Kwanini nyumba ikifika hapa inakuwaga ngumu kumalizia?

Kwanini nyumba ikifika hapa inakuwaga ngumu kumalizia?

Ni risky sana utaratibu huo (na nimeshuhudia)kwani ikitokea kwamba mmiliki wa hardware ulikolimbikiza fedha zako akifariki au hardware ikapata ajali e.g. kuungua moto, utapata wakati mgumu sana ku-claim fedha zako ulizowekeza kwake. Lakini pia na wewe unaweza kupata changamoto ya kimaisha. Ni bora ukawekeza benki ambako utapata na kafaida fulani kuliko kwa mtu baki i.e. hardware.
Mkuu ukilipa si unapewa risiti??

Mmiliki akifariki ndio mwisho wa huduma? 😃

Duuh umewaza mbali, kwakweli mie kwangu hii ilikua rahisi sana ndani ya mwezi nlikua nshawapa hela ya kutosha kazi ilikua kufata material tu hadi nkajihisi kama najenga bure. Hizo risk sikuzipa kipaumbele ila pia kuna mambo ukiyapa kipaumbele mkuu hupigi hatua.
 
Kudundulizia mfukoni ni ngumu, inatakiwa kudundulizia hardware.....

Ukipata kiasi unapeleka hardware kama wana lipa namba ndo kabisa haupati uvivu, ukipata tu unatuma, ukipata kiasi unatuma unashangaa mara ya kupaua imetimia.
Hii inaweza kuwa njia nzuri, lasivyo tutakimbilia kwenye uzi wa kimasihara
 
Ndivyo ilivyo, gharama za ujenzi zinabadilika kulingana na location kilipo kiwanja, muinuko/msawazo wa kiwanja, sehemu unayojenga either mjini au kijijini, accessibility ya eneo lako kwa ajili ya kupitisha materials, nature ya wakazi wa eneo hilo/majirani(wengine ni wachawi wa maendeleo), upatikanaji wa usafiri k.v boda, toroli, kenta n.k

Hivyo vitu hapo juu vinaweza kuku-suplize na mfumuko wa gharama za ujenzi hadi uje ushangae labda waliokupigia tathimini walikuwa mazwazwa au ukawashutumu mafundi kuwa wamekuibia

Kuna location moja nilianza msingi aisee ziliingia tofali za kutosha na kokoto pamoja na cement hadi niliishiwa pumzi. Wakati huo ulikuwa kiangazi mvua zilivoanza na kulikuwa ni bondeni kidogo kumbe ule udongo wa pale unatitia ukuta wa nyuma wa msingi ukatengeneza nyufa na kuachana na kingo za mbele yaani ikabidi nianze upyaa
Exactly. Ujenzi wa nyumba ni mchakato unaobadilika-badilika sana na wenye kustahili uvumilivu wa kiwango kikubwa. Ndo mana wanasema ujenzi wa nyumba yako huwa hauishi/haumaliziki 100%. Unaweza kufanya extension unaweza kubadili sakafu n.k.n.k. na ukiona mtu amekaa/anaishi kwenye nyumba yake alojenga mwenyewe, mpe heshima yake.
Ila Tahadhari: Usijenge nyumba yako kwa mali/gharama za kudhulumu - Utaikamilisha ndio; lakini Haitadumu kamwe.
 
Mkuu ukilipa si unapewa risiti??

Mmiliki akifariki ndio mwisho wa huduma? 😃

Duuh umewaza mbali, kwakweli mie kwangu hii ilikua rahisi sana ndani ya mwezi nlikua nshawapa hela ya kutosha kazi ilikua kufata material tu hadi nkajihisi kama najenga bure. Hizo risk sikuzipa kipaumbele ila pia kuna mambo ukiyapa kipaumbele mkuu hupigi hatua.
Utapewa risiti tena risiti halali kabisa ila usumbufu utakuja pale Mrithi wa mali ya marehemu atakapoanza mchakato wa kufuatilia mali za marehemu ww utasimama kusubiri na pengine hoja au mtafaruku baina ya mrithi na ndugu zake utazuka n.k. Lazima kutakuwepo na kuyumba kwa namna fulani katika malengo yako.
 
Utapewa risiti tena risiti halali kabisa ila usumbufu utakuja pale Mrithi wa mali ya marehemu atakapoanza mchakato wa kufuatilia mali za marehemu ww utasimama kusubiri na pengine hoja au mtafaruku baina ya mrithi na ndugu zake utazuka n.k. Lazima kutakuwepo na kuyumba kwa namna fulani katika malengo yako.
Daaah, mie haya mawazo kwakweli siyapi kipaumbele niwe mkweli.....sitafanya chochote nikiwaza hivyo, sasa hata ukijenga bahati mbaya nyumba ikianguka je?? Kwahiyo tusijenge 😁

#no negatives my 1st rule
 
Daaah, mie haya mawazo kwakweli siyapi kipaumbele niwe mkweli.....sitafanya chochote nikiwaza hivyo, sasa hata ukijenga bahati mbaya nyumba ikianguka je?? Kwahiyo tusijenge 😁

#no negatives my 1st rule
Uko sahihi ila ukumbuke kuzingatia pia kuna risk management na disaster preparedness. Usipuuzie hayo halafu yakitokea ukaja kusema ningelijua.........
Cha msingi hapo ni jenga huku ukikumbuka hayo yanaweza kutokea na ukachukua tahadhari/ukajiandaa kukabiliana endapo yakitokea. Yasipotokea unamshukuru Mungu.
 
Na wengi wakikwama huamua kuuza
Hapo ndio ardhi inakua na thamani kuliko Pagala, na huwezi kuita nyumba

Wajenzi wangekuwa wanawapa hints
 
Ukisha pata ramani ya nyumba, ijengee chini ( account) kwanza ndio uihamishie site

Ramani inakuonesha idadi nzima ya milango na madirisha( kimbembe kilipo) , matofali( haya sio ishu sanaana), cement, mchanga, kokoto, mbao, mabati n. K
 
Kuta ninaweza kupiga hata 3 kwa mpigo, ngoma ipo hapo kwenye kupaua.

Kuna mshikaji alikuwa mgodini mikwara mingi. Akanunua viwanja vitatu na kuanza kujenga vyote. Alipomaliza maboma wakamfukuza kazi. Mpaka leo zile nyumba hazikusogea zaidi ya miaka 9.
 
Si kweli ,watu wanatembea na nyumba mfukoni....Kuna Jamaa yupo State ,alikuja ndani ya miezi mitatu alimalzia mjengo kila kitu ,hakusimama hata hatua moja ilikuwa mwanzo mwenga kuanzia msingi kupaua ,finishing ,perving ,garden ,umeme ,maji ,fense.
Siyo suala la kuwa kule State, ni suala la wewe kujipanga mapema kifedha katika suala zima la ujenzi wa nyumba.
Unaweza kuwa mtu wa State na ukashindwa kujenga nyumba.
 
Na hapo ni bado....ikianza misele ya finishing ni ngumu zaidi....nadhani gharama huwa zaidi ya kuinua boma!
 
Nguvu ya kuanzia msingi hadi kwenye lenta inakuwaga ya kasi san,a kuanzia hapo hadi kumalizia wengi hurudi nyuma nini shida?

View attachment 3086249
Hapa tatizo kubwa ni kujipanga. Ukishajenga msingi,Kusimamisha boma ni kazi rahisi sana lakini tatizo huanzia kwenye kupaua kama hujajipanga.
Ukitaka ujenzi usikutese sana basi uwe unaanza kununua mahitaji ya ujenzi kabla hujafikia hatua ya mbele.
Mfano ukishajenga msingi anza kununua(kulipia) bati au mbao ili unapofikia hatua ya Kupandisha tofali unakuwa huna presha ya kupaua.
 
Back
Top Bottom