#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

Mapumbafu sana haya,yako selfish sana.Hivi hata Mpango hayakumuona,na jiwe je?Mim nimepigwa week tatu usiombe ikuguse
Hili la Corona lipo, na lipo ili tukabiliane nalo, umeandika Kwa uchungu Sana mkuu, naheshimu mawazo yako Isipokuwa matusi

Licha ya hivyo, umejiuliza pia kwamba kunaambao wamepoteza Maisha Yao Kwa sababu ya chanjo za majaribio?

Unadhani wanaumia Kwa kiasi gani ndugu za hao wafiwa??

Swala hili la Corona, ni swala lenye utata mkubwa sana, angalia nchi jirani hapo, wameagiza chanjo, baada Tu ya chanjo kuingia, Leo hii mitungi ya oxygen haotoshi mahospitalini

Huoni kwamba hili suala linautata??
 
So we unachotaka ni nini sasa?? Maana unalalamika bila kusema nini unataka
Watu wambiwe tatizo lipo na wachukue tahadhali zote huku maisha yakiendelea,laiti kila mmoja angetikiswa na hili jambo tungapata somo,collective effort,both internal and external zinahitajika kukabiliana hii changamoto.Watanzania hatuambiliki mpaka yatupate hata mimi nilikua nachukulia kirahisi sana km ilivyokua kwa jiwe lakin imenipa somo
 
Ok but watu kupoteza maisha wakati wa kujitibu ni tofauti na kutokuchukua hatua,ikumbukwe kuwa ni chanjo na tupo kwenye majaribio.Hivi hujawahi kuona dawa inatibu kwa fulani na mwingine inamletea matatizo hata kufariki?Mhim hapa ni hatua za ndani na nje zichukuliwe na kwa bahati nzuri kwetu ni kwamba tuna nafasi ya kujua ip chanjo nzuri kwakua zimeishaanza kufanyiwa majaribio na wenzetu,hivyo suala la Rais kuunda kamati ya wataalam ni jambo jema sana ktk kukabiliana na hii changamoto.
Bro nimepoteza ndugu na marafiki hvyo ninapoona watu wanaleta mzaha nakasirika sana.Dhana ya siamini mpaka inipate ni hatari
 
Hakuna korona bali kuna changamoto za upumuaji,kama ipo mbona Philip aliyezushiwa kifo cha Corona alitoka live na kuikana tena na kuwakoholea watu bila balakoa mbona hawakupata hiyo corona.Kumuelewa Jiwe kwenye Marketing ya Corona Unahitaji IQ kubwa.
 
Kuna wakati mnadhani mama sio wa Lumumba?

Upinzani wa TZ haujawahi kuwa serious..[emoji16]
Majitu ya lumumba hayawez kubali ushauri Mungu wao aliwazoesha vibaya, too bad mungu wao kafa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Magufuli alikuwa sahihi 100% suala la corona. Nashangaa watu wanaishabikia corona kama Mungu vile. Malaria inaua kila dakika, mamilioni kwa mwaka, watu kimya, corona yenye kuua mia hata elfu haiwezi watu kilele kibao. Pelekeni hizo nguvu kwenye malaria basi.
 
Mimi nadhani, timu itayofanya utafiti, ifanyie pia swala maambukizi ya Kasi Ikiwa Taifa linapoagiza chanjo, zikitua tu maambukizi nayo yanaongezeka Kwa Kasi!

Mf. Nchi jirani, Kwa tarifa za leo, inaonekana mitungi ya oxygen inaelekea kuzidiwa na wahitaji
 
Unataka tuweke lock down, huo ndio utaalam unaotaka, hao wenye lock down wanakufa wengi zaidi ya Tz sasa nini faida ya lockdown ? SSH ana tatizo, tena ni KUBWA.

Kupambana na Corona ni lockdown peke yake? Hakuna mtu anataka lock, bali njia nyingine za kisayansi zichukue nafasi. Mnatumia lockdown kama njia ya kubeba Utetezi wenu wa kiupotoshaji.
 

Kampeni ya malaria, ukimwi nk nazo zilivaliwa njuga, huenda ulikuwa hujazaliwa, waulize wazazi wako. Ni hivi, ushirikina sasa basi.
 
Poleni wakuu, tumempoteza rais wetu na misimamo yake, wafuasi tumebaki! Tuzingatie tu kwamba kila zama na kitabu chake! Tuteseke zetu kwa miaka minne, kama wale wenzetu waloteseka kwa miaka 6!
Wasalaam!
 
Yeye mbona hakuchomoka kwenye hiyo corona?
 
Kenya wanaofuata COVID19 protocols wako wapi?
Je hamsikii hosptali na mfumo wa afya ulivyozidiwa?
Mbona bongo tunaishi na vizuri tu na maisha yanaendelea kama kawaida?
Tunataka maisha gani zaidi?
Hamtaki maisha zaidi, mtupishe kwanza kwa hii miaka minne tuirudishe Tanzania duniani! Kwa anaye ona hawezi aende tu, huko nchi ya malaika ambapo malaika mkuu anaongoaza na kule hakuna corona wala lockdown, hata hospital za kuzidiwa hazipo! Mfumo wa afya haujazidiwa kama Kenya kule!
 
Mama Janeth hukumuona amevaa barakoa? Ama wewe macho yako yako kwenye makalio?
 
Kwani ni mungu yupi huyo wa hayo mambo yenu ya kinajimu unamzungumzia hapa? Mnazuia taarifa za watu 800 wamekufa badala ya kuzuia watu 800 kufa?!
 
Ni wapi kusikokuwa na Corona?
Ni nani mpaka sasa kaidhibiti Corona?

Habari ya Udoct na Uprof achana nao, na punguza jaziba hazisaidii!!

Kama unaona zinasaidia, toa faida moja wapi tuone

Hii kauli ya “nani kaidhibiti corona?” ni ujinga mwingine mkubwa mlioletewa na Jiwe. Kwa akili finyu, kudhibiti ni sawa na kumaliza. Ni magonjwa mangapi bado yapo duniani lakini tunasema yamedhibitiwa? Dunia inapambana na Covid-19 sisi tumekaa pembeni kama mashabiki au wanga kusubiri washindwe. Wakipata tiba imara eti ndio tuanze kulilia msaada!

Kuna nchi zimefanikiwa kushusha kiasi na kasi ya maambukizi na vifo vinavyotokana na Covid-19 na wanazo takwimu za kuthibitisha. Wanapitisha maamuzi kisayansi. Sisi tumekana na kuficha takwimu na kuendekeza kauli za kijinga kama “changamoto ya upumuaji”, “mtaani kwenu nani kafa kwa corona?”, “hakuna tiba ya corona”, “hatutaki chanjo”, “corona ni hofu tu”, nk.

Acha Mh SSH aturejeshee SANITY kwa kufanya mambo kwa akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…