Nimekuwa nikimfuatilia kada wa CCM Humphrey Polepole kuanzia alipotoa barua yake ya kujiuzulu ubalozi wa tanzania nchini Cuba; mazungumzo yake na Waandishi wa Habari na hata sasa (mazungumzo yake ya mwisho ameyafanya na Jenerali Ulimwengu).
Pamoja na mambo mengine, Polepole amekuwa akizungumzia desturi ya CCM ya kwamba aliyewahi kuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Spika hawapaswi kugombea Urais ndani ya CCM. Na sababu anayoisema ni kukosa jipya kwa watu hao mbele ya wapigakura wakati wa uchaguzi.
Ni ukweli ulio wazi kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa Makamu wa Rais. Kama angemaliza na Rais Magufuli, na kama CCM ingefuata 'desturi' hiyo, Rais Samia asingegombea Urais kupitia CCM. Lakini, Polepole hasemi jambo moja: Rais Samia hakuwa tu Makamu wa Rais, ndiye Rais aliye madarakani tangu mwaka 2021.
Kwahiyo, 'desturi' hiyo iliyosemwa na Polepole haimuhusu Rais Samia. Rais Samia ni sawa marais wengine waliotangulia, ambao wote walitokana na CCM, waliopitishwa na chama chao kutetea nafasi yao ya Urais. Hadi hapo, Rais Samia hawezi kuzuiliwa na 'desturi' hiyo ya Polepole.
Kwanini hili halisemi? Bahati mbaya au makusudi?
Acha ubutu wa akili; kwani katiba inasema kitu gani endapo rais aliye madarakani atafariki nani huchukua nafasi yake? Kila mwaka unaoishia na tano huwa ni mwanzo wa kutafuta mtu ambaye hakuwa kwenye madaraka ya juu kuteuliwa kuwania kiti hicho sio mtu kanogewa anataka kuendeleza hapana.
1. 1961-1965.....mpito.......................JK Nyerere
1. 1965-1970.......uchaguzi wa mtu na kivuli cheusi....JK Nyerere (Mwanzo wa katiba iliyopo na viraka vyake)
2. 1970-1975.......uchaguzi wa mtu na kivuli cheusi.....JK Nyerere
3. 1975-1980..........uchaguzi wa mtu na kivuli cheusi......JK Nyerere
4. 1980-1985.......uchaguzi wa mtu na kivuli cheusi.....JK Nyerere
5. 1985-1990.......uchaguzi wa mtu na kivuli cheusi....AH Mwinyi
6. 1990-1995.....uchaguzi wa mtu na kivuli cheusi......AH Mwinyi
7. 1995-2000....uchaguzi wa mtu kwa mizani ya mtu mwingine...BW Mkapa
8. 2000-2005....uchaguzi wa mtu kwa mizani ya mtu mwingine...BW Mkapa
9. 2005-2010...uchaguzi wa mtu kwa mizani ya mtu mwingine....JM Kikwete
10. 2010-2015...uchaguzi wa mtu kwa mizani ya mtu mwingine....JM Kikwete
11. 2015-2020...uchaguzi wa mtu kwa mizani ya mtu mwingine...... JP Magufuli
12. 2020-2025...uchaguzi wa mtu kwa mizani ya mtu mwingine....JP Magufuli (quarter phase)..VP SSH Successed
13. 2025-2030....? (concealled illegitimacy)......Start of fresh veins (sixth phase should start from this year)
14. 2030-2035....End of fresh veins
15. 2035-2040....Gen Zenith
16. 2040-2045...Gen Zenith
17. 2045-2050...Gen Alpha
18. 2050-2055....Gen Alpha
19. 2055-2060...Gen Alpha
20. 2060-2065...Gen Beta