Kwanini Polisi Tanzania wanaipigania CCM kufa na kupona?

Kwanini Polisi Tanzania wanaipigania CCM kufa na kupona?

kagoshima

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2015
Posts
2,887
Reaction score
5,687
Ni wazi kabisa sasa polis wamechukua nafasi ya CCM kushindana na vyama vya upinzani. Huku CCM ikiwa mtazamaji napengine kuwapo kama haipo.

Tofauti ndogo nikwamba polis wanamiliki siraha na mahabusu hivyo washindani wao wanakiona cha mtema kuni.

Ukiangalia kwa makini hawa polis na pengine hata iyo TISS wamewekeza nguvu kukipigania chama badala ya taifa. Mfano, walikua wapi Tiss na polisi wakati inchi inapigwa kwenye michongo ya kifisadi? Walikuwa wapi hizo idara zenye intelligence kali dhidi ya mikutano ya vyama vya upinzani? Kwenye wizi wa EPA kwenye uchotaji hela za Escrow kwenye sakata la Richmond Ufisadi kwenye UDA nk

Hapa ndipo pangekuwa kipimo cha uzalendo wao.

Utawaona sasa, wako bize kuteka, kukamata, kutesa, kupoteza, kubambikia kesi wafuasi wa vyma vya upinzani. Wanafanya hivi kulinda interest zao?

Interest za mabosi wao, interest za familia zao? Kwanini wanapigania sana interest za CCM na si interest za taifa?
 
1. CCM ipo madarakani.

2. Waliopo madarakani ndio boss wa kufanya maamuzi katika majukumu yao ili kuwasaidia kuendesha nchi wanavyotaka wao.

3. Bosi hanuniwi na wala hapingwi.
 
Maovu wanayofanya polisi na maovu ya CCM yanafanana kabisa na huwezi kutenganisha.

In fact CCM ikiondoka, polisi watafungwa wengi sana maana wamekuwa walitekeleza maovu mengi kwa maelekezo ya viongozi wa CCM.

Pia polisi wameumiza sana watu na kuwaonea, kunyang'anya Mali za watu na Mambo mengi sana ya kidhalimu.

Halafu pia usalama wa taifa nao hawawezi kukubali maana nao wanaonea watu, wanatajirika kupitia CCM
 
Kwa sababu katika barua zao walisema wako mtiifu so LAZIMA waheshim maboss zao
Nakuelewa mkuu . lakini hali inashangaza kunakipindi walitengeneza visu vyenye bendera ya CUF at kuichafua CUF at ugaidi. huoni wanachafua taaswira ya taifa kwa kufurahisha mabosi wao?
 
Polisi wanapewa vyeo na CCM wakishastaafu.

Mwenyekiti wa Sasa wa ccm wa mkoa wa Arusha Zelote Stephen ni mstaafu wa polisi.

Mangu ambaye sasa ni balozi ni IGP mstaafu.

Ndiyo maana wanapambana kufa na kupona ccm ibakie madarakani.
 
Ni wazi kabisa sasa polis wamechukua nafasi ya CCM kushindana na vyama vya upinzani. Huku CCM ikiwa mtazamaji napengine kuwapo kama haipo.

Tofauti ndogo nikwamba polis wanamiliki siraha na mahabusu hivyo washindani wao wanakiona cha mtema kuni.

Ukiangalia kwa makini hawa polis na pengine hata iyo Tiss wamewekeza nguvu kukipigania chama badala ya taifa.
Mfano, walikua wapi Tiss na polisi wakati inchi inapigwa kwenye michongo ya kifisadi?
Walikuwa wapi hizo idara zenye intelligence Kali dhidi ya mikutano ya vyama vya upinzani?
Kwenye wizi wa EPA
Kwenye uchotaji hela za Escrow kwenye sakata la Richmond
Ufisadi kwenye UDA nk

Hapa ndipo pangekuwa kipimo cha uzalendo wao.

Utawaona sasa, wako bize kuteka, kukamata, kutesa , kupoteza, kubambikia kesi wafuasi wa vyma vya upinzani. Wanafanya hivi kulinda interest zao ?

Interest za mabosi wao, interest za familia zao? Kwanini wanapigania sana interest za ccm na si interest za taifa?
Jeshi na Polisi wanaihitaji sana CCM kuliko CCM wanavyowahitaji wao. Mfano Kule Myammar (Burma) chama tawala kilipoanguka na yule mwanamama " Sun Ky" kuchukua madaraka , polisi na jeshi halikupeta tena ilikuwa full katiba na sheria zinavyosema.

Hapo Jeshi lilishindwa kuvumilia na kumpindua yule Mama na wao kuitwaa madaraka. Nafikiri huko baadae watairudisha CCM- Myammar kuchukua madaraka tena ili Jeshi na Polisi waendelee kupeta. Hivyo ndivyo mahesabu yalivyo hata kwa TZ na saga za CCM na jeshi (JWTZ) na Polisi.
 
Police wote nchin wapo chini ya Simon Sirro ambaye anaripot moja kwa moja kwa mwenyekiti wa CCM.
 
Kwasababu ccm wameshaishiwa hoja kwahiyo imewabidi wajisalimishe kuomba mbeleko ya vyombo vya dola kama hilo jeshi ulilolitaja.Ukiona chama cha siasa kilichoko madarskani kimejificha nyuma ya jeshi jua hicho chama ndo kinaishilia hivyo.pumzi zishakata kwahiyo wanatumia pumzi ya vyombo vingine kusukuma siku.
 
Ni wazi kabisa sasa polis wamechukua nafasi ya CCM kushindana na vyama vya upinzani. Huku CCM ikiwa mtazamaji napengine kuwapo kama haipo.

Tofauti ndogo nikwamba polis wanamiliki siraha na mahabusu hivyo washindani wao wanakiona cha mtema kuni.

Ukiangalia kwa makini hawa polis na pengine hata iyo Tiss wamewekeza nguvu kukipigania chama badala ya taifa.
Mfano, walikua wapi Tiss na polisi wakati inchi inapigwa kwenye michongo ya kifisadi?
Walikuwa wapi hizo idara zenye intelligence Kali dhidi ya mikutano ya vyama vya upinzani?
Kwenye wizi wa EPA
Kwenye uchotaji hela za Escrow kwenye sakata la Richmond
Ufisadi kwenye UDA nk

Hapa ndipo pangekuwa kipimo cha uzalendo wao.

Utawaona sasa, wako bize kuteka, kukamata, kutesa , kupoteza, kubambikia kesi wafuasi wa vyma vya upinzani. Wanafanya hivi kulinda interest zao ?

Interest za mabosi wao, interest za familia zao? Kwanini wanapigania sana interest za ccm na si interest za taifa?
Nao pumzi itakata tu, Cha msingi naona ebu twende tukawe wadau kila wilaya na akaunti maalum ya kuchangia Mawakili wetu pesa KILA Wilaya, watu waanze kushitakiwa KWa majina yao wafanyavyo sio tuone, ichi ni kipindi ambacho mahakama zetu hazitakiwi kupumua, Mawakili wetu wasomi tuwatumie ipasavyo ,tutaelewana vizuri Sana,
 
Common interests nilinde nikulinde.Mapoty wanailinda chakavu kupora kura na chakavu wanawalinda mapoti kupora raia.
 
Wajifunze kwa boss wao aliyekuwa bize kuua upinzani akafa yeye
 
Back
Top Bottom