GE2025 Kwanini Nyerere aliuchukulia urais katika muktadha wa Ufalme?

GE2025 Kwanini Nyerere aliuchukulia urais katika muktadha wa Ufalme?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Lakini ujamaa wa China uongozi ulikuwa unapatikana kwa ushindani mkali sana na hata kuna wakati walitaka kumtoa madarakani Mao na Deng, pia hata wakati huu wa Xi Jinping kuna wabishi ndio maana anapambana kuwa prune.
Xi Jinping anadeal na wala rushwa na wahujumu. Ni kunyongwa au kufungwa maisha haina mjadala​
 
Sioni kama Kambona, Malecela, Kolimba, Warioba, Mrema, Salim Ahmed Salim, Mwandosya na Lowassa walikuwa watu wapuuzi, nafikiri hawa ndio waliofaa zaidi na wangeweza kutuongoza kama wangekuwa na jitihada za kutosha kuupambania urais. Sioni pia kama wakina Mpina, Lissu, Mpango, Mbowem, Zitto n.k ni watu wa hovyo na nafikiri wangefaa zaidi.
Kumbe kuchanganyikiwa kwako kunaanzia huku?
Ndiyo maana sikuielewa mada yako ililenga nini hasa nilioisoma kwa mara ya kwanza.

Sasa nieleze kama hao wote ulio wataja walizuiwa na "ufalme" wa Mwalimu Nyerere kuuPigania uongozi.
Jieleze bila kujichanganya mwenyewe.
Jieleze "walifaa zaidi" kwa viPi; na walizuiwa na nani?

Akina Kikwete, Mwinyi, Magufuli, MkaPa, Samia, wao hawakuzuiwa kwa vile ni sehemu ya warithi wa "kifalme"? Tueleze tofauti ya hawa na hao uliowataja nini?

Ni Mwl Nyerere ndiye amewakataza akina Zitto, Mango, Luhaga, MPina wasigombee urais. Umewasiliana nao wakakueleza kwamba hawawezi kugombea kwa sababu ya "mfumo" wa kifalme uliotengenezwa na Mwl Nyerere?

Ni kama unajieleza kuwa waTanzania wote wametengenezwa kuwa mateka wa Mwl. Nyerere, kiasi kwamba hata bila yeye kuweo miaka zaidi ya 20 watu hawa wanaendelea tu kujiweka ndani ya umateka!

Sasa niambie, mtu ukiwa mwenye akili nzuri, kama ulivyo wewe utaamini vii mawazo ya namna hii?
Na ukaona uoteze muda wako kuanzisha mada juu yake!
 
Au unaonaje? Maana hii tabia ya watu kushindwa kimaisha na kumtafuta wa kumtupia lawama imezidi sana.Mtu Hana ulemavu wowote na ana fursa nzuri lakini ni msingiziaji class one!
Ni vigumu kujuwa msukumo wa baadhi ya hawa watu unatokana na nini; kushikilia uchungu moyoni miaka yote hii.
 
Back
Top Bottom