Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa Kanisa Katoliki?

Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa Kanisa Katoliki?

Bikira Maria hana dhambi kama tulivyo sisi wengine.
Malaika alimwambia Bikira Maria kuwa amebarikiwa kuliko wanawake wote, hivyo basi, Bikira Maria ni mtakatifu. Kwa utakatifu huo bila shaka yuko mbinguni.
Ndiyo maana tunamwomba atuombee sisi wakosefu.
 
Bikira Maria hana dhambi kama tulivyo sisi wengine.
Malaika alimwambia Bikira Maria kuwa amebarikiwa kuliko wanawake wote, hivyo basi, Bikira Maria ni mtakatifu. Kwa utakatifu huo bila shaka yuko mbinguni.
Ndiyo maana tunamwomba atuombee sisi wakosefu.
Hakuna mwanadamu ambaye asili yake siyo dhambi,,, pia hiyo haimpi yeye kuwa intercessor,, intercessor ni Roho Mtakatifu pekee
 
Martin Luther alihama Kanisa Katoliki baada ya kutawaliwa na roho ya zinaa. Kutokana na Mapadri wakatoliki kutooa yeye kama mmojawapo wa kanisa Katoliki alilazimika kuachana na kanisa Katoliki ili kutimiza azma yake ya kuishi na mke.
Mtume Paulo anaeleza wazi kuwa, ni vema mtumishi wa Mungu asioe wala kuolewa, kwani hakuna mtu anayeweza kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmmoja kwani atampenda huyu na kumwacha au kumchukia mwingine.
Pia mtume Paulo anasema kuwa, kwa sababu ya ZINAA kila mtu na aoe au aolewe kuliko kuwaka tamaa.
Kwa hiyo Martin Luther aliachana na kanisa Katoliki Kutokana na kuzingirwa na roho ya ZINAA.
NB. Martin Luther ndiye chimbuko la KKKT.
 
Bikira Maria alikingiwa dhambi ya asili ili aje kumzaa Yesu ambaye alikuwa ni mtu kweli na Mungu kweli.
Yesu asingezaliwa na mama mwenye dhambi, ndiyo maana ilikuwa kwanza Bikira Maria akingiwe dhambi ya asili kama maandalizi ya kumzaa mkombozi.
 
Kama bikira maria yuko mbinguni je biblia inasema uongo juu yawatu waliokufa..maana biblia inasema yesu atakapo ludi atawaamusha waluo lala katika kiristo .. Inamaana watu waliokufa katika kiristo .. Sasa kama bikira wenu yuko mbingu pamoja nahao mnaowabandika utakatifu je wao hawata fufuliwa
 
Wapo watakaoamshwa mara Yesu ajapo, lakini siyo Bikira Maria.
Kwa kifupi ni kwamba, huwezi kumlinganisha Bikira Maria na mtu yeyote awaye yote.
Hata katika mazingira ya kawaida kabisa, MAMA wa mtu maarufu huheshimiwa sana, kwa mfano MAMA wa Rais wa nchi ni lazima ataheshimiwa karibu sawa na anavyoheshimiwa Rais mwenyewe.
Je, MAMA aliyemzaa Mkombozi (Mungu ) asiheshimiwe?
 
Kama mama wa laisi gani hapa kwetu tz anae eshimiwa au naww umetoka ndotoni
 
Mm nilisha waambia ninyi wa Rc mutuletee maandiko ya kibiblia yanayo kubaliana yakwamba bikira mariamu yuko mbinguni nikipatikana andiko moja linalokili hivyo siingii tena jf
 
Huyu bikira maria munae msema baada yakumzaa yesu aliendelea na maisha yake yy namumewe naakaendela kuza nakuzaa watoto wengi tu.ndomaana biblia inawatambua nduguze yesu..ukisoma biblia utawaona nduguzake yesu ..nahuyu bikira aliishi kama wengine nakisha akafa kama wengine ..hizi habali eti alipaa mbinguni niuongo uliopindukia naupaganani ..kama munabisha leteni maandiko ya kibiblia.. Sio blaha blaha
 
Hivi martin luther wa ihave a dream na na huyu wa kanisa ni watu wawili tofauti maana sjaelewaga jamn
 
Kwahiyo warc munataka kusema mwanzo wakainisa kathoriki ni bikira maria
 
Ndugu yangu, si kila kitu lazima kiandikwe kwenye Biblia. Kuna mambo ambayo yalitokea baada ya kuandikwe Biblia, hivyo mambo hayo ndiyo yanayoitwa MAPOKEO. Hata hivyo Biblia yenyewe inakiri kwamba kuna mambo mengi aliyoyatenda Yesu ambayo hayakuandikwa kwenye Biblia. Biblia inasema kuwa kama yangeandikwa mambo yote kwenye Biblia, Dunia ingejaa vitabu.

Lakini pia ni udhaifu wa hali ya juu sana wa FIKRA kutegemea kila kitu kiandikwe kwenye Biblia.
Binadamu ana akili na utashi, hivyo basi inatarajiwa kuwa Binadamu yeyote atumie pia akili zake kuambanua mambo kuliko kusubiri tu kuandikiwa na mtu mwingine.

MAPOKEO ni muhimu pia katika maisha yetu ya kawaida. Hata hawa wazazi wetu ni MAPOKEO. Ni MAPOKEO kwa sababu wewe mwenyewe huwezi kuthibitisha kuwa yule ni mama yako kwani huwezi kujua kuwa ni kweli ulizaliwa na yule mama au la?

Naomba kuwasilisha.
 
Habali za mapokeo yesu aziliyapiga malufuku .. Naakasema mufatamapokeo yawazee wenu nakuaacha maneno yangu yakweli..yaletayo uzuma ..
 
Acheni kulaghai watu kuweni wawazi biblia ndio msingi wa wakiristo sivinginevyo wala hayo mapokeo mnayo yafata
 
Biblia haikuandikwa na Kanisa Katoliki! Iliandikwa miaka mingi sana kabla ya uwepo wa Katoliki...Bibilia ilikuwepo kabla ya ujio wa Yesu.
Martin Luther King alileta mageuzi makubwa ya kiimani,ikumbukwe enzi hizo za utawala wa Rumi ilikuwa marufuku kwa mtu wa kawaida yaani mkristo wa kawaida kusoma Biblia badala yake wali dilute Biblia na kuanzisha Mithali za waumini!...enzi hizo msamaha ulikuwa unatozwa fedha tena fedha nyingi na wakati mwingine uliweza kulipia gharama fulani na kwenda kufanya maasi
Siku moja Martin Luther King akiwa anapita kwenye kitaa huko Ujerumani akaona kutabu kikubwa chenye jalada jeusi akakinunua,wakati anakisoma ndio akaona andiko kuwa kwa kupigwa kwake tumesamehewa Bure!
Akaanza kuhoji kwa wakubwa wa Vatican kwa nini watu walipishwe wakato msamaha ni Bure?hapo ndio mgigoro ulianza na kwa wakati huo Vatican wakaogopa kumwua maana ilikuwa miaka michache tangu wamwue Galileo Galilei

Nb soma 99 Thesis of Dr Martin Luther King
 
Biblia haikuandikwa na Kanisa Katoliki! Iliandikwa miaka mingi sana kabla ya uwepo wa Katoliki...Bibilia ilikuwepo kabla ya ujio wa Yesu.
Sijui kama unajitambua kweli wewe...?

Hata wakati wa Yesu Biblia kulikuwa hakuna...Biblia imekamilika mwaka 300 AD....Vitabu vyote vya Agano jipya vimeandikwa baada ya miaka na miongo mingi kupita toka Yesu Afufuke.. Sijui kama unalielewa hili..

Kingine Kanisa Katoliki ndio lime-compile Biblia Takatifu.....
 
Back
Top Bottom