Kwanini Polepole halioni hili? Ni makusudi au bahati mbaya?

Kwanini Polepole halioni hili? Ni makusudi au bahati mbaya?

Tuseme polepole kakosea Ila je kwanini Samia hakufata taratibu na katiba ya Ccm .

Mfano kupigiwa kura , kutafuta wadhamini , kwenda kuchukua Fomu ya urais n.k.?

Pole pole yawezekana hayuko sahihi Ila Ccm ndo hawako sahihi Sana .
Mazingira ya kuingia ikulu ya Samia ni tofauti na marais watano waliomtangulia. JPM angekuwa hai mpaka leo Samia angekuwa anajiandaa kustaafu akiwa makamu wa rais.

Kuingia kwa kiapo baada ya kifo hakumuondolei sifa ya urais wake, hakuondoi ukweli kwamba kwa yeye kuapishwa tayari keshakuwa na hadhi sawa na Hayati JPM na wote waliotangulia kuwa marais.

Anapoajiandaa kuhudumia kwa miaka mitano ya mwisho kikatiba, utamaduni ni ule ule kwamba rais anayekuwa bado yupo kazini huwa hapingwi na wote wanaochukua fomu kwa nia ya kuutaka urais.
 
Anaomba sawa, kuomba kuna kukubaliwa na kukataliwa.

Akikataliwa je nani yupo mbadala? Unajua maana ya kuomba?

Ni lazima kuwe na Mtu mwingine pemben ambae hata kama tusipokuptsha basi ataptishwa yeye.

Hata kama ni KIBABE ila lazima awekwe hata mtu geresha wa kuzugia

Kwann hamna, huoni kama kashajiamulia kupita na haombi kama usemavyo.

Mke Wako akwambie Naomba kwenda Saloon, Muda huo kashafika saloon anasukwa.. hapo kakuomba au kashafanya?

Huyu yeye Haombi maana yuko peke ake Tusitumie neno Kuomba vibaya..

Huyu ni Dikteta alie amua kuganda madarakani.

Sababu alizotumia ndio ambazo

Wananchi/Pole Pole hatumuelewi
Kama umri wako ni mdogo haya uliyoyaandika yana maana pamoja na wote wa rika lako.

Marais wanne waliomtangulia Samia, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na JPM hawakuchukuliwa fomu na watia nia wa urais wakati wakiwa na miaka mitano ya urais wao, kwanini kwa Samia hali ibadilike?.

Punguzeni kuwa mawakala wa mizengwe ya kisiasa.
 
Nimekuwa nikimfuatilia kada wa CCM Humphrey Polepole kuanzia alipotoa barua yake ya kujiuzulu ubalozi wa Tanzania nchini Cuba; mazungumzo yake na Waandishi wa Habari na hata sasa (mazungumzo yake ya mwisho ameyafanya na Jenerali Ulimwengu).

Pamoja na mambo mengine, Polepole amekuwa akizungumzia desturi ya CCM ya kwamba aliyewahi kuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Spika hawapaswi kugombea Urais ndani ya CCM. Na sababu anayoisema ni kukosa jipya kwa watu hao mbele ya wapigakura wakati wa uchaguzi.

Ni ukweli ulio wazi kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa Makamu wa Rais. Kama angemaliza na Rais Magufuli, na kama CCM ingefuata 'desturi' hiyo, Rais Samia asingegombea Urais kupitia CCM. Lakini, Polepole hasemi jambo moja: Rais Samia hakuwa tu Makamu wa Rais, ndiye Rais aliye madarakani tangu mwaka 2021.

Kwahiyo, 'desturi' hiyo iliyosemwa na Polepole haimuhusu Rais Samia. Rais Samia ni sawa na marais wengine waliotangulia, ambao wote walitokana na CCM, waliopitishwa na chama chao kutetea nafasi yao ya Urais. Hadi hapo, Rais Samia hawezi kuzuiliwa na 'desturi' hiyo ya Polepole.

Kwanini hili halisemi? Bahati mbaya au makusudi?
Rais Samia alikuwa Makamo wa Rais kweli na kwa katiba pia akawa Rais na akawa wa kwanza katika Historia ya nchi yetu kuwa Rais ambae hakuchaguliwa ama bila ridhaa ya wanachi.
Sasa anachokisemqa POLEPOLE ni kuwa kama hata kweli alitaka kugombea mwaka huu mchakto unatakiwa kuwa wazi na wanaccm waamuakama watampa ridhaa ama wataona wanahitaji mgombea mwingine na si yeye.
Kwa bahti baya hilo halikuiwa kama hivyo lkn wakaleta short cut a,bayo imeletea malalamika na kuwanyima ccm mamlaka yao ya kuchagua na ikawa nai matakwa ya wachache na lilikaaa kama jambo ambalo lilipangwa kwa njia haramub na inaonekana waliopngwa kuna nguvu walikuwa wanaikwepa.
 
Hoja ni huyo anayechukua fomu hitimisho ni kiapo chake cha urais.

Akishaapa inaanza awamu inayokuwa chini yake, tatizo tunashindwa kumuangalia Samia katika nafasi ya urais tunamdharau sasa tuendelee kuishi na dharau zetu wakati yeye akiishi miaka ya urais wake.


So hapaswi kuchukua form na kuomba wadhamini?
 
Nimekuwa nikimfuatilia kada wa CCM Humphrey Polepole kuanzia alipotoa barua yake ya kujiuzulu ubalozi wa Tanzania nchini Cuba; mazungumzo yake na Waandishi wa Habari na hata sasa (mazungumzo yake ya mwisho ameyafanya na Jenerali Ulimwengu).

Pamoja na mambo mengine, Polepole amekuwa akizungumzia desturi ya CCM ya kwamba aliyewahi kuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Spika hawapaswi kugombea Urais ndani ya CCM. Na sababu anayoisema ni kukosa jipya kwa watu hao mbele ya wapigakura wakati wa uchaguzi.

Ni ukweli ulio wazi kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa Makamu wa Rais. Kama angemaliza na Rais Magufuli, na kama CCM ingefuata 'desturi' hiyo, Rais Samia asingegombea Urais kupitia CCM. Lakini, Polepole hasemi jambo moja: Rais Samia hakuwa tu Makamu wa Rais, ndiye Rais aliye madarakani tangu mwaka 2021.

Kwahiyo, 'desturi' hiyo iliyosemwa na Polepole haimuhusu Rais Samia. Rais Samia ni sawa na marais wengine waliotangulia, ambao wote walitokana na CCM, waliopitishwa na chama chao kutetea nafasi yao ya Urais. Hadi hapo, Rais Samia hawezi kuzuiliwa na 'desturi' hiyo ya Polepole.

Kwanini hili halisemi? Bahati mbaya au makusudi?
Samia amekuwa na taasisi ya Urais kwa miaka kumi! Miaka mitano kama Makamu wa Rais ( kumbuka Rais na makamu wake ni kitu kimoja katika kutawala na ndio maana wanaomba kura pamoja). Miaka mitano mwingine amehudumia kama Rais. Hivyo kutokana na desturi hakutakiwa kuchukua form lakini kutokana na uchu wake wa madaraka anang’ang’ania kutaka kuendelea akifadhiriwana mafisadi wahuni wakiongozwa na Rostam Aziz. We Angalia tu zawadi na fedha anazohonga amezipata wapi?
 
Rais Samia alikuwa Makamo wa Rais kweli na kwa katiba pia akawa Rais na akawa wa kwanza katika Historia ya nchi yetu kuwa Rais ambae hakuchaguliwa ama bila ridhaa ya wanachi.
Sasa anachokisemqa POLEPOLE ni kuwa kama hata kweli alitaka kugombea mwaka huu mchakto unatakiwa kuwa wazi na wanaccm waamuakama watampa ridhaa ama wataona wanahitaji mgombea mwingine na si yeye.
Kwa bahti baya hilo halikuiwa kama hivyo lkn wakaleta short cut a,bayo imeletea malalamika na kuwanyima ccm mamlaka yao ya kuchagua na ikawa nai matakwa ya wachache na lilikaaa kama jambo ambalo lilipangwa kwa njia haramub na inaonekana waliopngwa kuna nguvu walikuwa wanaikwepa.
Waliompitisha Samia kugombea kwa njia ya haramu ni hawa wahuni waliokiuza chama kwa wafanyabiashara ili “ The Tanzania State” iendelee kuwa CAPTURED for another five years!!
Huu Unatakiwa uwe muendelezo wa “ State capture ya enzi ya Kikwete na “Home shopping Centre” kabla haijabadilishwa kuwa GSM! Na hawa ndio waliochangia ccm zaidi ya shilingi billion KUMI ; Je unadhani watazirudishaje kama sio kutolipa kodi?
 
Back
Top Bottom