Kwanini Paul Pogba anasifiwa, mbona hana lolote?

Kwanini Paul Pogba anasifiwa, mbona hana lolote?

Ndugu kwa sasa hakuna mido Kama pogba hivi unafuatilia soccer kweli
 
Albania walikaza sana baada ya kuingia pogba na wenzie kila kitu kilibadilika
 
Na hatari zake mr "no pirlo, no part" nae kakosa, moja vs toronto hapo yupo juve, nyingine alikuwa kitu km ac milan hv vs barcelona akakosa pia.. Ndio hapowatu wanasema penalt ni km ugoni tu ipo siku yatakutokea yakukutokea.

Hussein Masha pekee atosha. Yeye ndiye mfalme Wa Penati kupata kutokea
 
Albania walikaza sana baada ya kuingia pogba na wenzie kila kitu kilibadilika
Inasemekana Mpira wa miguu ndio mchezo rahisi kuliko yote iliyopo , yaani ukichoka unampasia mwenzio , ni tofauti na ndondi au riadha , hata wewe unaweza kupiga pasi ya mwisho .
 
Huna lolote ! Zaidi umejaa hofu iliyochanganyika na jazba na kuchanganyikiwa , hii habari ya sokwe unayorudirudia kuandika humu umeitoa wapi ? Usinilishe maneno ya kijinga .
Jaap Stam,Juan Sebastian Veron na David Beckham hawakuwa wazuri wakati wakiondoka Old Trafford?Nani alikuambia Ferguson alimwachia Pogba?
 
Jazba na Mapovu yako havitaweza kuondoa ukweli niliouweka hapa , maandishi yako marefu sana lakini zaidi ya kutaja majina ya watu sijaona chochote ! Mpira ni uwanjani , nani kasema nini au gazeti hili limeandika nini hizo ni mbwembwe tu .
Wewe hutaji majina ya watu hapa?Huyo Pogba,Messi na Mwaikimba uliowataja sio watu?Kwa hiyo na wewe huna chochote,sivyo?
Mpira ni uwanjani yes,kwani Pogba anacheza soka kwenye bahari?Hayo maandishi marefu mbona umeyasoma na kuyaelewa?
 
Ndugu kwa sasa hakuna mido Kama pogba hivi unafuatilia soccer kweli
We waache wabongo wamezoea maneno,wenzetu huko ni vitendo tu.
Leo hii nadhani Kimmich atalala anamuota Pogba kwa jinsi alivyomdhalilisha kwa kumnyanganya mpira eneo la hatari na kumchezesha dansi murua kabla ya kupiga cross iliyozaa bao la pili.
 
Nimeangalia game ya France na Romania mpaka dk hii ya 88 na nusu ambapo France inaongoza 2-1 , kiukweli huyu mchezaji anasifiwa bure tu .

Baada ya yeye kutolewa ndio timu ikapata uhai , kwa ufupi ni kwamba alikuwa mzigo kwa timu .

Sasa zile sifa zake zote za kule juventus ilikuwa za uongo ?
Tangia aokoe gori lile na kuifingia ujeruman Gori moja bassiii ni habari zake tu,ila hana jipya
 
We waache wabongo wamezoea maneno,wenzetu huko ni vitendo tu.
Leo hii nadhani Kimmich atalala anamuota Pogba kwa jinsi alivyomdhalilisha kwa kumnyanganya mpira eneo la hatari na kumchezesha dansi murua kabla ya kupiga cross iliyozaa bao la pili.
Hivi hilo ndilo la kumweka kwenye viwango vya dunia ? Kuna tatizo kubwa sana kwa wachambuzi wa soka wa Tanzania , ushindi wa jana wa France umechangiwa na timu kucheza kwa pamoja ( Total Football ).

Pogba hana uwezo wowote wa kuamua matokeo ya mchezo kama wafanyavyo akina messi au Ronaldo , ni mchezaji wa kawaida sana .
 
Back
Top Bottom