Kwanini Polepole halioni hili? Ni makusudi au bahati mbaya?

Kwanini Polepole halioni hili? Ni makusudi au bahati mbaya?

Kwanini hili halisemi? Bahati mbaya au makusudi?
Hata kama ukiliondoa hilo.
Taratibu zilizotumika kumpata mgombea wa CCM kwenye hicho kikao cha Jan. 19; bado ni tatizo kubwa.

Na siyo hivyo tu, Samia mwenyewe alishaingiza mkanganyiko toka mwanzo alipo shika madaraka; alipo jitangazia awamu yake mpya, ya sita; kwa maana ya tano ilikomea alipo anzia yeye. Kwenye katiba hakuna awamu ya miaka minne; ambayo itafuatiwa na mingine mitano kukamilisha awamu ya sita; huku yote yakiwa hayaendani na mipango ya chama , i.e., ILANI ya CCM. Hakuna ilani iliyopangwa kukamilishwa ndani ya miaka mitano atakayochukuwa Samia.

Kwa hiyo, unaweza kumlaumu Poleole kwa kutozungumzia hayo unayo yasema wewe; lakini usisahau kuzungumzia pia lengo/mipango ya maksudi ya kukiuka taratibu na hata Katiba ya chama, na ile ya Jamhuri.

Hila OVU huzaa matokeo OVU.
 
Pole pole shujaa mpya wa chadomo ni takataka kama takataka zingine.

Alitaka nani awe rais wa JMT?
Chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan, Tanzania ni bora kabisa kuvumilia takataka inazoweza kuzisafisha; kuliko uharibifu mkubwa unaotokana na uongozi mbovu chini ya Samia.
 
Kwanini sio sawa kusema SSH kawa raisi kwa kipindi kimoja mkuu?
..Kipindi kimoja kinacover uchaguzi mmoja hadi uchaguzi mwingine unaofuata..kwanza hakuchaguliwa km rais, pili amechukua urais tayari miezi miwili ilishapita toka rais aapishwe..
 
TUNAIMAANI NA SAMIA,...... MNAOKUMBUKA HUU WIMBO WA 19.1.2025 HEBU NIKUMBUSHENI KIDOGO... KAMA UNAKUKERA VUMILIA NI MAPITO TU...NAYO YATAPITA.
 
..Kipindi kimoja kinacover uchaguzi mmoja hadi uchaguzi mwingine unaofuata..kwanza hakuchaguliwa km rais, pili amechukua urais tayari miezi miwili ilishapita toka rais aapishwe..
mbona katiba inatambua kwamba yeye kashapiga kipindi kimoja?
 
Nimekuwa nikimfuatilia kada wa CCM Humphrey Polepole kuanzia alipotoa barua yake ya kujiuzulu ubalozi wa tanzania nchini Cuba; mazungumzo yake na Waandishi wa Habari na hata sasa (mazungumzo yake ya mwisho ameyafanya na Jenerali Ulimwengu).

Pamoja na mambo mengine, Polepole amekuwa akizungumzia desturi ya CCM ya kwamba aliyewahi kuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Spika hawapaswi kugombea Urais ndani ya CCM. Na sababu anayoisema ni kukosa jipya kwa watu hao mbele ya wapigakura wakati wa uchaguzi.

Ni ukweli ulio wazi kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa Makamu wa Rais. Kama angemaliza na Rais Magufuli, na kama CCM ingefuata 'desturi' hiyo, Rais Samia asingegombea Urais kupitia CCM. Lakini, Polepole hasemi jambo moja: Rais Samia hakuwa tu Makamu wa Rais, ndiye Rais aliye madarakani tangu mwaka 2021.

Kwahiyo, 'desturi' hiyo iliyosemwa na Polepole haimuhusu Rais Samia. Rais Samia ni sawa marais wengine waliotangulia, ambao wote walitokana na CCM, waliopitishwa na chama chao kutetea nafasi yao ya Urais. Hadi hapo, Rais Samia hawezi kuzuiliwa na 'desturi' hiyo ya Polepole.

Kwanini hili halisemi? Bahati mbaya au makusudi?
Haujamuelewa Pole Pole ,amesema "WATCH_HUNDRED" alikuwa makamu wa Rais kwa miaka mitano na Rais kwa miaka mitano kasoro miezi miwili tu kwa kifupi SIR100 kashagonga miaka 10 kuwa kwenye High Ranks ,sasa aongezewe mitano tena aende kufanya kitu gani? #KATAA_WAHUNI.
 
Urais wa Rais Samia ulianza 2021. Anaomba kupata awamu yake ya pili. Haombi kama Makamu wa Rais, anaomba kama Rais aliye madarakani


Samia hakuchaguliwa kuwa Rais bali makamu wa Rais. Yaani mtu wa kuchukua nafasi ya urais kama dharula irampata Rais. Dharula ikatokea, akawa Rais wa dharula kumalizia kipindi cha aliyechaguliwa.

Kama ana hamu ya kuwa Rais, achukue fomu kama wagombea wengine, akiwa kama mgombea mpya, siyo kama Rais aliyechaguliwa. Yeye amemalizia awamu ya Magufuli. Hana awamu yoyote mpaka sasa. Kama anautaka urais wa awamu ya sita, aingie kwenye kinyang'anyiro kama wagombea wengine.
 
Tuseme polepole kakosea Ila je kwanini Samia hakufata taratibu na katiba ya Ccm .

Mfano kupigiwa kura , kutafuta wadhamini , kwenda kuchukua Fomu ya urais n.k.?

Pole pole yawezekana hayuko sahihi Ila Ccm ndo hawako sahihi Sana .
Ingebadilisha nini hata kama angefuata utaratibu??
 
Katiba ipi na inatambuaje..fafanua
katiba ibara ya 40.jpg


ya nchi
 
Jipya lililopo ni kama ifuatavyo..
1. Ilani huwa hazifanani kwa vipindi hvyo viwili.
2. Muundo wa baraza la mawaziri hutofautiana kutoka kipindi kimoja kwenda kingine kutegemeana na rais aliyepo madarakani.
3. Utekelezaji wa ilani hyo hutofautiana kutok kipindi kimoja kwenda kingine kutegemeana na bajeti ya nchi kulingana na sera, dira na hali ya uchumi kwa kipindi hicho cha miaka 5.
4. Hata wajumbe wa kisekta wa chama na vikao vyake huwa ni tofauti (kumbuka kila baada ya miaka 5, ccm hufanya uchaguzi wa ndani)
5. Ari ya kiongozi mwenyewe ikiwemo aina yake ya uongozi.
6. Mapokeo ya wananchi kwa kipindi hcho cha uongozi.

SABABU NI NYINGI MNO.
Na hizi sababu ulizozitaja ndo anazozitumia Mseveni na Kagame kujiongezea mda wa kubaki madarakani
 
Nimekuwa nikimfuatilia kada wa CCM Humphrey Polepole kuanzia alipotoa barua yake ya kujiuzulu ubalozi wa tanzania nchini Cuba; mazungumzo yake na Waandishi wa Habari na hata sasa (mazungumzo yake ya mwisho ameyafanya na Jenerali Ulimwengu).

Pamoja na mambo mengine, Polepole amekuwa akizungumzia desturi ya CCM ya kwamba aliyewahi kuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Spika hawapaswi kugombea Urais ndani ya CCM. Na sababu anayoisema ni kukosa jipya kwa watu hao mbele ya wapigakura wakati wa uchaguzi.

Ni ukweli ulio wazi kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa Makamu wa Rais. Kama angemaliza na Rais Magufuli, na kama CCM ingefuata 'desturi' hiyo, Rais Samia asingegombea Urais kupitia CCM. Lakini, Polepole hasemi jambo moja: Rais Samia hakuwa tu Makamu wa Rais, ndiye Rais aliye madarakani tangu mwaka 2021.

Kwahiyo, 'desturi' hiyo iliyosemwa na Polepole haimuhusu Rais Samia. Rais Samia ni sawa marais wengine waliotangulia, ambao wote walitokana na CCM, waliopitishwa na chama chao kutetea nafasi yao ya Urais. Hadi hapo, Rais Samia hawezi kuzuiliwa na 'desturi' hiyo ya Polepole.

Kwanini hili halisemi? Bahati mbaya au makusudi?
Anajua fika..

Lakini wazima huwa hatuambiani "umejamba" ila ukiona harufu ya uchuzi inakuzidia, unaondoka mdogo mdogo kimya kimya...

Lakini huoni jambo moja, kwamba, hiyo ni lugha tu lakini the fact behind the scene ni kuwa anashindwa tu kusema kuwa "HUYU HAPANA, HATAKIWI KWA SBB HANA UWEZO WA KUONGOZA NCHI IWAPO ATASHINDA..!"

Hata hivyo indirectly ameshasema mara nyingi sana. Mfano wake kusema kuwa "nchi kwa sasa haina uongozi" unadhani logic yake ni nini...?

Maana yake iko very straight kuwa, HUYU ALIPO HAFAI, HANA UWEZO...!

Kwenye hii video, hajaficha kitu. Kamwambia kabisa "YOU CAN'T BE, MADAM...☹!!"

View: https://youtu.be/qeGhGDagxYg?si=C8Y5WA-hT_ggNvJW
 
..ibara ya 37(5) inasemaje..
ibara hiyo ya 40(4) lengo la kukupa hiyo ni kusasahisha comment yako hii

..Kipindi kimoja kinacover uchaguzi mmoja hadi uchaguzi mwingine unaofuata..kwanza hakuchaguliwa km rais, pili amechukua urais tayari miezi miwili ilishapita toka rais aapishwe..


hiyo 40(4) sioni tatizo lake
 
ibara hiyo ya 40(4) lengo la kukupa hiyo ni kusasahisha comment yako hii




hiyo 40(4) sioni tatizo lake

37 (5) kwa muktadha wa Samia inaongelea rais aliyekuwa VP anavyopata kuwa rais baada ya rais wa awali kufariki.

40(4) Inampa Samia nafasi ya kugombea urais 2025 lakini inamnyima nafasi ya kugombea urais 2030.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Back
Top Bottom