#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

Magufuli alikuwa anakosolewa humu ni haki zao watu kukosoa wanapoona kuna makosa hivyo na Samia pia lazima nae akosolewe ukoasoaji haujaishia kwa Jiwe tu. Sasa Mama samia kwa kuanza kwa yeye kuvaa barakoa tu na kusisitiza na raia wavae barakoa ni jambo lenye kuhitaji ushauri wa kutoka kwenye kamati? Hoja ni kwamba anajificha nyuma ya kamati kwa kumuogopa nani wakati mwanzo tulishakuwa tumezuia mikusanyiko,kusisitiza kunawa mikono na kuvaa barakoa,level seat n.k hayo yote yalikuwa ni hatua za kitalaamua za kushughulika na corona ila tukaacha sasa hayo nayo ni ya kusubiri ushauri wa kamati wakati tulishayafanyaga huko mwanzoni?
Mkemia aliharibu kwa kuzuia takwimu kuchukuliwa akidai wote wamepona kabisa. Sasa Mama anatoaje maamuzi bila analysis na tafiti ya kitaaluma?

Mwanzoni tulianza vizuri ila walipoingiza siasa wakaharibu kila kitu....
 
Mpendwa wetu alikua ni rais mnajim
Dunia nzima hili jambo limetesa sana
Ila Magu alielewa hii kitu imetokana vp

M/mungu alitaka kuwakumbusha watu wake kwamba wamemsahau vya kutosha hivyo haraka wamrudie

Ile Magu kutamka hadharani kua hili tuna mwachia m/mungu , bas hapo mungu akatupa kinga
Na nan ni mbora wa kinga isipokua ulinzi toka kwa mungu???????

Bas Hakimu Mfawidhi , jiandae hutokuja kusikia watu 800 wamekufa kwa siku kisa korona
Kama NYC, hutokuja kuona jiran zako wanakufa kama kuku.

Hili jambo ni mungu tu anatulinda.

NB: kinyume na msimamo wa mpendwa wetu
Tujiandae na mengi
Sema mpendwa wako na mama yako usitujumuishe sisi
 
Chanjo lazima Ili kutotengwa kimataifa, mbona mataifa mengine wametumia wewe ulitakaje
 
Magufuli alikuwa anakosolewa humu ni haki zao watu kukosoa wanapoona kuna makosa hivyo na Samia pia lazima nae akosolewe ukoasoaji haujaishia kwa Jiwe tu. Sasa Mama samia kwa kuanza kwa yeye kuvaa barakoa tu na kusisitiza na raia wavae barakoa ni jambo lenye kuhitaji ushauri wa kutoka kwenye kamati? Hoja ni kwamba anajificha nyuma ya kamati kwa kumuogopa nani wakati mwanzo tulishakuwa tumezuia mikusanyiko,kusisitiza kunawa mikono na kuvaa barakoa,level seat n.k hayo yote yalikuwa ni hatua za kitalaamua za kushughulika na corona ila tukaacha sasa hayo nayo ni ya kusubiri ushauri wa kamati wakati tulishayafanyaga huko mwanzoni?
Wasukuma mnamuandama mama, Samia ni Rais hadi 2045, amtaki ameni nchi
 
Kwa hali wanayopitia Kenya kwa sasa kwa sababu ya Corona, JPM ni shujaa wa Africa.
Huyo unayemsifia corona ndio ilimchukua then unampa sifa za bure tu. Jan na feb medical dept ya TZ ilifika breaking point ssa tulikua na tofauti gani na Kenya.

Shukuruni tu ile wave kwa TZ ilipita so waliokufa wamekufa waliopona ndio wapo kina mwandosya, mpango etc sasa jiwe alisaidia nini?
 
Hili suala!! Linahitaji tafiti Kweli za kisayansi, Ila maamzi yake yanahitaji Hekima kuliko huo utafiti wa kisayansi

Ni kweli kabisa lakini Rais kusema hatukuwa na msimamo kuhusu hili swala la Corona ni unafiki na uongo mkubwa!
 
Samia anaweza kuwa mjinga lakini ni wazi Magufuli alishughulika na Covid kilimbukeni kabisa (Primitive) ndiyo maana ilimuondoa, Naamini mama samia atashughulika nalo Kisayansi.
Usiwe Mpumbavu Hakuna Atakaye Ishi Milele, We Choko Whithout The Covid People Can Not Die? Sayansi Inatulazimisha Pia Tuvae Barakoa. Sijamuoa Huyo Mama Yenu Akivaa Barakoa... Hiyo Ni Signal Ya Unafiki Na Hatua Za Awali Kuonesha Rais Wenu Yupo Tu Kama Msukule, Kuna Watu Wameshika Remote
 
Wasalaam wana jamvi!

Nimeshangazwa sana na Mh Rais kusema ataunda kamati kuhusu swala la Corona ili baadae tuwe na msimamo kuhusu Corona!

Mimi kwenye hili nimejiuliza maswali hivi ni kweli Tanzania hatukuwa na msimamo kuhusu Corona? Huyu Rais si alikuwa Makamu wa Rais na Rais wake alishasema wazi kuwa Tanzania hakuna Corona na kama ipo ni ndogo sana?

Hii kamati anayounda anataka imwambie nini kipya asichokijua? Anataka aanze kutoa takwimu za Corona sasa anataka kamati imshauri?

Anataka aweke watu Lockdown sasa anataka kamati imshauri?

Anataka kulazimisha watu kuvaa barakoa sasa anataka kama imshauri?

Anataka kupokea chanjo ya Astrazeneca sasa anataka kamati imshauri?

Rais anaogopa nini kusema alikuwa hakubaliani na jinsi mtangulizi wake alivyo kuwa anaikabili Corona? Rais anaogopa nini kusema wamejiandaa kupokea chanjo ya Astrazeneca hivi karibuni?

Sidhani kama Rais anatakiwa kujificha nyuma ya kamati kwenye swala kama hili ambalo liko wazi!

Kuna kitu gani hajui ambacho anataka kamati imwambie?

Kwanini anajificha nyuma ya kamati anashindwa nini kuwambia watanzania wajiandae kudungwa Astrazeneca?

Kama Tanzania hatuna msimamo kwanini yeye havai barakoa? Hajui huo nao ni msimamo? Anataka ashauriwe nini?


Wasalaam!

Mama anania ya dhati ya kupambana na gonjwa hili. Kwa hatua anazochukua tutavuka.

Watu kama mleta mada mmetuchelewesha sana.
 
Anataka wamshauri nini asichojua? Huu nao ni uongo mtupu na upotevu wa pesa! Hivi kweli hatuna msimamo juu ya Corona? Leo hii amesahau kuwa avai barakoa? Hajui kutovaa Barakoa ni msimamo tayari?
Tungekuwa na msimamo tungezipimisha kware, mimbuzi , makondoo, mapapai na oil za magari maabara kuu ya taifa ?!

Odhis *
 
Mbona umelazimisha tu Astrazeneca kwani hakuna chanjo nyingine tofauti na hiyo?

Chanjo ambayo inatakiwa kuletwa tanzania ni Astrozeneca sasa Rais badala ya kuwambia watu wajiandae kudungwa yeye anasema ameunda kamati wakati anajua fika wameshakubali kuletwa chanjo ya Astrazeneca na alishaamua...kwanini anajificha nyuma ya kamati
 
FB_IMG_1616596917378.jpg

Tusubiri hiyo team itashauri nini, Alale salama JPM.
 
Mataga na wapiga vigelegele wa Sukuma gang mnapita katika kipindi kigumu sana.

Ghafla mmegeuka kuwa wapinzani. Hahahahaha

Sasa hii ina uhusiano gani na mada wewe kijana!
 
Sukumaz wamepoteana baada ya jamaa yao kusepa na mdudu. Wamebaki kumshambulia mama wa watu wakati Jiwe mwenyewe ndio alizembea mpaka ronaa ikasepa nae
Kilichomlaza JPM bado ni kitendawili. Bado kuna theory kuwa ni outside job kwa kushirikiana na insiders. Vita ya kiuchumi ni very real.

Vyovyote vile, kaacha alama mioyoni mwa watu isiyofutika kirahisi. Msifurahie kupita kiasi.
 
We mjinga nini?
Kwani Rais ni Daktari?
Na anafanya weledi kuwatumia wataalam kuliko yule alisema tuijfukize na kula Bupiji, halafu akaondoka yeye!

Mimi sio mjinga nimehoji!

Hivi Rais anapokuwa avai barakoa anafikiri amefata msimamo gani kuhusu Corona?
Anajificha nyuma ya kamati maana hata mtoto mdogo anajua fika kuwa kamati itamwambia afanye Lock down,watu wavae barakoa, Watu wajiandae na Astrazeneca!

Rais anaogopa kuonekana alikuwa kinyume na msimamo wa mtangulizi wake na hicho kichaka cha kamati ndio anataka kukitumia!
 
Unataka tuweke lock down, huo ndio utaalam unaotaka, hao wenye lock down wanakufa wengi zaidi ya Tz sasa nini faida ya lockdown ? SSH ana tatizo, tena ni KUBWA.
Mkuu una tkkwimu za waliokufa na korona hapa kwetu?
Wamekufa wengi kwa sababu wana records sisi unaweza hata kusema hakuna aliyekufa na korona na ukawa sahihi, maan a hatukichagua kusema hali halisi
 
Kwani chanjo ya corona ni astrazeneca tu??? Mbona umeshindwa hata kuficha upumbavu wako????

Nyie mapandikizi ya nchi jirani mliyojiunga Ccm Kwa sababu ya pandikizi mwenzenu Magufuli jiandaeni tu. Nchi inarudi kwenye sanity na sio ujinga na upumbavu wenu.

Rais yuko sahihi hafanyi maamuzi kwa kukurupuka, anasikiliza kwanza ushauri wa kitaalamu. Hivyo ndo dunia ya kisasa inavyokwenda

Mkuu punguza jazba

Kama Rais hajui msimamo wa nchi kuhusu Corona sasa kwanini amekuwa Rais?
Sasa kutovaa barakoa ni msimamo gani?
 
Back
Top Bottom