Ukimpiga DNA utashangaa ukiambiwa ana miaka 30 ! Waaafrica hawaaminiki , madaraka selemani aliandikwa CAF kuwa na miaka 25 wakati ukweli alikuwa na miaka 42 .
Mkuu kuweka rekodi sawa tu,Pogba alizaliwa na kukulia Ufaransa,huko Guinea anakusikia tu.
Kimpira amekuzwa na mfumo wa soka wa Ulaya,ni zao la academy za Roissy-en-Brie,Trocy na Le Havre pamoja na timu za taifa za France under 16,17,18,19,20 na sasa hii ya wakubwa.Pia amekuzwa academy ya Manutd.Amechezea Man utd na Juventus,klabu kubwa za soka barani Ulaya.
Iwapo unaweza kuthibitisha tatizo la umri kwa Pogba,basi itakuwa ni tatizo la mfumo wa soka wa Ulaya,na sio Africa.
Najiuliza ni kwanini umeamua kujump into asili ya Pogba kwenye technical issue uliyokuwa unaizungumzia,ilhali mchezaji huyu "kimpira" si mwafrika kabisa.
Hata hivyo,ni kweli huku Africa tuna changamoto zetu kwenye uendeshaji wa soka yetu,pamoja na yote,najivunia Uafrika wangu,najivunia Madaraka Selemani pia.Ana legacy yake kwenye soka yetu,kwa kiwango chetu,haijalishi alikuwa babu au katoto.