Kwanini Paul Pogba anasifiwa, mbona hana lolote?

Kwanini Paul Pogba anasifiwa, mbona hana lolote?

Mkuu.. Hivi sasa ndo kwanza ana miaka 23, hebu tumpe miaka 2 au 3 mbele, ndo tumuhukumu.
Ukimpiga DNA utashangaa ukiambiwa ana miaka 30 ! Waaafrica hawaaminiki , madaraka selemani aliandikwa CAF kuwa na miaka 25 wakati ukweli alikuwa na miaka 42 .
 
Hivi hilo ndilo la kumweka kwenye viwango vya dunia ? Kuna tatizo kubwa sana kwa wachambuzi wa soka wa Tanzania , ushindi wa jana wa France umechangiwa na timu kucheza kwa pamoja ( Total Football ).

Pogba hana uwezo wowote wa kuamua matokeo ya mchezo kama wafanyavyo akina messi au Ronaldo , ni mchezaji wa kawaida sana .
Haya mkuu.Nadhani tukubaliane kutokukubaliana.To me Pogba ni mmojawapo wa viungo bora kabisa duniani kwa sasa.Kwako wewe ni wa kawaida.Basi sawa.
 
Ukimpiga DNA utashangaa ukiambiwa ana miaka 30 ! Waaafrica hawaaminiki , madaraka selemani aliandikwa CAF kuwa na miaka 25 wakati ukweli alikuwa na miaka 42 .
Mkuu kuweka rekodi sawa tu,Pogba alizaliwa na kukulia Ufaransa,huko Guinea anakusikia tu.
Kimpira amekuzwa na mfumo wa soka wa Ulaya,ni zao la academy za Roissy-en-Brie,Trocy na Le Havre pamoja na timu za taifa za France under 16,17,18,19,20 na sasa hii ya wakubwa.Pia amekuzwa academy ya Manutd.Amechezea Man utd na Juventus,klabu kubwa za soka barani Ulaya.
Iwapo unaweza kuthibitisha tatizo la umri kwa Pogba,basi itakuwa ni tatizo la mfumo wa soka wa Ulaya,na sio Africa.
Najiuliza ni kwanini umeamua kujump into asili ya Pogba kwenye technical issue uliyokuwa unaizungumzia,ilhali mchezaji huyu "kimpira" si mwafrika kabisa.
Hata hivyo,ni kweli huku Africa tuna changamoto zetu kwenye uendeshaji wa soka yetu,pamoja na yote,najivunia Uafrika wangu,najivunia Madaraka Selemani pia.Ana legacy yake kwenye soka yetu,kwa kiwango chetu,haijalishi alikuwa babu au katoto.
 
Mchezaji wa kiwango cha dunia ni yule anayesaidia timu yake .
 
Nimeangalia game ya France na Romania mpaka dk hii ya 88 na nusu ambapo France inaongoza 2-1 , kiukweli huyu mchezaji anasifiwa bure tu .

Baada ya yeye kutolewa ndio timu ikapata uhai , kwa ufupi ni kwamba alikuwa mzigo kwa timu .

Sasa zile sifa zake zote za kule juventus ilikuwa za uongo ?
Yaani bro umesema huyu jamaa hana kitu sijui anasifiwa nini
 
mkuu athlete kila mtu anamaono yake hata mzee jose morinyo mpaka leo anasema hakuna mchezaji katika nchi ya ureno wa kumfananisha na USEBIO yule mreno mweusi aliyetisha miaka ya nyuma hata mimi leo ni shabiki wa SAINT GAUCHO yaani hata atokee nani no one like him
 
Back
Top Bottom