Ndiyo ni kweli kabisa hususan pale inapotokea badiliko kwenye bei za vifaa, gharama ya usafirishaji, uaminifu na umakini wa mafundi.
Haiwezekani ukawepo site muda wote kama nyapara/msimamizi saa zote kwani wewe binafsi pia unayo majukumu mengine muhimu.
Halafu usisahau pia kwamba, kwa bahati mbaya baadhi ya vifaa vinaweza kuharibika e.g. kuvunjika kwa ceiling boards(Gypsum boards), sink za vyooni, Vioo au kitasa kuwa ni kibovu n.k. Tena inawezekana ukalazimika kubomoa sehemu fulani ambayo imejengwa vibaya au unataka kufanya maboresho katika ramani yako. Mambo ni mengi yanayoweza kuyumbisha bajeti ya awali kiasi kwamba ile 25% uliyoweka kama tahadhari ikaisha na bado isitosheleze.