Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,383
Hiyo link nimeisoma ila imejaa upotoshaji mtupu hasa pale wanapolazimisha kuwa kanisa la SDA linapinga Uungu wa Roho Mtakatifu, na pia Mungu Mwana. huu ni uongo na upotoshaji wa wazi.Katika misingi ya imani ya SDA, utatu mtakatifu ni nguzo ya kwanza kabisa. Kwa kuwasaidia tu kwa kipindi chote cha robo hii ya mwaka kuanzia January hadi March kanisa linaendelea na muongozo wa kujifunza Biblia, mada kuu ni kuhusu Roho Mtakatifu.Leo kulikuwa na mjadala mzuri sana kituo cha Radio cha Morning Star FM 105:3.Kuhusu Uungu wa Roho Mtakatifu.Mjadala unaendelea kila jumatatu hadi alhamisi kuanzia saa 12 hadi saa 1 jioni.Ijumaa mjadala hufanyika kwa lugha ya kiingereza.Kwa Neema ya Yesu nategemea kushiriki mjadala siku ya ijumaa.Sogea karibu na redio upate mafundisho ya Mungu hasa nini Wasabato wanaamini kuhusu Mungu Roho Mtakatifu kwa mujibu wa Biblia. Karibuni sana, achaneni na hadithi za kutunga kwenye mitandao.Mkuu mbona umeng'ang'ania hapo kwenye hizo ngonjera za zamani za Ellen G White...??
Hiyo link umepitia..? Umeisoma..?
Mnadiriki kubadilisha Biblia..?