Mimi fundi alinipigia kuwa tatumia mbao mia mbili...lakini mpaka anamaliza kupaua nilitumia mbao zaidi ya miatatu....
Nikimuuliza vipi mbona ulikadiria kidogo akaishia kucheka,akasema "boss ningekuambia mbao mia tatu usingekubali tuanze kazi"...
Ujenzi ni process kwani unapanga hiki mara kinatokea kingine....
Bahati nzuri kuhusu bati nilikua nanunua mdogo mdogo huko nyuma,nilinunua bati nyingi hadi nyingine zilibakia😂😂
Fundi aliekadiria bati alizidisha makadirio.
NILICHOJIFUNZA
Vijana wengi tunaishi kwa matumaini ya kuwa na pesa nyingi huko mbeleni lakini inaweza kuwa si kweli...
Kama una kiwanja anza kujenga na hizo hizo laki mbili zako unazopata.
Punguza matumizi yasiyo na ulazima.
Nikipiga thamani ya nyumba yangu hadi sasa ni kama milioni 50 lakini sijawahi shika hata milioni 10 cash na wala sijajenga kwa mkopo na sidaiwi na mtu yoyote....
Kujenga ni process na inahitaji uvumilivu