Uchaguzi 2020 Kwanini Rais anajitangazia ushindi?

Englishlady

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2013
Posts
2,736
Reaction score
3,644
Hii ya Rais wa sasa kuwakataza wateule wake wasiende kugombea eti kuwa waridhike na akiwataka kuingia kwenye Baraza la Mawaziri atawateua.

Najiuliza ameshajihesabia kuwa ameshashinda? Kwa Mamlaka gani ambayo anayo na kujihakikishia ushindi? What if akapigwa za uso?

Anyway, nimejiuliza pia hawa wateule kushupaza shingo ni kuwa wanajua hatapita? He he he! Wameamua wajiendee mjengoni wakawe wapinzani, au hawakuridhika na utendaji kazi wake wameona waende kwenye muhimili mwingine?

Nawaza tu jamani, kuwaza ni kukomaza ubongo.
 
Yaani kwa matarajio yako kuna kidampa anaweza kupambana na JPM. Sio tu ndani ya Tanzania Rais John Pombe Magufuli ni kiongozi wa mfano Afrika na Dunia.
 
Sasa kwa akili yako unafikiri kwa vile Membe anakubalika na kikundi chabwatu wake wa Rondo basi atashinda Urais?
 
Hata kama ni siasa, ni vyema majaliwa ya mwanadamu yakawekwa mikononi mwa Muumba wake. Hakuna kitu kibaya kama kuwa na kiburi cha uzima kutokana na madaraka ama utajiri.

Pengine labda tukuchulie alikuwa akifanya utani tu kwa wateule wake, ijapokuwa kwa kumaanisha ni yeye mwenyewe ambaye ndiye aliyewatuma kutia nia kwa malengo yake ya baadaye.
 
Yaani kwa matarajio yako kuna kidampa anaweza kupambana na JPM.
Sio tu ndani ya Tanzania Rais John Pombe Magufuli ni kiongozi wa mfano Africa na Dunia.
Nakumbuka kauli ya polepole wakati tupo mkutano wa UVCCM vijana jiungeni Jamiiforums mkapambane na hoja tutawaona haujaonywa tu bado boss?
 
Hata kibaka mzoefu wa kuikwapua simu huwa anabajeti anakopa bangi kwa uhakika wa kulipa akishaiba hiyo simu. Hana wasiwasi wa kukamatwa na kupigwa kipigo cha mbwa koko.
 

Hili la msingi sana hatujui ya kesho.

Kumkataza mtu kutimiza ndoto zake huku wewe ukiwa hujui kama kesho utaishi ama utashinda si jambo jema hata kidogo.
 
Kwanini ajitangazie?

Asubiri tume itangaze.

Au tunaenda kupiga kura za nini? Si aache tu tuelewe moja
Kwani mkuu tume na Magufuli wana tofauti gani?huyu faza anajulikana toka huko nyuma kwamba anawateuwa watu kwa kazi fulani na mshahara wanalipwa but unamkuta tena yeye ndiye anaye-act kuongoza zile idara alizofanya teuzi tayari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani kwa matarajio yako kuna kidampa anaweza kupambana na JPM.
Sio tu ndani ya Tanzania Rais John Pombe Magufuli ni kiongozi wa mfano Africa na Dunia.
Kuna maandamano makubwa apa Italia wanataka aende akawe kiongozi wao.
 
Ndugu wana jf tuwe na majibizano ya kiungwana,tuache utani na mizaha katika maoni au mawazo mbadala ya wengine,kila mtu ana maono yake
Tujibu kwa hoja na si jazba
 
Englishlady,

Tazama Ramani, utaona nchi nzuri.
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka.

Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri.
Nchi iliyo mashuhuri huitwa Tanzania.

Majira yetu haya, yangekuwaje sasa?
Utumwa wa Nchi, Magufuli ameukomesha.


Chemichemi ya furaha, amani matumaini
Nitalalamika kukuacha Tanzania.
 

Sasa kwanini tunaingia kwenye uchaguzi? tunapoteza pesa bure, aendelee tu kama tayari ni rais, tuchague wabunge tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…