Kwanini Prince Dube anachezeshwa dakika 90 kila mchezo?

Nilishangaa kumuona Ramovic alipokuja tu kawa ndiye chaguo lake la kwanza na kumpa dakika 90 za kucheza nikapata wasiwasi pengine kuna hali ya ushinikizaji wa upangaji wa kikosi. Alipoondoka Ramovic, kwenye mechi dhidi ya Ken Gold nilitaka nithibitishe juu ya kile nilichokuwa ninakihisi ila nilipoona tena Dube yupo first eleven halafu kacheza dakika zote 90 nikahitimisha kuwa upangaji wa kikosi ndani ya Yanga kuna kiongozi anashinikiza kupangwa kwa baadhi ya wachezaji.

Uozo anaonesha Dube hakuna kocha anaweza kuvumilia huo upumbavu wake. Hana stamina, hatumii akili, mapepe kibao hatulii na hakai kwenye nafasi. Mzize kamuacha mbali Dube kwa kila kitu uwanjani. Nadhani Baleke angepewa nafasi kama alivyopewa Dube angekuwa na takwimu nzuri kuliko Prince mpumbavuleo Dube
 
Jean Baleke ni mshambuliaji wa kati aliyekamilika sana ukimlinganisha na Dube. Sijui ni nani alimpiga zengwe kiasi cha kushindwa kupewa nafasi ya kucheza hata kwenye mechi za kawaida kabisa, huku Dube akibebwa kwa kila hali.
 
Dube anafanya shughuli nyingi uwanjani
Anakimbiza sana
Anajua kusimama
Kwa striker kupata hata nafasi ya kukosa goli ni ngumu, najua wengi hamjacheza nafasi hiyo
Japo Dube anakosa confidence
 
Dube anafanya shughuli nyingi uwanjani
Anakimbiza sana
Anajua kusimama
Kwa striker kupata hata nafasi ya kukosa goli ni ngumu, najua wengi hamjacheza nafasi hiyo
Japo Dube anakosa confidence
Watu wanataka magoli Sheikh. Kukimbia kimbia tu hovyo uwanjani kama kuku aliyekatwa shingo, kunaisaidiaje timu kushinda?

Mimi kwenye ukweli huwa sikopeshi. Prince Dube kwenye timu yetu bado anajitafuta. Na kama ana mpango wa kufikia viwango vya Fiston Mayele, basi anatakiwa apambane sana kwenye stamina, pace, na utulivu.
 
Nina mashaka sana na prince kama atatoboa msimu ujao.....
 
Jean Baleke ni mshambuliaji wa kati aliyekamilika sana ukimlinganisha na Dube. Sijui ni nani alimpiga zengwe kiasi cha kushindwa kupewa nafasi ya kucheza hata kwenye mechi za kawaida kabisa, huku Dube akibebwa kwa kila hali.
Dube ana utukutu flani wa kukaba na kuwanyima utulivu mabeki

Ni mzuri wa kujiposition

Kwa mfumo wa yanga dube ni false striker kama mdoli wafungaji halisi ni wengine

Na hiyo ndo tofauti ya dube na musonda, dube anafanana na mzize utukutu

Hukuona mechi ya MC ALGER alianzishwa musonda hakuleta impact yoyote

Tatizo la dube kwa sasa ni lile alilopitia mzize miaka michache iliyopita

Avumiliwe
 
Jifunze kutazama mpira Kwa utulivu utaiona potential ya Dube
Ni mchezaji amekamilika
Nadhani anapata pressure ya kufanya vizuri kila mechi, ambayo hajawahi kupata popote kwenye kazi yake
 
Unajua mpira sana mkuu
 
Mchezaji wa kimataifa havumiliki,manake atakuwa amejaza ile list ya wachezaji 12 huku akiwa hana mchango ktk team,kwa mchezaji wa ndani sawa.
 
Mchezaji wa kimataifa havumiliki,manake atakuwa amejaza ile list ya wachezaji 12 huku akiwa hana mchango ktk team,kwa mchezaji wa ndani sawa.
Timu kutokuwa na strikermakini ni janga la kidunia
 
Naumia sana kuona DUBE anapangwa na kucheza kwa 90minutes
 
Hivi Dube alikua ana fake injury Azam? Mbona tangu atue utopolo haendi tena wodini.

Nb: takwimu zake kwa sasa sio mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…