GE2025 Kwanini Nyerere aliuchukulia urais katika muktadha wa Ufalme?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Sio tu katika katiba ya nchi ambapo Mwl Nyerere aliujenga urais katika hadhi ya ufalme bali pia hata katika maongezi yake na utamaduni ni hivyo pia. Nyerere aliwajengea raia mtizamo kwamba watu kutaka kuwa rais au kuwa na ndoto hizo ni kama aina fulani ya dhambi hivi, kwamba urais huwa unaenda kwa mtu aliyepangiwa na Mungu kama upakwa mafuta tu na hakipaswi kuwa kitu cha kutafutwa kwa juhudi. Nyerere aliichukulia Ikulu kama mahali patakatifu pia! Hii ni dhana ya ufalme.

Legasi yake iko hadi kwa raia wa kawaida leo hii, mtu akionyesha nia au harakati za kuwa Rais kwa njia za kidemokrasia na halali kabisa ataambiwa ana tamaa ya madaraka, ataambiwa urais sio wa kila mtu, ataonekana kama muhaini na mvurugaji n.k Hili jambo linawarudisha nyuma sana watu wenye potential kubwa ya kuwa viongozi bora wa kuongoza taifa hili na kulifikisha katika ukuu wake.

Mtizamo wa mwalimu Nyerere kuwa hivi ulitokana na nini hasa?

Ni kwa sababu alitoka katika familia ya chifu, ni imani ya kidini au aliona hii ndio namna ya kujenga nchi bora?
 
Sio tu katika katiba ya nchi ambapo Mwl Nyerere aliujenga urais katika hadhi ya ufalme bali pia hata katika maongezi yake na utamaduni ni hivyo pia. Nyerere aliwajengea raia mtizamo kwamba watu kutaka kuwa rais au kuwa na ndoto hizo ni kama aina fulani ya dhambi hivi, kwamba urais huwa unaenda kwa mtu aliyepangiwa na Mungu kama upakwa mafuta tu na hakipaswi kuwa kitu cha kutafutwa kwa juhudi. Nyerere aliichukulia Ikulu kama mahali patakatifu pia! Hii ni dhana ya ufalme. Legasi yake iko hadi kwa raia wa kawaida leo hii, mtu akionyesha nia au harakati za kuwa Rais kwa njia za kidemokrasia na halali kabisa ataambiwa ana tamaa ya madaraka, ataambiwa urais sio wa kila mtu, ataonekana kama muhaini na mvurugaji n.k

Mtizamo wa mwalimu Nyerere kuwa hivi ulitokana na nini hasa?
Ni kwa sababu alitoka katika familia ya chifu, ni imani ya kidini au aliona hii ndio namna ya kujenga nchi bora?
alikuwa tapeli tu mkuu
 
Sio tu katika katiba ya nchi ambapo Mwl Nyerere aliujenga urais katika hadhi ya ufalme bali pia hata katika maongezi yake na utamaduni ni hivyo pia. Nyerere aliwajengea raia mtizamo kwamba watu kutaka kuwa rais au kuwa na ndoto hizo ni kama aina fulani ya dhambi hivi, kwamba urais huwa unaenda kwa mtu aliyepangiwa na Mungu kama upakwa mafuta tu na hakipaswi kuwa kitu cha kutafutwa kwa juhudi. Nyerere aliichukulia Ikulu kama mahali patakatifu pia! Hii ni dhana ya ufalme.

Legasi yake iko hadi kwa raia wa kawaida leo hii, mtu akionyesha nia au harakati za kuwa Rais kwa njia za kidemokrasia na halali kabisa ataambiwa ana tamaa ya madaraka, ataambiwa urais sio wa kila mtu, ataonekana kama muhaini na mvurugaji n.k Hili jambo linawarudisha nyuma sana watu wenye potential kubwa ya kuwa viongozi bora wa kuongoza taifa hili na kulifikisha katika ukuu wake.

Mtizamo wa mwalimu Nyerere kuwa hivi ulitokana na nini hasa?
Ni kwa sababu alitoka katika familia ya chifu, ni imani ya kidini au aliona hii ndio namna ya kujenga nchi bora?
Your observation runs counter to this Video: Jinsi Baba wa taifa Nyerere Alivyoweka Msingi wa Uchaguzi wa Mgombea Rais wa CCM
 
Mtizamo wa mwalimu Nyerere kuwa hivi ulitokana na nini hasa?
Kwani wewe kwa maoni yako unafikiri urais ni nafasi anayo iPata mPuuzi yeyote mradi tu ameitaka?
Huoni haya yanayotokea sasa hivi; au unataka vielelezo vya namna gani?

Ndiyo, kwa mwendelezo wa mawazo hayo hayo ," ikulu ni mahali Patakatifu", siyo mahali Pa kwenda kuchezea na kuvuruga hali ya nchi na mali zake. Hadhi ya taifa lolote inaanzia Ikulu.

Hayo mawazo ya "ufalme" unayaona hivyo wewe, lakini Mwalimu hakuongoza wala kuishi kifalme.
 
Nyerere ndio ndie muasisi mkuu wa umasikini wa hii nchi,tamaa zake za madaraka zinatuumiza hadi leo
Wewe ni kasuku, au robot lililowekewa 'software' kutaPika tu lililowekewa?
 
Ipo kiimani zaidi, Nyerere alikuwa padri aliyechangamka

Ila ukichunguza kwa kiasi chake watu wanaokulia kwenye malezi ya kiseminari(kama nyerere) lazima dhana ya Ufahamu wa kikristo ikae akilini mwao

Mfano: kiongozi mkuu kwenye dhana ya ukristo(Yesu) anafundisha, anayetaka kuwa mkuu kati yenu ajitoe kuosha miguu ya maamuma wasio na shukrani.!

Yeye(nyerere) akiamka asubuhi ikulu anakuta chai kaandaliwa suti safi na usafiri juu na ratiba yake ya siku ikifuatwa kama alivyoamuru.! Weka Mbali mishahara yao wanayoita wenyewe posho

Kwanini nafsi isimsute na kutoa onyo kwa yeyote anayepapigania.! Pana ulevi pale
 
Kosa la Nyerere lilikuwa ni lile la kufikiri Ujamaa ndiyo mfumo bora kabisa wa kisiasa na maisha ya jumla ya wananchi, kuliko ubepari! Na hapa ndipo alipo haribu kila kitu. Role model wake China baada ya kuona kuna mambo mazuri pia kwenye ubepari, kwenye miaka ya 1970's waliona ni bora wachukue mazuri ya Ujamaa na mazuri ya Ubepari; na mwisho wa siku ikaja kuzaliwa hii China ya sasa!

Yeye alijifanya mbishi huku akiamini Ubepari ni unyonyaji tu! Na wakati una mambo yake mengine mazuri tu yakiwemo haya ya demokrasia na uhuru wa wananchi kwenye kujiamulia mambo yao.

Ona sasa ametengeneza Katiba ya Kijamaa ya mfumo wa chama kimoja! Katiba ya kumtukuza mtu mmoja (Rais na mwenyekiti wa chama)! Katiba inayotambua uwepo wa chama dola! Katiba inayowalazimisha watumishi wote wa umma kuwa makada wa chama dola!

Na matokeo yake ndiyo haya sasa.
 
Uoga na kutojiamini kwake JK.
 
Kwani wewe kwa maoni yako unafikiri urais ni nafasi anayo iPata mPuuzi yeyote mradi tu ameitaka?
Huoni haya yanayotokea sasa hivi; au unataka vielelezo vya namna gani?

Ndiyo, kwa mwendelezo wa mawazo hayo hayo ," ikulu ni mahali Patakatifu", siyo mahali Pa kwenda kuchezea na kuvuruga hali ya nchi na mali zake. Hadhi ya taifa lolote inaanzia Ikulu.

Hayo mawazo ya "ufalme" unayaona hivyo wewe, lakini Mwalimu hakuongoza wala kuishi kifalme.
Sioni kama Kambona, Malecela, Kolimba, Warioba, Mrema, Salim Ahmed Salim, Mwandosya na Lowassa walikuwa watu wapuuzi, nafikiri hawa ndio waliofaa zaidi na wangeweza kutuongoza kama wangekuwa na jitihada za kutosha kuupambania urais. Sioni pia kama wakina Mpina, Lissu, Mpango, Mbowem, Zitto n.k ni watu wa hovyo na nafikiri wangefaa zaidi.
 
Kosa la Nyerere lilikuwa ni lile la kufikiri Ujamaa ndiyo mfumo bora kabisa wa kisiasa na maisha ya jumla ya wananchi, kuliko ubepari! Na hapa ndipo alipo haribu kila kitu. Role model wake China baada ya kuona kuna mambo mazuri pia kwenye ubepari, kwenye miaka ya 1970's waliona ni bora wachukue mazuri ya Ujamaa na mazuri ya Ubepari; na mwisho wa siku ikaja kuzaliwa hii China ya sasa!

Yeye alijifanya mbishi huku akiamini Ubepari ni unyonyaji tu! Na wakati una mambo yake mengine mazuri tu yakiwemo haya ya demokrasia na uhuru wa wananchi kwenye kujiamulia mambo yao.

Ona sasa ametengeneza Katiba ya Kijamaa ya mfumo wa chama kimoja! Katiba ya kumtukuza mtu mmoja (Rais na mwenyekiti wa chama)! Katiba inayotambua uwepo wa chama dola! Katiba inayowalazimisha watumishi wote wa umma kuwa makada wa chama dola!

Na matokeo yake ndiyo haya sasa.
Lakini ujamaa wa China uongozi ulikuwa unapatikana kwa ushindani mkali sana na hata kuna wakati walitaka kumtoa madarakani Mao na Deng, pia hata wakati huu wa Xi Jinping kuna wabishi ndio maana anapambana kuwa prune.
 
Sio tu katika katiba ya nchi ambapo Mwl Nyerere aliujenga urais katika hadhi ya ufalme bali pia hata katika maongezi yake na utamaduni ni hivyo pia. Nyerere aliwajengea raia mtizamo kwamba watu kutaka kuwa rais au kuwa na ndoto hizo ni kama aina fulani ya dhambi hivi, kwamba urais huwa unaenda kwa mtu aliyepangiwa na Mungu kama upakwa mafuta tu na hakipaswi kuwa kitu cha kutafutwa kwa juhudi. Nyerere aliichukulia Ikulu kama mahali patakatifu pia! Hii ni dhana ya ufalme.

Legasi yake iko hadi kwa raia wa kawaida leo hii, mtu akionyesha nia au harakati za kuwa Rais kwa njia za kidemokrasia na halali kabisa ataambiwa ana tamaa ya madaraka, ataambiwa urais sio wa kila mtu, ataonekana kama muhaini na mvurugaji n.k Hili jambo linawarudisha nyuma sana watu wenye potential kubwa ya kuwa viongozi bora wa kuongoza taifa hili na kulifikisha katika ukuu wake.

Mtizamo wa mwalimu Nyerere kuwa hivi ulitokana na nini hasa?

Ni kwa sababu alitoka katika familia ya chifu, ni imani ya kidini au aliona hii ndio namna ya kujenga nchi bora?
Nyerere alikuwa sahihi.

Kwasababu mtu akiwa Ikulu anatakiwa kuumia na kuumiza kichwa kwaajili ya shida za watu.

Ikulu siyo sehemu ya DEALS, BIASHARA, STAREHE na KUTUMIA MADARAKA KUUA WATU, KUFIRA, na KUTEKA WATU.

Hakuna mtu mwema anayetamani kubeba shida za watu, kwa kuhonga watu ili aende IKULU.
 
Back
Top Bottom