Kwanini Rais amepoteza mvuto kabla ya kutimiza siku 100?

Kwanini Rais amepoteza mvuto kabla ya kutimiza siku 100?

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Habari wanaJF,

Katika uwanja wa siasa kwa ngazi ya Urais tumezoea kuona Rais aliyeingia Madarakani akijizolea umaarufu na sifa kedekede pindi anaposhika hatamu ya uongozi

Kipimo cha Rais huanza ndani ya siku 100 tangu ale kiapo. Lakini imekuwa kinyume kwa Rais wa sasa amekuwa wa kawaida sana ndani ya muda mfupi.

Nadhani yafuatayo yamechangia yeye kupoteza mvuto kwa kasi:

- Hotuba zake zimekosa msisimko, nadhani ni kwasababu Waandishi wake wamekuwa waki-copy na kupaste hotuba zake. Kila hotuba tunasikia yale yale (Taifa kufiwa, Jinsia yake, lazima aombe epewe muda nk)

- Wizara ya Habari inamuangusha kwa 100% watu wanatamani kuona ubabaishaji unaondoka Serikalini lakini ndani ya wiki Moja Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imetoa maboko mara mbili (1: BASATA na Wasanii, 2: Mechi ya Simba SC vs Yanga SC)

- Kuendelea kuwepo Madarakani kwa baadhi ya Watendaji ambao Wananchi tuliamini walipaswa kuondoka baada ya zama za Mwendazake kuisha. Ameondoka mmoja tu, yule aliyekuwa boss wa Manispaa ya Temeke. Lakini bado kuna wengine wengi wanapaswa kupumzishwa.

Hayo ni kwa uchache, nakushauri fanya yafuatayo kujinusuru dhidi ya chuki na visirani vya Wananchi kabla haujachelewa.

- Safisha Serikali yako, baki na watu Wenye weledi tu (mfano ni Mama wa Afya anapaswa kupumzika ametulaghai sana)

- Kama kuna wafungwa wa kisiasa basi nakusihi wape uhuru wao. Familia zao zinawapenda na kuwahitaji.

- Ile ripoti ya matumizi ya fedha Serikalini ambayo uliomba bado haijakamilika? kama tayari basi tuweke wazi na ikiwezekana watu wawajibike kama kuna makandokando

- Usijidanganye ukaendelea kugawa Mabenz ya Serikali au ya fedha za walipa Kodi. Wananchi hatuoni mantiki ya kufanya hivyo.

- Acha kuwa na hotuba zinazojirudia rudia. Siku hizi ukianza tu tunajua unakoelekea.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Jamani wafuasi wa Jiwe hebu muacheni Mama afanye kazi zake. Mbona Jiwe kila alipohutubia ni yale yale. Alikuwa na mapya yapi au msisimko upi?!

Kwa ujumla unayoyaona ni madhaifu yaliomo ndani ya chama. Na tusitarajie makuuubwa kwa mama , kwa sababu waliomzunguka kuanzia usalama, chamani, serikalini all most ni wale wale.
 
Hii haihusiani na ufuasi wa nani na nani?
 
Kwa Mataga na lile genge la kikabila waumini kindaki ndaki wa awamu ya tano, mama hana mvuto.
Kumbe wewe ni mataga😂😂😂
Hebu tuambie mvuto upi umepotea
 
Jamani wafuasi wa Jiwe hebu muacheni Mama afanye kazi zake. Mbona Jiwe kila alipohutubia ni yale yale. Alikuwa na mapya yapi au msisimko upi?!

Kwa ujumla unayoyaona ni madhaifu yaliomo ndani ya chama. Na tusitarajie makuuubwa kwa mama , kwa sababu waliomzunguka kuanzia usalama, chamani, serikalini all most ni wale wale.

Mama ana kauli nyingi tamu tamu matendo zero.Malkia mwenye kauli tamu “in Lissu voice”
 
Back
Top Bottom