Hamuwezi kupinga ukweli kuwa Kanisa Katoliki na papa wenu ndio mnyama wa ufunuo 13 na 14. Pia ndiye Kahaba Mkuu wa ufunuo 17:5.Anaitwa Kahaba mkuu kwa kupotosha Biblia Takatifu, wamejiundia Biblia yao imeongezwa maneno na vitabu visivyovuviwa na Roho Mtakatifu.Kanisa hili limehusika kutesa watakatifu na hivi karibuni litaibuka tena kupitia New World Order. Kanisa katoliki limejipa uhalali wa kuwa msemaji wa Mungu hapa duniani (kufuru). Kwa uzushi huo, wakisaidiwa na mataifa makubwa ikiwemo Marekani, watalazimisha dunia nzima wafuate mafundisho ya kiroma ikiwemo ibada ya siku ya kwanza ya juma yaani jumapili ambayo iliasisiwa na kanisa katoliki.Mtu awaye yote atakayekataa kutii sheria ya jumapili amri itatolewa auawe (Ufunuo 13:15-18). Daniel aliiliona hili anasema " kutatokea wakati wa taabu ambao mfano wake haujakuwepo tangu kuumbwa kwa dunia, lakini watu wa Mungu wataokolewa (Daniel 12:1). Yesu anasema " mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka" (Mathayo 24:13).