#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

Hivyo vifo ndio vinatangazwa sana na ndio vinavyofanya watu waogope corona na kuona ni ugonjwa hatari na ndio maana vinatangazwa sana kuliko wanaoumwa na kupona japo ndio wengi. Sasa kama wenzetu huko wenye huduma bora za afya na kufuata tahadhari zote wengine hadi lockdown ila bado unasikia maelefu ya watu wanakufa kwa siku ndio maana ikaonekana afrika tutaokota maiti barabarani,kuna muda hadi kulitokea ule uvumi wa kwamba hospitali zimezidiwa wagonjwa Tz,ila sasa hivi inaonekana tatizo hatuna takwimu story za maiti barabarani na hospitali kuzidiwa wagonjwa hazipo tena.
 

Ni sahihi Mkuu.
 
Sikiliza wakenya wanavyopinga hayo mambo ya corona na mikopo inayoendelea kuwanyonga.
Lengo la WHO ni kutaka kufanya corona biashara.
Kama nchi tukikataa hizo chanjo na mikopo wao wanaona hasara.
Kenya toka wamefanya hiyo tahadhali mpaka sasa hakuna mafanikio zaidi ya kuongeza karantini kwa sasa kuingia nairobi na kuongeza mikopo ambayo sasa inaenda kufika tilioni saba za wakenya kama watapokea hizo dora bilioni 2.
Sasa nyie mnaotaka corona iwe biashara mna nini mnataka kukiuza hapa tanzania?
Wanaoshabiakia corona hapa tz ni wale wanaotaka kuuza ma barakoa na ma sanitizer mliorundika kwenye mastoo yenu.
Mengine hakuna.
 
Nadhani ametumia hekima na busara kulisemea jambo hili.Kwanza kutoleta hamaki kwa watanzania ambao bado tuko wajinga kwa kuamini kuwa Maombi tu yataondoa Covid -19 huku watu wanakufa!
Pili anajaribu kuishawishi Jumuia ya Kimataifa ambayo inaamini kuwa kuna Covid-19 Tanzania lakini Serikali inapuuza hivyo kuitenga kimataifa.
Kwa sasa nachoona Mama anatujenga watanzania kwa kugusa yale yaliyotumiza ili tuweze kumwamini kwamba ataweza kutuongoza kupambana na changamoto zinazotukabili.
 
Takwimu za huo ugonjwa hakuna anayejua..kwa hio watu hawaez kuchukua tahazar bila kujua takwim.mama yuko sahihi lazima tujue hLi yetu
Kwamba kuvaa barakoa na kunawa mikono hadi ujue takwimu?
 
Kwahio unataka muendelezo wa kufanya mambo ya kitaalamu, Kisiasa ?

Yeye pale ni mwanasiasa unataka a-solve mambo ya Kiafya (ambayo sio utaalamu wake)
 
Sasa kulikuwa kunahitaji hadi iundwe kamati ndio ijekusema kuwa sasa tuvae barakoa na kunawa mikono,tunaona hawashikani mikono tunajua hiyo ni katika tahadhari za kujikinga na corona,sasa ni kamati gani iliyowaambia wasivae barakoa na wakusanyane ila wasishikane mikono tu? dunia nzima tunaona wanavaa barakoa hadi waliyochanjwa chanjo za corona ila Tz ndio hadi tuunde kamati ndio wataalamu wetu watushauri hivyo.
 
wacha tusikie hiyo kamati ni ipi n itakuja na ushauri gani
 
Ndio hapo alipojificha nyuma ya kamati,kuhimiza watu wavae barakoa (kwa kuanza na yeye) pamoja na kunawa mikono kuna mtu angesema ni dikteta au anafanya maamuzi yasio ya kitaalamu?
 
Kweli kabisa, wanasayasi wa dunia nzima tayari wameshasema kuna Covid-19 ambayo inaua bila kubagua watu, bara, dini wala hali ya maisha ya mtu. walishasema namna ya kujikinga ni kukaa mbali na mikusanyiko, kunawa mikono, kutakasa mikono, kuvaa barakoa na kuepuka safari zisizo za lazima. Wakaenda mbali zaidi kuwa wazee na wenye changamoto za maradhi mengine wako kwenye hatari zaidi, hakuna dawa bali kuna chanjo ambazo zinasaidia kidogo kutoa kinga na watu wameshaanza kupokea dose. Hivyo, kuunda kamati ili ijadili nini zaidi ya ku comply na WHO resolutions.

Labda cha kujali hapo ni tutumie chanjo ya wapi, Marekani, Uingereza, Urusi au Uchina? Nothing less nothing more about Covid-19.
 
Mama yuko sahihi pamoja na kuwepo kwenye awamu ya tano haimaanishi alishirikishwa na pengine maamuzi yalikuwa ni ya mtu mmoja. Tumwache afanye anachokiamini.
 
Huo msamiati "kujificha" ulioamua kuutumia kwe ye huu uzi ulitaka kumaanisha nini!?

Kama hujui na hujui taratibu basi elewa tuu kwamba Rais ametoa maagizo na wahusika wanayafanyia kazi

Raisi kajificha, 😂

Kwa lugha nyingine Raisi kajibanza mahali tusimuone, bahati mbaya kaacha traces ndio Mkuu anatuambia hapa kamuona alikojibanza.
 
Unataka tuweke lock down, huo ndio utaalam unaotaka, hao wenye lock down wanakufa wengi zaidi ya Tz sasa nini faida ya lockdown ? SSH ana tatizo, tena ni KUBWA.
Kuna watu wamemshika masikio ndio wanaongoza nchi kupitia mlango wa nyuma kwa kifupi kama rais ameonyesha udhaifu mkubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…