zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Mkemia aliharibu kwa kuzuia takwimu kuchukuliwa akidai wote wamepona kabisa. Sasa Mama anatoaje maamuzi bila analysis na tafiti ya kitaaluma?Magufuli alikuwa anakosolewa humu ni haki zao watu kukosoa wanapoona kuna makosa hivyo na Samia pia lazima nae akosolewe ukoasoaji haujaishia kwa Jiwe tu. Sasa Mama samia kwa kuanza kwa yeye kuvaa barakoa tu na kusisitiza na raia wavae barakoa ni jambo lenye kuhitaji ushauri wa kutoka kwenye kamati? Hoja ni kwamba anajificha nyuma ya kamati kwa kumuogopa nani wakati mwanzo tulishakuwa tumezuia mikusanyiko,kusisitiza kunawa mikono na kuvaa barakoa,level seat n.k hayo yote yalikuwa ni hatua za kitalaamua za kushughulika na corona ila tukaacha sasa hayo nayo ni ya kusubiri ushauri wa kamati wakati tulishayafanyaga huko mwanzoni?
Mwanzoni tulianza vizuri ila walipoingiza siasa wakaharibu kila kitu....