Ndugu wanajamvi,
Tumesikia kuhusu kitabu kipya cha Erick Kabendera kinachoitwa "The Name of the President: The Memoir of a Jailed Journalist". Kabendera amefunguka kwa kina juu ya utawala wa Magufuli na madai ya udikteta. Hii inatufanya tujiulize maswali mengi kuhusu sababu halisi za kufungwa kwake.
Ni wazi kuwa Kabendera alikuwa mwandishi wa habari shupavu, lakini je, hatua za kumkamata na kumfungia zilikuwa za haki? Au zilikuwa juhudi za kumnyamazisha kwa sababu ya uandishi wake?
Kwa vile tunafahamu kwamba baadhi ya wanachama wetu hapa ni wafanyakazi wa idara za usalama, jeshi, na ulinzi, tunapenda kupata mitazamo yenu juu ya suala hili:
1. Je, ni nini hasa kilichosababisha Kabendera kuonekana tishio kwa utawala wa Magufuli?
2. Kuna ukweli wowote katika madai kuwa utawala huo ulitumia nguvu za dola kuzima uhuru wa vyombo vya habari?
3. Kwa maoni yenu, je, kufungwa kwa Kabendera kulikuwa na athari gani kwa tasnia ya uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania?
4. Kwa nini utawala wa Magufuli ulikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya waandishi wa habari huru kama Kabendera?
Tunaomba mjadala huu uwe wa kistaarabu, wa kina, na wa kuheshimu maoni tofauti. Ikiwezekana, tusaidiane kupata ukweli ili kuangazia mustakabali wa uhuru wa vyombo vya habari nchini mwetu.
Karibuni!
View attachment 3191541