#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

Kama huelewi sasa tukupashe vizuri.
Text book ujinga ni kujidai unajua kilakitu wakati hujui.
Mtangulizi wake kwa mabavu aliyokuwa anatumia nani alikuwa anahoji maamuzi yake?
Yule alikuwa kombe la wanaharamu unalipisha lipite.
Kina Kigwangala ndio tunawasikia sasa wakipinga yaliyotokea.
They know now they are safe.

Kina Mzee Shamte walidiriki kuhoji maamuzi yake wamefia jela kwa kubambikwa kesi za uhujumu uchumi.

Mama kapatia kabisa, ukiwa rais siyo kwamba wewe unajua kila kitu, tubu kila mtu kwa akili yako.

Katika hili mama yuko rught 101%.
Mnaopinga muko na ajenda, uzuri mnajulikana.
 
Unataka tuweke lock down, huo ndio utaalam unaotaka, hao wenye lock down wanakufa wengi zaidi ya Tz sasa nini faida ya lockdown ? SSH ana tatizo, tena ni KUBWA.
Hakuna aliyesema lockdown, usiwe na haraka kama mpika gongo! Subiri kamati ya kitaalamu itasema!
 
Hebu tuende kiroja kwa hoja tuandikie msimamo wa Tanzania kuhusu Covid 19.

Tanzania hakuna Corona kama nchi nyingine na hajaathiri kama nchi zingine ndio maana Rais Samia havai barakoa!

Huo ndio msimamo lakini nashangaa Rais Samia anashindwa kukiri tulikuwa na msimamo lakini hakuupenda na sasa ataanza kuvaa barakoa!

Lakini havai barakoa na bado anasema Tanzania hatukuwa na msimamo hahaha
 
Kwahiyo Jiwe mnasema kafa kwa corona kwa sababu hakuchukua tahadhari? kwa hoja kama hizo ndio maana mnaambiwa hata huko wanakochukua tahadhari bado takwimu zao zinaonesha wanaendelea kufa kwa wingi pamoja na tahadhari sasa kama unafikiri Jiwe asingekufa kama angechukuwa tahadhari basi tungeona huko kwa wenzetu vifo vikipungua kama sio visingekuwepo kabisa.
 
Labda amesikia kilio cha chadema cha kutaka nchi ikae lockdown hivyo anataka atuweke Lockdown
 

Sasa kwanini havai barakoa kama msimamo wa mtangulizi wake ulikuwa wakipumbavu? Kwa hiyo na kuvaa barakoa anaisubiri kamati ?
 

Mkuu barakoa si nguo ambayo mtu lazima kuvaa.

Kunapo social distancing hata usipovaa barakoa ni sawa.

Msimamo unaokubalika haukuwapo hicho ndiyo mama anachokazia.

Kuna tatizo gani wenye ujuzi wao wakishauri? Acheni wataalamu watoe yao ya kiushauri.

Tulikotoka kila mtu fundi.

Mwanzo mpya, matumaini mapya!
 

Nimekuelewa na nina kubaliana na wewe kabisa lakini ninachopinga ni Rais kusema hatukuwa na msimamo wakati yeye hadi sasa havai barakoa!

Hivi anasubiri kamati ije kumshauri kuvaa barakoa?
Kwanini tusiamini kuwa ana ajenda anataka kuzipitisha nyuma ya kamati?
 
Kamati itamshauri tupate chanjo, ya aina gani na kwa utaratibu gani.

Hahahaha kamati imshauri wakati walishakubali kupokea chanjo ya Astrazeneca?
 

Naamini katika taaluma..

Nimeshauri mama asitumie nguvu, maana yake endapo chanjo italetwa aende na ambao wako tayari, huku elimu na hamasa ikiendelea kutolewa kwa ambao hawako tayari.
 
Unasema wanakufa kwasababu wanazo takwimu nyie hata kama mnakufa kwa korona hamtojua.
Sasa hawa wanaosema Jiwe kafa kwa corona wamejuaje? maana unaambiwa fulani kafa kwa corona ila wale watu wa karibu wa marehemu huoni kama wameambukizwa huwaoni hata na mafua sasa hii corona ya bongo ni ya aina gani?
 
Tungekuwa na msimamo tungezipimisha kware, mimbuzi , makondoo, mapapai na oil za magari maabara kuu ya taifa ?!

Odhis *

Sasa kama hatuna msimamo ni kwanini Rais havai barakoa? Au na hilo anasubiri kamati ije kumshauri?
 
Chanjo lazima Ili kutotengwa kimataifa, mbona mataifa mengine wametumia wewe ulitakaje

Kwani nani kakataa? Swala hapa ni kwanini Rais anadanganya hatukuwa na msimamo kuhusu Corona wakati hadi sasa havai barakoa? Au ananiogopa?
 
Mama hataki kuwa Dikteta anataka kila jambo ashauriwe
Wewe una akili sawa sawa? Yani hata yeye kuvaa barakoa ni hadi aunde kamati ndio imshauri avae barakoa na kwamba akivaa bila kushauriwa ni udikteta?
 
Sasa hapo kosa liko wapi kutafutabushauri wa kitaalamu mengine mkae kimya Kwanza kukosoa tu hata mambo hayana maana. Huyu Rais anahaki ya kuendesha anavyoona inafahaa
 

Mkuu Asante kwa kunisaidia!
 
Mama anafanya mambo kitaalamu, ametulia kimya kusikiliza ushauri wa kitaalamu.

Usikivu nao ni kipaji kama vipaji vingine.
 

Anataka kamati imshauri nini kipya ambacho hakujui? Anaogopa nini? Ni kwanini anasema hatuna msimamo kuhusu Corona na wakati hapo alipo havai barakoa?
 
Hajui takwimu maana mkemia alizificha na kukataza wasitangaze. Sasa ni kosa kufanya tafiti ya kisayansi? Hvi nchi hii Mkemia alikia anaipeleka wapi?

Sasa kwanini havai barakoa? Au anamuogopa Jiwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…