#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

Tunataka msimamo Kisayansi sio wa Huo wa wapiga nyungu akina Jafo . Na lile banda la Nyungu pale Muhimbili ling'olewe lipelekwe Makumbusho

Kutovaa Barakoa kwa Samia ni msimamo gani na aliutoa wapi? Kwanini ana danganya tanzania hatuna msimamo?
 
waTanzania mlishaanza kuwa masugu kwa kutawaliwa kinguvunguvu,
Magu akienda na kujiamulia kivyakevyake mkamuita dictator ,huyu nae akiita watu kushauriana nao na kuunda ushirika katika maamuzi mnamuona hana anachokijua.
Mna tatizo la mzoea vya kunyonga ambavyo vilikuwa vimeanza kutoa mizizi na miche .Ila mipango ya Mungu hakuna anaeijua.

Nimekuelewa lakini Rais asitudanganye kuwa Tanzania hatuna msimamo kuhusu Corona!

Atwambie kutovaa kwake Corona ni msimamo gani kuhusu Corona?
 
Yaani lazima niwe nimeugua corona ndio nione madhaifu ya Magufuli? Una akili timamu kweli?

Jambo la pili, huwezi kujifanya kichaa kwamba Tanzania haina corona wakati Dunia nzima ina corona et imungu ametusaidia, huyo mungu alishindwa nini kumsaidia magufuli corona isimuue?
Huyo mungu aliyeruhusu Magufuli afe na hiyo Corona ndiye huyo aliyeruhusu wewe usife na Corona??

Mbona ni kama unakichwa kikubwa lakini kumbe mavi tupu yamejaa kichwani
 
Yuko sahihi kabisa maana lazima ashauriwe kitaalam ili ajue ni njia ipi sahihi tunatumia, kama hujafanya utafiti huna mamlaka ya kusema lolote , huyu sio kama jiwe anasikiliza ushauri na anaongeza na zakwake baada ya kuambiwa, hapa Rais tunaye nyie masalia ya chattle mwacheni mama afanye kazi .

Sasa nani alimshauri asivae barakoa?
Hivi kweli unafikiri kamati inaweza kumshauri nini cha ziada kuhusu Corona?
 
Kamati itamshauri tupate chanjo, ya aina gani na kwa utaratibu gani.
Sasa nani alimshauri asivae barakoa?
Hivi kweli unafikiri kamati inaweza kumshauri nini cha ziada kuhusu Corona?
 
Mimi sio mjinga nimehoji!

Hivi Rais anapokuwa avai barakoa anafikiri amefata msimamo gani kuhusu Corona?
Anajificha nyuma ya kamati maana hata mtoto mdogo anajua fika kuwa kamati itamwambia afanye Lock down,watu wavae barakoa, Watu wajiandae na Astrazeneca!

Rais anaogopa kuonekana alikuwa kinyume na msimamo wa mtangulizi wake na hicho kichaka cha kamati ndio anataka kukitumia!

Mkuu kujitathmini mwenyewe kuhusiana na ujinga au werevu si sahihi sana.

Kwamba maamuzi ya wataalamu ni yapi, kwanini kuandikia mate?

Ushauri wa kitalaamu ni wa kuzingatiwa bila ya kujali utasema vipi.

Salama yetu iko ndani ya ushauri wa kitalaamu tu wala si vinginevyo.

Kumbuka kama social distancing inazingatiwa 100% hakuna haja ya barakoa wala lockdown.

Kama social distancing haiwezekaniki Barakoa ni lazima.

Kama kuna maeneo ugonjwa utapunguzwa kasi kwa udhibiti zaidi ikiwamo lockdown, na iwe hivyo!
 
Mtani Ruta . Rais Samia yuko sahihi kabisa . Hili jambo halitaki siasa wala mzuka. Nilishangaa mwaka Jana boss (RIP) alipotaka kuongelea hali ya Corona nchini. Badala ya kuita wataalamu wa afya, aliwaita wakuu wa vyombo vya Dola . Huyu ametaka kuwashirikisha wataalamu wahusika wa tatizo lenyewe.

Kinachowasumbua nyinyi wafuasi wa Jiwe ni kuwa hamuamini kuwa Jiwe limedondoka na halinyanyuki tena . Huyo amepita na zama zake.

Hata Magu enzi za Mkapa na Kikwete hukumsikia akisema neno. Lakini alipoingia akawananga . So is normal

Odhis *

Mtani mimi ninachosema Rais asiseme kuwa hatukuwa na msimamo kuhusu Corona maana itakuwa ni uongo na unafiki...
Hivi kweli unafikiri kamati itamshauri nini cha ziada asicho kijua?
Au ana ajenda zake anataka kuzipenyeza kwenye mgongo wa kamati?

Kwanini avai barakoa? Huo ni msiamo gani?
 
Wasalaam wana jamvi!

Nimeshangazwa sana na Mh Rais kusema ataunda kamati kuhusu swala la Corona ili baadae tuwe na msimamo kuhusu Corona!

Mimi kwenye hili nimejiuliza maswali hivi ni kweli Tanzania hatukuwa na msimamo kuhusu Corona? Huyu Rais si alikuwa Makamu wa Rais na Rais wake alishasema wazi kuwa Tanzania hakuna Corona na kama ipo ni ndogo sana?

Hii kamati anayounda anataka imwambie nini kipya asichokijua? Anataka aanze kutoa takwimu za Corona sasa anataka kamati imshauri?

Anataka aweke watu Lockdown sasa anataka kamati imshauri?

Anataka kulazimisha watu kuvaa barakoa sasa anataka kama imshauri?

Anataka kupokea chanjo ya Astrazeneca sasa anataka kamati imshauri?

Rais anaogopa nini kusema alikuwa hakubaliani na jinsi mtangulizi wake alivyo kuwa anaikabili Corona? Rais anaogopa nini kusema wamejiandaa kupokea chanjo ya AstraZeneca hivi karibuni?

Sidhani kama Rais anatakiwa kujificha nyuma ya kamati kwenye swala kama hili ambalo liko wazi!

Kuna kitu gani hajui ambacho anataka kamati imwambie?

Kwanini anajificha nyuma ya kamati anashindwa nini kuwambia watanzania wajiandae kudungwa Astrazeneca?

Kama Tanzania hatuna msimamo kwanini yeye havai barakoa? Hajui huo nao ni msimamo? Anataka ashauriwe nini?

Wasalaam!
Hiyo inaitwa "safe mode" au diplomatic approach, usipende kutafuniwa kila kitu, hatua za Rais mpaka sasa na body language yake vinaongea kwa sauti kubwa kuhusu mitazamo yake kuhusu mwendazake, kila mtu mwenye akili amemuelewa Rais, isipokuwa wewe tu ndio unasubiri kila kitu akutafunie kila kitu! sometimes you need to connect the dots to solve the equation, period.
 
Bado mnamboleza kifo cha Mungu wenu sio ? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Mungu hataki dhihaka mzee. Korona imemchukua jiwe wenu na sasa watu wamekuwa free kuexpress what they truly are, jiwe was a curse to this country.
Hadi sasa Mama Samia havai barakoa,mwanzo tulisema ni kwa sababu ya Jiwe ila sasa Jiwe hayupo ila bado Mama samia havai barakoa wala hata kusisitiza tu watu wavae barakoa.

Anamuogopa nani?
 
Nawasalimu kwa jina la JMT.

Muhimu, Mama asitumie nguvu.

Baadhi ya maoni ya Watanzania kuhusu chanjo..

View attachment 1746410

Mkuu tulio tayari kuchanjwa kabla yake ututake radhi.

Msimuwekee watanzania wote kama vile tumewatuma. Mbona mapendekezo yamekuwa wazi kabisa?

Achanjwe anayetaka. Msiokubali kuchanjwa hakuna anayewalazimisha. Ila kuvaa barakoa ni muhimu kuwa lazima. Hamuwezi kuachwa kutaka kuwaambukiza wengine kwa raha zenu. Au vipi jombi?
 
Kwenye suala la Corona lazima tukubali Magufuli alichemka big time.

Hakuna mtu mwenye akili timamu angekubaliana na Magufuli kwa jinsi alivyoishughulikia korona.

Huwezi kuwa dogma ukajifanya Tanzania haina korona wakati Dunia nzima ina korona eti mungu ametusaidia, huyo mungu alishindwa nini kumsaidia korona isimuue?

Nakubaliana na mama, shughulika na korona kitaalam.
Magu bwana alikuwa comedian haswa! Eti sisi anatwambia kwenye Korona tumtegemee Mungu wakati yeye kajizungushia mabunduki mia mia, sijui alishindwa nini kumtegemea Mungu amlinde badala ya bunduki chungu mzima! Mwache apite hivi? Sijui tumwite juha au mnafiki mkubwa?!
 
Tunataka msimamo Kisayansi sio wa Huo wa wapiga nyungu akina Jafo . Na lile banda la Nyungu pale Muhimbili ling'olewe lipelekwe Makumbusho
Mtaalamu wa nyungu alivaa barakoa , msibani , kwa kweli nilishangaa sana
 
Hadi sasa Mama Samia havai barakoa,mwanzo tulisema ni kwa sababu ya Jiwe ila sasa Jiwe hayupo ila bado Mama samia havai barakoa wala hata kusisitiza tu watu wavae barakoa.

Anamuogopa nani?

Na bado tunajiuliza kama anasema Tanzania hatuna msimamo kuhusu Corona sasa hebu tujiulize kama havai barakoa sasa huo ni msimamo gani kuhusu Corona?
 
Nimekuelewa lakini Rais asitudanganye kuwa Tanzania hatuna msimamo kuhusu Corona!

Atwambie kutovaa kwake Corona ni msimamo gani kuhusu Corona?
Hebu tuende kiroja kwa hoja tuandikie msimamo wa Tanzania kuhusu Covid 19.
 
magufuli alikuwa sahihi.
Kuhusu chanzo cha kifo chake umeshaambiwa sasa unapolazimisha kuwa alikufa na Corona unatia mashaka..
mbinu za kupambana na Corona za magufuli zilizaa matunda..
Mpaka sasa yanaonekana.
KUFA KWAKE NI AHADI ALIYOWEKEANA NA MUNGU WAKE
Kwenye suala la Corona lazima tukubali Magufuli alichemka big time.

Hakuna mtu mwenye akili timamu angekubaliana na Magufuli kwa jinsi alivyoishughulikia korona.

Huwezi kuwa dogma ukajifanya Tanzania haina korona wakati Dunia nzima ina korona eti mungu ametusaidia, huyo mungu alishindwa nini kumsaidia korona isimuue?

Nakubaliana na mama, shughulika na korona kitaalam.
 
Magu bwana alikuwa comedian haswa! Eti sisi anatwambia kwenye Korona tumtegemee Mungu wakati yeye kajizungushia mabunduki mia mia, sijui alishindwa nini kumtegemea Mungu amlinde badala ya bunduki chungu mzima! Mwache apite hivi? Sijui tumwite juha au mnafiki mkubwa?!

Sasa turudi kwenye mada huyo ameshakufa sisi tupo! Rais havai barakoa bado anasema Tanzania hatuna msimamo kuhusu Corona aoni kama anasema uongo na unafiki? Hajui kuwa kutovaa barakoa nao ni msimamo?
 
Back
Top Bottom