Kwanini Rais Magufuli alimfunga Kabendera?

Kwanini Rais Magufuli alimfunga Kabendera?

mike2k

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2016
Posts
1,571
Reaction score
3,448
Ndugu wanajamvi,

Tumesikia kuhusu kitabu kipya cha Erick Kabendera kinachoitwa "In the Name of the President: The Memoirs of a Jailed Journalist". Kabendera amefunguka kwa kina juu ya utawala wa Magufuli na madai ya udikteta. Hii inatufanya tujiulize maswali mengi kuhusu sababu halisi za kufungwa kwake.

Ni wazi kuwa Kabendera alikuwa mwandishi wa habari shupavu, lakini je, hatua za kumkamata na kumfungia zilikuwa za haki? Au zilikuwa juhudi za kumnyamazisha kwa sababu ya uandishi wake?

Kwa vile tunafahamu kwamba baadhi ya wanachama wetu hapa ni wafanyakazi wa idara za usalama, jeshi, na ulinzi, wafanyakazi wa ikulu na watumishi wa inner circle tunapenda kupata mitazamo yenu juu ya suala hili:

1. Je, ni nini hasa kilichosababisha Kabendera kuonekana tishio kwa utawala wa Magufuli?

2. Kuna ukweli wowote katika madai kuwa utawala huo ulitumia nguvu za dola kuzima uhuru wa vyombo vya habari?

3. Kwa maoni yenu, je, kufungwa kwa Kabendera kulikuwa na athari gani kwa tasnia ya uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania?

4. Kwa nini utawala wa Magufuli ulikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya waandishi wa habari huru kama Kabendera?

Tunaomba mjadala huu uwe wa kistaarabu, wa kina, na wa kuheshimu maoni tofauti. Ikiwezekana, tusaidiane kupata ukweli ili kuangazia mustakabali wa uhuru wa vyombo vya habari nchini mwetu. Jambo zuri ni kwmaba mzee hayupo tena kwa sababu kipindi cha utawala wake hadi hili jukwaa la siasa lilikuwa compromised. Niliwahi kupost threads zenye hoja na zilifutwa na maadmin bila sababu hali hii ikasababisha nilichukie sana hili jukwaa la siasa.

Karibuni kwa mjadala.

IMG_4806.jpeg
 
Kibendera kaandika kitabu Kwa ajili ya maslahi yake binafsi ya kufedha, pamoja na kujipa relief kutokana na uchungu alionao baada ya kuenyeshwa sana na serikali ya Magufuli uliompelekea kupoteza mzazi....!!

Na kafanya hivyo sababu Kuna wenzake wengi sana ambao bado wana uchungu kama yeye na wanahitaji relief ambapo wataipata kwa kumpa support ya kununua na kukisoma hicho kitabu.

Ila Kwa bahati mbaya kwao hakuna chochote kitakachabadili image na mitazamo waliyonayo watanzania kuhusu Magufuli.

Eti ameona aandike Kwa lugha ya kigeni kabisa hahahhaha..!!
 
Jidanganye
 
Hàya majibu ànayo Pascal Mayalla , ilisemekana ndo alimchoma kabendera kwa Magufuli. Hii ni inasemekana mimi sina uhakika.
Huyu jamaa alikuwa ànatumia feki I'd huko "gazetini" kuandika màmbo ya "kuçhafua nchi"! Mayalla akamweka wazi kwa home boy wake.
Kuna page ya kabendera imemwandika Pascal Mayalla.
Yaani Kabendera kusema Serikali ya ccm ninya kifisadi tena akianishia namna ufisadi unavypanyika. Kwa mtu mwema angesema Mwandishi amemsaidi kuibua wizi. Lakini yeye wala hana habari ndio kwanza anakutia ndani eti unaichafua serikali yake.
 
Kabendera ni mwandishi wa habari za kiuchunguzi [Investigative Journalism] ni watu wanaokuwa katika hatari ya kupoteza maisha au kufungwa maana muda mwingine huingia katika anga za hatari.

Azory Gwanda akichunguza masuala ya Kibiti alipotea hadi leo.

Stan Katabaro akichunguza kashfa ya uuzwaji wa Loliondo[ Loliondo gate ] aliuwawa.

Nakuwekea hapa makala ya Gold Mafia kutoka Al Jazeera uone wandishi wa namna hiyo wanavyoingia kupekenyua data katika mazingira magumu.

Gold Mafia ni skendo iliyomuhusisha rais wa Zimbabwe na wasaidizi wake wakiwemo ndugu kufanya utakatishaji pesa wa mamilioni ya dola kupitia biashara ya dhahabu.

Angalia waandishi walivyokuwa wakiingia anga za hatari kupata data na ukweli juu ya utakatishaji pesa uliohusisha hadi rais wa nchi ya Zimbabwe.

View: https://youtu.be/evWEuVR1XIs?si=tKtDsSzJYBL1Lj_u
 
Ndugu wanajamvi,

Tumesikia kuhusu kitabu kipya cha Erick Kabendera kinachoitwa "The Name of the President: The Memoir of a Jailed Journalist". Kabendera amefunguka kwa kina juu ya utawala wa Magufuli na madai ya udikteta. Hii inatufanya tujiulize maswali mengi kuhusu sababu halisi za kufungwa kwake.

Ni wazi kuwa Kabendera alikuwa mwandishi wa habari shupavu, lakini je, hatua za kumkamata na kumfungia zilikuwa za haki? Au zilikuwa juhudi za kumnyamazisha kwa sababu ya uandishi wake?

Kwa vile tunafahamu kwamba baadhi ya wanachama wetu hapa ni wafanyakazi wa idara za usalama, jeshi, na ulinzi, tunapenda kupata mitazamo yenu juu ya suala hili:

1. Je, ni nini hasa kilichosababisha Kabendera kuonekana tishio kwa utawala wa Magufuli?

2. Kuna ukweli wowote katika madai kuwa utawala huo ulitumia nguvu za dola kuzima uhuru wa vyombo vya habari?

3. Kwa maoni yenu, je, kufungwa kwa Kabendera kulikuwa na athari gani kwa tasnia ya uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania?

4. Kwa nini utawala wa Magufuli ulikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya waandishi wa habari huru kama Kabendera?

Tunaomba mjadala huu uwe wa kistaarabu, wa kina, na wa kuheshimu maoni tofauti. Ikiwezekana, tusaidiane kupata ukweli ili kuangazia mustakabali wa uhuru wa vyombo vya habari nchini mwetu.

Karibuni!

View attachment 3191541
Kabendera alikuwa anatumika na watu wa nje kumhujumu Magufuli alitaka kupindua utawala wa Magu.
Mwandishi wa habari unaandika artcles 4 kwa mwezi kwenye akaunt yako unalipwa million 300. Unachomoa pesa unazitawanya kwa wakosoaji wa serikali mitandaoni. Hiyo investigative journalism kilikuwa kichaka cha money laundering alikuwa anatumika kwa kazi maalum kazi chafu.
 
Kibendera kaandika kitabu Kwa ajili ya maslahi yake binafsi ya kufedha, pamoja na kujipa relief kutokana na uchungu alionao baada ya kuenyeshwa sana na serikali ya Magufuli uliompelekea kupoteza mzazi....!!

Na kafanya hivyo sababu Kuna wenzake wengi sana ambao bado wana uchungu kama yeye na wanahitaji relief ambapo wataipata kwa kumpa support ya kununua na kukisoma hicho kitabu.

Ila Kwa bahati mbaya kwao hakuna chochote kitakachabadili image na mitazamo waliyonayo watanzania kuhusu Magufuli.

Eti ameona aandike Kwa lugha ya kigeni kabisa hahahhaha..!!
Kikubwa, kama jamii tutafute njia ya kuponya ikiwemo kuondoa vimelea au masalia ya yale aliyoayaasisi ambayo hayakuwa mazuri na hili itawezekana kama tutasoma na kuielewa sura ya mwisho ya Kitabu cha Kabendera.
 
Kabendera alikuwa anatumika na watu wa nje kumhujumu Magufuli alitaka kupindua utawala wa Magu.
Mwandishi wa habari unaandika artcles 4 kwa mwezi kwenye akaunt yako unalipwa million 300. Unachomoa pesa unazitawanya kwa wakosoaji wa serikali mitandaoni. Hiyo investigative journalism kilikuwa kichaka cha money laundering alikuwa anatumika kwa kazi maalum kazi chafu.
MWANDISHI APINDUE SERIKALI? ANA JESHI?
 
Back
Top Bottom