Kwanini Rais amepoteza mvuto kabla ya kutimiza siku 100?

Kwanini Rais amepoteza mvuto kabla ya kutimiza siku 100?

Jamani wafuasi wa Jiwe hebu muacheni Mama afanye kazi zake. Mbona Jiwe kila alipohutubia ni yale yale. Alikuwa na mapya yapi au msisimko upi?!

Kwa ujumla unayoyaona ni madhaifu yaliomo ndani ya chama. Na tusitarajie makuuubwa kwa mama , kwa sababu waliomzunguka kuanzia usalama, chamani, serikalini all most ni wale wale.
Wewe na mleta Uzi wote ni wapuuzi!!
 
Kiswahili ni kigumu.

Swali huwa lina alama (?).

Panapo hiyo ni kukosa kuelewa tu, kudhani unaambiwa au hata kupata wazo kuwekewa neno achilia mbali mdomoni.

Shida yako wewe ni kutaka kila mtu awe kile unachokitaka wewe
 
Rekebisha kichwa cha habari.maudhui Yako yamejaa ushauri tofauti na kichwa cha habar.nakushauri kichwa cha habari kisomeke hivi mh rais tupia jicho mambo haya ili kuendana na falsafa Yako.
Ushauri umepokelewa lakini si lazima nilifanyie kazi
 
Usiniwekee maneno mdomoni..... nimeachana na nani?
Serikali yetu ipo imara
Huwezi mlinganisha SAMIA SULUHU au DR MPANGO na SALUM MWALIMU au TUNDU

Kumbe ilibidi ukarekebishe zaidi? Mstari wa kwanza nilishaujibu.

Mstari mpya wa pili kuwa umeachana na nani? Pia ni kutokana na kutolewa kiswahili.

"Nao" - wazi wazi ilikuwa ni u-Mataga.

Mengine yaliyofuata ni utopolo ule ule tokea kwa Mataga na lile genge ambalo kiswahili siyo lugha yao ya taifa.

Ukweli mchungu:

IMG_20210510_071631_070.jpg


Tulieni hivyo hivyo kazi inapoendelea.
 
Kumbe ilibidi ukarekebishe zaidi? Mstari wa kwanza nilishaujibu.

Mstari mpya wa pili kuwa umeachana na nani? Pia ni kutokana na kutolewa kiswahili.

"Nao" - wazi wazi ilikuwa ni u-Mataga.

Mengine yaliyofuata ni utopolo ule ule tokea kwa Mataga na lile genge ambalo kiswahili siyo lugha yao ya taifa.

Ukweli mchungu:

View attachment 1779464

Tulieni hivyo hivyo kazi inapoendelea.


Chadema mna nongwa kama nywele
 
Habari wanaJF,

Katika uwanja wa siasa kwa ngazi ya Urais tumezoea kuona Rais aliyeingia Madarakani akijizolea umaarufu na sifa kedekede pindi anaposhika hatamu ya uongozi

Kipimo cha Rais huanza ndani ya siku 100 tangu ale kiapo. Lakini imekuwa kinyume kwa Rais wa sasa amekuwa wa kawaida sana ndani ya muda mfupi.

Nadhani yafuatayo yamechangia yeye kupoteza mvuto kwa kasi:

- Hotuba zake zimekosa msisimko, nadhani ni kwasababu Waandishi wake wamekuwa waki-copy na kupaste hotuba zake. Kila hotuba tunasikia yale yale (Taifa kufiwa, Jinsia yake, lazima aombe epewe muda nk)

- Wizara ya Habari inamuangusha kwa 100% watu wanatamani kuona ubabaishaji unaondoka Serikalini lakini ndani ya wiki Moja Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imetoa maboko mara mbili (1: BASATA na Wasanii, 2: Mechi ya Simba SC vs Yanga SC)

- Kuendelea kuwepo Madarakani kwa baadhi ya Watendaji ambao Wananchi tuliamini walipaswa kuondoka baada ya zama za Mwendazake kuisha. Ameondoka mmoja tu, yule aliyekuwa boss wa Manispaa ya Temeke. Lakini bado kuna wengine wengi wanapaswa kupumzishwa.

Hayo ni kwa uchache, nakushauri fanya yafuatayo kujinusuru dhidi ya chuki na visirani vya Wananchi kabla haujachelewa.

- Safisha Serikali yako, baki na watu Wenye weledi tu (mfano ni Mama wa Afya anapaswa kupumzika ametulaghai sana)

- Kama kuna wafungwa wa kisiasa basi nakusihi wape uhuru wao. Familia zao zinawapenda na kuwahitaji.

- Ile ripoti ya matumizi ya fedha Serikalini ambayo uliomba bado haijakamilika? kama tayari basi tuweke wazi na ikiwezekana watu wawajibike kama kuna makandokando

- Usijidanganye ukaendelea kugawa Mabenz ya Serikali au ya fedha za walipa Kodi. Wananchi hatuoni mantiki ya kufanya hivyo.

- Acha kuwa na hotuba zinazojirudia rudia. Siku hizi ukianza tu tunajua unakoelekea.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Ivi nyie mmerogwa au??
 
Back
Top Bottom