daraja la kigamboni
JF-Expert Member
- Apr 28, 2016
- 3,127
- 3,062
Hii point nimeichukuaTafizo binadamu mbwembwe nyingi mnoooo. Mara sijui choo cha million tatu tile 120.000 per sqm. Wewe jenga kwa uwezo wako basi.
Pagumu kupau tuu kwenye ujenzi maana inahitajika hela ya mkupuo.
Kwengine kote easy tuu.
Uita fundi maikl anatemgeneza chumba kimoja baada ya miezi mitatu akuja kutegeneza chingine
Siyo hatua zote ni ngumu kumalizia. Hatua ngumu hapo ni kuweka paa tu kwa sababu inahitajika hela za pamoja ili kuweka paa tofauti na huko nyuma ulikuwa unaweza kujenga boma kidogo kidogo na hakuna madhara. Ila hauwezi kuweka nusu paa japo watu wanafanya.Nguvu ya kuanzia msingi hadi kwenye lenta inakuwaga ya kasi san,a kuanzia hapo hadi kumalizia wengi hurudi nyuma nini shida?
View attachment 3086249
Hapa umeongea jambo la msingiChukua mkopo ili umalizie kujenga usichukue ili uanze kujenga utakuja nishukuru
KweliMimi fundi alinipigia kuwa tatumia mbao mia mbili...lakini mpaka anamaliza kupaua nilitumia mbao zaidi ya miatatu....
Nikimuuliza vipi mbona ulikadiria kidogo akaishia kucheka,akasema "boss ningekuambia mbao mia tatu usingekubali tuanze kazi"...
Ujenzi ni process kwani unapanga hiki mara kinatokea kingine....
Bahati nzuri kuhusu bati nilikua nanunua mdogo mdogo huko nyuma,nilinunua bati nyingi hadi nyingine zilibakia😂😂
Fundi aliekadiria bati alizidisha makadirio.
NILICHOJIFUNZA
Vijana wengi tunaishi kwa matumaini ya kuwa na pesa nyingi huko mbeleni lakini inaweza kuwa si kweli...
Kama una kiwanja anza kujenga na hizo hizo laki mbili zako unazopata.
Punguza matumizi yasiyo na ulazima.
Nikipiga thamani ya nyumba yangu hadi sasa ni kama milioni 50 lakini sijawahi shika hata milioni 10 cash na wala sijajenga kwa mkopo na sidaiwi na mtu yoyote....
Kujenga ni process na inahitaji uvumilivu
Mkuu, fafanua kitaalamu. Binafsi nimeyapenda.Hayo madirisha nimecheka sana😀
Sababu ni kuwa kuanzia hapo, vitu vingi ni lazima ufanye kwa mara moja.. mfano, huwezi kupiga kenchi au kupaua kwa kidogo kidogo, au kupiga rangi mara nyingi kazi hizo zikianza inabidi umalize hivyo zinahitaji hela nyingi kwa wakati mmoja.Nguvu ya kuanzia msingi hadi kwenye lenta inakuwaga ya kasi san,a kuanzia hapo hadi kumalizia wengi hurudi nyuma nini shida?
View attachment 3086249
Hata me nimeliona hiloMwisho wa yote, hiyo kazi imenyooka sana. Heshima kwao mafundi.