#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

Wasalaam wana jamvi!

Nimeshangazwa sana na Mh Rais kusema ataunda kamati kuhusu swala la Corona ili baadae tuwe na msimamo kuhusu Corona!

Mimi kwenye hili nimejiuliza maswali hivi ni kweli Tanzania hatukuwa na msimamo kuhusu Corona? Huyu Rais si alikuwa Makamu wa Rais na Rais wake alishasema wazi kuwa Tanzania hakuna Corona na kama ipo ni ndogo sana?

Hii kamati anayounda anataka imwambie nini kipya asichokijua? Anataka aanze kutoa takwimu za Corona sasa anataka kamati imshauri?

Anataka aweke watu Lockdown sasa anataka kamati imshauri?

Anataka kulazimisha watu kuvaa barakoa sasa anataka kama imshauri?

Anataka kupokea chanjo ya Astrazeneca sasa anataka kamati imshauri?

Rais anaogopa nini kusema alikuwa hakubaliani na jinsi mtangulizi wake alivyo kuwa anaikabili Corona? Rais anaogopa nini kusema wamejiandaa kupokea chanjo ya AstraZeneca hivi karibuni?

Sidhani kama Rais anatakiwa kujificha nyuma ya kamati kwenye swala kama hili ambalo liko wazi!

Kuna kitu gani hajui ambacho anataka kamati imwambie?

Kwanini anajificha nyuma ya kamati anashindwa nini kuwambia watanzania wajiandae kudungwa Astrazeneca?

Kama Tanzania hatuna msimamo kwanini yeye havai barakoa? Hajui huo nao ni msimamo? Anataka ashauriwe nini?

Kwanini Tusiamini ana ajenda zake mkononi anataka azipitishe nyuma ya kamati ili watanzania waamini ni msimamo wa kamati kumbe ni msimamo wake?

Wasalaam!
Mwendazake amewajaza ujinga watu mpaka akina Nshomile wamekuwa wajinga wa kutupa, uamuzi wa Rais ni sahihi kabisa kwa sababu kuna Chanjo aina nyingi kwa ugonjwa mmoja zikiwa zimegunduliwa na Taasisi tofauti za nchi tofauti, zinatengenezwa na kampuni tofauti na dawa za Chato pia zipo.
 
Kwenye suala la Corona lazima tukubali Magufuli alichemka big time.

Hakuna mtu mwenye akili timamu angekubaliana na Magufuli kwa jinsi alivyoishughulikia korona.

Huwezi kuwa dogma ukajifanya Tanzania haina korona wakati Dunia nzima ina korona eti mungu ametusaidia, huyo mungu alishindwa nini kumsaidia korona isimuue?

Nakubaliana na mama, shughulika na korona kitaalam.
Sasa Kwan JPM alikosea wapi kuhusiana na korona kwa sababu ukiangalia takwimu za waliochukua hizo tahadhali za kitaalamu ndo wanao ongoza kwa maambukizi na vifo mi naona JPM alikuwa sahihi kabisa
 
Mama anafanya mambo kitaalamu, ametulia kimya kusikiliza ushauri wa kitaalamu.

Usikivu nao ni kipaji kama vipaji vingine.

Kwa hiyo unataka kuniambia ana wasubiri wataalam wamwambie kuwa sasa aanze kuvaa barakoa?

Kwa hiyo kutovaa barakoa unaona ni msimamo gani?
 
Hakuna anaetaka lockdown, tatizo ni kukataa uwepo wa corona eti mungu katusaidia, huyo mungu alishindws nini kumsaidia magufuli aliuwawe na corona?

Japan, korea kusini na nchi nyingi hawana lockdown ila wanahimizana kuchukua tahadhari. Sisi hapa kiongozi anakataa ugonjwa huo haupo kwa maksudi tu sasa ugonjwa huo umemuua.
Kwani Mungu ndio aliyekwambia Magufuli kafa kwa corona? sisi tunajua kuwa kila mtu atakufa iwe kwa corona au sababu nyengine na ndio maana huko kwa wenzetu pamoja na tahadhari zote za kujikinga na corona ila bado watu wanakufa na corona hiyo hiyo,sasa hayo Magu kufa na corona una ushahidi nayo ili tuweze kusema kuwa Mungu wa Jiwe kashindwa kuzuia Jiwe asife kwa corona? Au unatumia tu kifo chake na kusingizia ni kifo cha corona wakati huna uhakika?
 
Wasalaam wana jamvi!

Nimeshangazwa sana na Mh Rais kusema ataunda kamati kuhusu swala la Corona ili baadae tuwe na msimamo kuhusu Corona!

Mimi kwenye hili nimejiuliza maswali hivi ni kweli Tanzania hatukuwa na msimamo kuhusu Corona? Huyu Rais si alikuwa Makamu wa Rais na Rais wake alishasema wazi kuwa Tanzania hakuna Corona na kama ipo ni ndogo sana?

Hii kamati anayounda anataka imwambie nini kipya asichokijua? Anataka aanze kutoa takwimu za Corona sasa anataka kamati imshauri?

Anataka aweke watu Lockdown sasa anataka kamati imshauri?

Anataka kulazimisha watu kuvaa barakoa sasa anataka kama imshauri?

Anataka kupokea chanjo ya Astrazeneca sasa anataka kamati imshauri?

Rais anaogopa nini kusema alikuwa hakubaliani na jinsi mtangulizi wake alivyo kuwa anaikabili Corona? Rais anaogopa nini kusema wamejiandaa kupokea chanjo ya AstraZeneca hivi karibuni?

Sidhani kama Rais anatakiwa kujificha nyuma ya kamati kwenye swala kama hili ambalo liko wazi!

Kuna kitu gani hajui ambacho anataka kamati imwambie?

Kwanini anajificha nyuma ya kamati anashindwa nini kuwambia watanzania wajiandae kudungwa Astrazeneca?

Kama Tanzania hatuna msimamo kwanini yeye havai barakoa? Hajui huo nao ni msimamo? Anataka ashauriwe nini?

Kwanini Tusiamini ana ajenda zake mkononi anataka azipitishe nyuma ya kamati ili watanzania waamini ni msimamo wa kamati kumbe ni msimamo wake?

Wasalaam!
Samia ni mzanzibar, na wazanzibari siku zote wana akili kubwa, mama hataki lawama ije kwake moja kwa moja ndio mana ataunda hiyo kamati ili ionekani kulikuwa na togetherness tofauti mwendazake ambaye yeye aliamini kauli yake inatosha kuabudiwa ni watanzania milioni 60. Kwa ufupi mama anatafuta mahala pazuri pa kujiweka kwa hii corona ili 2025 awe salama zaidi, ie Biden

Na uzuri wake hiyo kamati atateuwa vichogo kutoka kule kule tanganyika
 
Waulize kanisa katoliki wamapoteza watumishi wao wangapi kwa changamoto za upumuaji kwa kipindi cha miezi mitatu tu ya mwaka huu
Tanzania hakuna Corona kama nchi nyingine na hajaathiri kama nchi zingine ndio maana Rais Samia havai barakoa!

Huo ndio msimamo lakini nashangaa Rais Samia anashindwa kukiri tulikuwa na msimamo lakini hakuupenda na sasa ataanza kuvaa barakoa!

Lakini havai barakoa na bado anasema Tanzania hatukuwa na msimamo hahaha
 
Nimekuelewa na nina kubaliana na wewe kabisa lakini ninachopinga ni Rais kusema hatukuwa na msimamo wakati yeye hadi sasa havai barakoa!

Hivi anasubiri kamati ije kumshauri kuvaa barakoa?
Kwanini tusiamini kuwa ana ajenda anataka kuzipitisha nyuma ya kamati?

1. Mkuu ukiweza kuwa mbali na wengine walau kwa 1.5m toka mtu, barakoa haina ulazima tena. Ni muhimu sana kulielewa hili mkuu.

Wasiolielewa hili wanahangaika sana na mabarakoa hata wakiwa pekee yao vymbani wakidhihirisha umbumbumbu wao.

2. Kutokea hapo juu kigezo chako cha yeye kutovaa barakoa kinakuwa kimesambaratika chote.

Hivyo si sahihi kudhani kuwa anasubiri kushauriwa na kamati kuvaa barakoa. Havai pote unapokuwa yuko katika umbali salama.

3. Kwa mawili hayo hapo juu, ni wazi kuwa tuhuma zako hazina msingi wowote.

Au nasema uongo ndugu zangu?

Tumwache mama atusaidie kulitokomeza gonjwa hili linaloendelea kupukutisha maisha ya wapendwa wetu wengi.
 
Kwa hiyo unataka kuniambia ana wasubiri wataalam wamwambie kuwa sasa aanze kuvaa barakoa?

Kwa hiyo kutovaa barakoa unaona ni msimamo gani?
Eeeh! kama wataalamu wa MNH walivyoambiwa watengeneze sehemu ya kupigia nyungu very pathetic.

Bukoba unakuja lini poti.
 
Huo msamiati "kujificha" ulioamua kuutumia kwe ye huu uzi ulitaka kumaanisha nini!?

Kama hujui na hujui taratibu basi elewa tuu kwamba Rais ametoa maagizo na wahusika wanayafanyia kazi
 
Wasalaam wana jamvi!

Nimeshangazwa sana na Mh Rais kusema ataunda kamati kuhusu swala la Corona ili baadae tuwe na msimamo kuhusu Corona!

Mimi kwenye hili nimejiuliza maswali hivi ni kweli Tanzania hatukuwa na msimamo kuhusu Corona? Huyu Rais si alikuwa Makamu wa Rais na Rais wake alishasema wazi kuwa Tanzania hakuna Corona na kama ipo ni ndogo sana?

Hii kamati anayounda anataka imwambie nini kipya asichokijua? Anataka aanze kutoa takwimu za Corona sasa anataka kamati imshauri?

Anataka aweke watu Lockdown sasa anataka kamati imshauri?

Anataka kulazimisha watu kuvaa barakoa sasa anataka kama imshauri?

Anataka kupokea chanjo ya Astrazeneca sasa anataka kamati imshauri?

Rais anaogopa nini kusema alikuwa hakubaliani na jinsi mtangulizi wake alivyo kuwa anaikabili Corona? Rais anaogopa nini kusema wamejiandaa kupokea chanjo ya AstraZeneca hivi karibuni?

Sidhani kama Rais anatakiwa kujificha nyuma ya kamati kwenye swala kama hili ambalo liko wazi!

Kuna kitu gani hajui ambacho anataka kamati imwambie?

Kwanini anajificha nyuma ya kamati anashindwa nini kuwambia watanzania wajiandae kudungwa Astrazeneca?

Kama Tanzania hatuna msimamo kwanini yeye havai barakoa? Hajui huo nao ni msimamo? Anataka ashauriwe nini?

Kwanini Tusiamini ana ajenda zake mkononi anataka azipitishe nyuma ya kamati ili watanzania waamini ni msimamo wa kamati kumbe ni msimamo wake?

Wasalaam!
Utalimia meno sasa hivi
 
Wewe una akili sawa sawa? Yani hata yeye kuvaa barakoa ni hadi aunde kamati ndio imshauri avae barakoa na kwamba akivaa bila kushauriwa ni udikteta?
Kamati itamshauri, Mama akijiamulia tu kufanya mambo iko siku ataingia Ofisini na vazi la kuogelea sijui mtasemaje
 
Mi na familia yangu hatutachoma chanjo!
Hapo ndo nakumbuka magu
Dunia nzima hakuna aliyelazimishwa kuchanja. Chanjo ikiletwa Tanzania watachanjwa wanaotaka tu. Msiotaka no problem. Magufuli alichofanya ni kuwanyima fursa wanaotaka kuchanjwa kwa kuzuia chanjo isije kabisa Tanzania. Sasa serikali ikiamua chanjo ije tatizo litakuwa wapi?
 
Wasalaam wana jamvi!

Nimeshangazwa sana na Mh Rais kusema ataunda kamati kuhusu swala la Corona ili baadae tuwe na msimamo kuhusu Corona!

Mimi kwenye hili nimejiuliza maswali hivi ni kweli Tanzania hatukuwa na msimamo kuhusu Corona? Huyu Rais si alikuwa Makamu wa Rais na Rais wake alishasema wazi kuwa Tanzania hakuna Corona na kama ipo ni ndogo sana?

Hii kamati anayounda anataka imwambie nini kipya asichokijua? Anataka aanze kutoa takwimu za Corona sasa anataka kamati imshauri?

Anataka aweke watu Lockdown sasa anataka kamati imshauri?

Anataka kulazimisha watu kuvaa barakoa sasa anataka kama imshauri?

Anataka kupokea chanjo ya Astrazeneca sasa anataka kamati imshauri?

Rais anaogopa nini kusema alikuwa hakubaliani na jinsi mtangulizi wake alivyo kuwa anaikabili Corona? Rais anaogopa nini kusema wamejiandaa kupokea chanjo ya AstraZeneca hivi karibuni?

Sidhani kama Rais anatakiwa kujificha nyuma ya kamati kwenye swala kama hili ambalo liko wazi!

Kuna kitu gani hajui ambacho anataka kamati imwambie?

Kwanini anajificha nyuma ya kamati anashindwa nini kuwambia watanzania wajiandae kudungwa Astrazeneca?

Kama Tanzania hatuna msimamo kwanini yeye havai barakoa? Hajui huo nao ni msimamo? Anataka ashauriwe nini?

Kwanini Tusiamini ana ajenda zake mkononi anataka azipitishe nyuma ya kamati ili watanzania waamini ni msimamo wa kamati kumbe ni msimamo wake?

Wasalaam!
Scientific facts ni muhimu
 
Naamini katika taaluma..

Nimeshauri mama asitumie nguvu, maana yake endapo chanjo italetwa aende na ambao wako tayari, huku elimu na hamasa ikiendelea kutolewa kwa ambao hawako tayari.

Inapendeza sana kwa hili:

"Anayetaka kuchanjwa na achanjwe, kwa wakati na muda wake ambao yeye mwenyewe panapo majaliwa angependa."

Tupeane uhuru bila kujali cheo wala nafasi ya mtu katika jamii. Tusitishane wala kuchagizana kuwa nani aanze au nani aishie.

Si ndiyo ustaarabu mkuu?
 
Tanzania hakuna Corona kama nchi nyingine na hajaathiri kama nchi zingine ndio maana Rais Samia havai barakoa!

Huo ndio msimamo lakini nashangaa Rais Samia anashindwa kukiri tulikuwa na msimamo lakini hakuupenda na sasa ataanza kuvaa barakoa!

Lakini havai barakoa na bado anasema Tanzania hatukuwa na msimamo hahaha
Kiutaalamu anaetakiwa kuvaa barakowa ni mwenye maradhi na sio aliekuwa hana maradhi ,hata hio chanjo ni lazima uweke sahihi yako ili ikikudhuru pasiwepo na lawama na umoja wa WHO haijalazimisha imetua neno watu washawishiwe mpaka washawishike kukubali kudungwa hio chanjo,sa ivi zipo aina nyingi tu.

Mtu kama hataki kudungwa halazimishwi itabidi atongozwe na serikali mpaka akubali,mfano hupandi SGR,hupandi mabasi ya mwendo kasi huruhusiwi kuingia kwenye wizara za serikali ,kwa nini kwa sababu umekataa kudungwa chanjo ,hizo ndio njia zinazotumika au zinaanza kutumika huko majuu. Ili mtu akubali ,hili la ndege nasikia lipo njiani hupandi ndege kama hujadungwa chanjo.

hata ukidungwa bado unaambiwa uwe unafanyiwa test wakati wa kusafiri.
 
Kukikuwa na stand ya hovyo
Sasa si aseme wazi, kwa nini anataka kujificha nyuma ya watu wengine, she’s weaker na ni loudspeaker ya Brussels, London na Washington, hatuna Rais, tuna jokeli tu wa kuteleza chochote anachoambiwa na mabeberu huko.
 
Usiwe Mpumbavu Hakuna Atakaye Ishi Milele, We Choko Whithout The Covid People Can Not Die? Sayansi Inatulazimisha Pia Tuvae Barakoa. Sijamuoa Huyo Mama Yenu Akivaa Barakoa... Hiyo Ni Signal Ya Unafiki Na Hatua Za Awali Kuonesha Rais Wenu Yupo Tu Kama Msukule, Kuna Watu Wameshika Remote

Mbona unatokwa na povu, tulia dawa ikuingie vema , sawa hakuna atakeye ishi milele ila kuna vifo vingine vya Kiboya, mzee kafa Kiboya sana yaani. Kuvaa Barakoa ni moja tu ya njia za kujikinga na Covid.

Huyo mzee wenu alisema Mungu ameondoa Corona Tanzania, Mungu ametupa akili tuzitumie nyie mnazitumia kwa kupiga ramli matokeo yake ndiyo hayo, Covid imemchomoa, wenye akili zao walikuwa wana Mzoom tu mwamba, Mmebaki nyie mnatatarika kama maindi ya Bisi.
 
Back
Top Bottom