Hakuna kazi zingine zisizo ingilia mawasiliano ya mtu?

Maanake kuna jamaa kauza godoro la sita kwa sita yale ya Dodoma kwa laki mbili kwa kuwa kapitia mpito sasa analala kwenye Chaga na pesa haijamsaidia bado anabangaiza godoro halina hata miezi mitatu
 
Labda wamatekeleza ule msemo "if you want to be full you must be empty"
 
Inategemea lakini,kimfaacho mtu chake.kama kuna issue inaitaji upate pesa ili upige hatua flani kwenye maisha ukakosa iyo pesa,na simu yako inauzika basi uza tu,pesa uatakayo pata unachukua kiswaswadu cha kujishkiza.
Kuna watu wanapitia changamoto nyingi za maisha hata akikwambia basi utamshauri tu auze tu akuna namna.
 
Sasa umeambiwa uuze simu, hàpo unajiongeza wewe kamà kweli ukiuza simu utatatua tatizo au utaongeza tatizo?

Unapopewa ushauri humu pindi upatapo shida unàtakiwa na wewe kuuchuja kama ni wa faida au LA.

Wengine ni kufurahisha genge tu.
 
Kumekuwa na mawazo mengi yanayotolewa hapa jukwaani na baadhi ya wadau kwa watu wenye uhitaji wa aina hiyo.

Moja ya wazo huwa najiuliza sana ni kwanini linatolewa sana ni hili.

Uza simu.

Uza simu kanunue karanga tembeza vyuoni na saiti.

Uza simu kanunue mitumba na viatu pale sijui wapi saa 12 asubuhi viatu ni 2000tsh/pair

Nakadhalika na kadhalika.

Swali langu je ni kweli kuuza simu ndo suluhisho?
Hakuna kazi zingine zisizo ingilia mawasiliano ya mtu?

Maanake kuna jamaa kauza godoro la sita kwa sita yale ya Dodoma kwa laki mbili kwa kuwa kapitia mpito sasa analala kwenye Chaga na pesa haijamsaidia bado anabangaiza godoro halina hata miezi mitatu
Tushaulizwa swali kama Hilo na lecture wa economics kuuza Mali yako wakati wa shida ni way out ya kutatua tatizo linalo kukabili but unatakiwa ufanye uchambuzi je hio Mali yako ni asset or liability. Kama huna source of income simu especially smartphone ni liability coz yenyewe tu Ili kuzitumia unahitaji uwe na pesa ya kununua credit so kuuza ktk mazingira hayo ni swala ambalo ni zuri lakin kama wewe ni mkulima unapouza shamba mind that you made a wrong choice ko kama inatumia simu kupata kipato ni kosa vinginevyo ni sawa

Sent from my SH-04H using JamiiForums mobile app
 
We wala usiuze simu yako mkuu. We kaa nayo tu uwe unaomba omba vocha ukipata unatulia zako sebuleni kwa shemeji unaanza kutuma msg kwenye magrupu na JF unalalamika maisha magumu na unalalamika serekali haikujali na bila kusahau unalalamika huna mtaji.

Utauzaje simu?
 
Haikuhusu wewe mwenye smart kitochi,
Hiyo Ina maanisha Kama unamiliki cm ya laki tatu unaweza uza hata laki na nusu laki ikawa mtaji na hamsin ukawa na cm ndogo.
Ishu inakuja Kuna aina ya biashara kufanya inapaswa kuwa na roho ya paka hasa kwa Hawa watoto wanaotoka chuo wanaoambiwa wajiajiri.
 
Nyoongeza hapo kaka "huwezi tatua tatizo Kwa njia zile zile zilizokuleta tatizo"

Sent from my SH-04H using JamiiForums mobile app
 
Labda kwa biashara uliyoanzisha ina wateja ila huna mtaji wa kutosha. Uza chochote ila uwe na nidhamu ya pesa, utatoboa.
 
We wala usiuze simu yako mkuu. We kaa nayo tu uwe unaomba omba vocha ukipata unatulia zako sebuleni kwa shemeji unaanza kutuma msg kwenye magrupu na JF unalalamika maisha magumu na unalalamika serekali haikujali na bila kusahau unalalamika huna mtaji.

Utauzaje simu?
Mkuu@kambaku naona umemjibu ipasavyo mtoa mada maana alichokiuliza kinaendana na IQ yake na uwezo wa kufikiri pia!![emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom