#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

Lkn bado kuna chawa wake walikuwa wanamsifu na kumpongeza.

Hata huyu mpandisha huu uzi wala hakuupandisha kwa bahati mbaya ,no alitaka kupata pa kuanzia ili aendelee kumsifia jiwe.
 
Unataka tuweke lock down, huo ndio utaalam unaotaka, hao wenye lock down wanakufa wengi zaidi ya Tz sasa nini faida ya lockdown ? SSH ana tatizo, tena ni KUBWA.
Hakuna sehemu watu wamelazimisha nchi iwe na lockdown jaribu kutumia viungo vyenu vya kufikiri na kuwaza.
 
Mkuu mwendazake alikuwa sahihi hizo chanjo zimeanza kuua watu badala ya kuwa kinga hapo jirani kwa hao waitikia bee ya mabeberu waliochanjwa wameanza kuugua na wengine kufa , kama chanjo kachanjeni punda sio watu,hata kunipe bilioni sichanji,hii AstraZeneca ni hatari kwa afya ya watu lakini sababu imetoka kwa mabeberu basi kila mjinga anashabikia,ingekuwa hayo madhara yanatokana na kupiga nyungutungesikia dunia nzima imehamia Tanzania na kutulaani sana, sichanjwi ng'o kama siku yangu imefika basi nitaenda kwa mola wangu lakini siokufanywa mbuzi wa majaribio. Hapo Kenya sasa wameanza kujiju na kutambua kwamba wanasiasa wanatumia ugonjwa wa COVID-19 kupata pesa za mikopo kutokakwa mabeberu na ndio maana kila siku unasikia lockdown,chanjo mara barakoa mara sijui nini. Mama anataka kuturudisha Misri!
 
Rais wetu anajua kabisa Sayansi ni Sayansi na sio Siasa, lazima ashauriwe na Wanasayansi sio Lumumba
Wanataka waanze kumshauri na huyu ili wampoteze mazima kama walivyo mpoteza jiwe
 
Mkuu punguza jazba

Kama Rais hajui msimamo wa nchi kuhusu Corona sasa kwanini amekuwa Rais?
Sasa kutovaa barakoa ni msimamo gani?

De facto, Tanzania huwa ina msimamo wa Rais wa JMT (personal stance) na huo ndio huwa msimamo wa nchi. Hatujawahi kuwa na msimamo wa nchi UNAOJITEGEMEA nje ya utashi wa Rais wa JMT aliyeko madarakani! Hii ni katika kusimamia sera ya chama tawala ya kulinda “amani, umoja na mshikamano” wa kitaifa!

Kwa muktadha huo, msimamo juu ya Covid-19 tuliokuwa nao hadi sasa ni wa Hayati JPM. Leo hii hayupo na yake hayapo tena.

Sasa kuwa na subira Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan atengeneze msimamo rasmi wa Tanzania kuhusu Covid-19 wa kipindi hiki cha Rais wa Sita wa JMT. Usimpangie.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; kazi iendelee!
 
Unayeandika hivi, usikute hujawahi hata kuambukizwa hiyo Corona, na pengine unaposema Magufuli hakuwa Sawa katika kushughurikia Corona ukilinganisha na nchi gani ambao kwao wameshughurikia vizuri na Corona kwao haipo mpaka Leo ni Nani na nchi gani??
Uzuri wa corona inawatafuna watu wenye kushupaza shingo kama nyinyi ndiyo inaondoka nao .
 
Kwanini Tusiamini ana ajenda zake mkononi anataka azipitishe nyuma ya kamati ili watanzania waamini ni msimamo wa kamati kumbe ni msimamo wake?
Hata suala la kuomgezewa muda wa kiutswala wa mwendazake aliamza kuwatumia akina sukuma baadae wakaja wanyonge ubongo sifuri kuwa wanaandamana kuonyesha uungwaji mkono wa hao wabunge. Mlizoea kuonea umma wa WaTz lakini Mungu hadhihakiwi. Umeambiwa tiba ya covid 19 ni lockdown? Sasa tunaimba wimbo mmoja kwa style moja. La mwendazake sasa ni historia usitarajie itajirudia. Tumejifunza mengi sana ila Mungu hadhihakiwi. Ungeuguliwa na mtu akapona au wewe binafsi usingeandika haya uliyoandika kama ushawishi kwa wengine.
 
Kenya wanaofuata COVID19 protocols wako wapi?
Je hamsikii hosptali na mfumo wa afya ulivyozidiwa?
Mbona bongo tunaishi na vizuri tu na maisha yanaendelea kama kawaida?
Tunataka maisha gani zaidi?
Mnaishi vizuri kwa vigezo gani?
Wakati hata mashine za kupimia hiyo corona mlitwambia kuwa ni feki?
 
Pipa na funiko mnasifiana.
Huo ujinga mlikuwa mnamjaza Jiwe tuu.

Kwa mama Samia mmekwama maana kamwe hawezi kusikiliza maneno yenu ya kishirikina
 
Watu kama Magufuli ndio wanaosababisha
Nilivyoona id yako nikajua wewe ni mkushi mwenzetu, kumbe ni opposite.

Dah bora ungejiita plato, sio hayo majina yetu wakushi,
Halafu unakuja na mambo ya chanjo.

Jina lako, fake id yako ni vizuri ikaendana na mtamazamo wako.

Ni km upo tayari niambie nikupe id inayoendana na mtazamo wako.

Sisi wakushi hatutaki chanjo.
 
Hiari? Unaweza safiri nchi za nje bila chanjo ya yellow fever? Mbona hamkuipinga.

Unajua inferiority complex ni ugonjwa mkubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…