Kwanini Rais Magufuli alimfunga Kabendera?

Waliokupeleka shule hawakukosea!
 
Hata Mimi nilimkubali sana Magufuli kwa mengi, lakini kuna maeneo alikuwa anakosea mpaka unashangaa kiongozi mkubwa kama yeye anawezaje kufanya hayo?

Mfano:
1. Kutangaza hadharani kutokumwelewa mkurugenzi yeyote atakayemtangazia ushindi wa ubunge mgombea wa upinzani ilhali analipwa na kuhudumiwa na Serikali!

2. Kutangaza waziwazi nia yake ya kuufuta upinzani nchini wakati ni Serikali ndiyo iliyouruhusu mfumo wa vyama vingi!

3. Kuwanunua wapinzani kwa kisingizio cha kuungwa mkono!

4. Kuwapeleka kibabe bungeni wabunge 19 wa viti maalum kinyume cha utaratibu baada ya kujizolea nafasi zote za ubunge na hivyo kukosekana kwa wabunge wa upinzani bungeni!

5. Kutangaza kutoyapa kipaumbele cha maendeleo maeneo yanayoongozwa na wapinzani!
 
Gaidi aliyejitoa mhanga ili wewe uliyeshiba maharagwe uone faida za kodi yako unayolipa seeikalini.
Aliyejitoa muhanga kwenye nini? Aliikuta nchi vitani?
 
Mafanikio mojawapo ya kitabu ni kusomwa na watu wengi. Naamini hajawaandikia Watanzania pekee, bali ulimwengu. Na Watanzania wanapenda kusoma vitabu, wengi wao wanajua English pia. Kwa hiyo bado lengo la mwandishi litakuwa limetimia endapo kitapata wasomaji wengi.
 
Watanzania wakisome kitabu cha kabendera kilichoandikwa kwa kingereza wakati katiba ya nchi yao wenyewe ambayo ipo kwa kiswahili hawajawahi kufungua hata ukurasa mmoja?
 
Ungetoa na muhutasari wake alau ingesaidia.
 
Acha porojo za ccm lumumba humu,mwandishi apindue nch,ugoro sio nzuri kwa afya ya akili
 
Hiyo ya kutowapa maendeleo sehemu zilizochagua upinzani ilikuwa ni turning point mbaya sana. Hata ile ya bukoba kwa wahanga wa tetemeko. Alionesha ubaguzi wa wazi

Ila tutasemaje mkuu, ukiongea kitu negative unaonekana mpinga legacy. Tunaishia kukaa kimya tu
 
Magu alisema "money laundering "
 
Kabendera siyo investigative journalist; ukisoma hata kitabu chake utaona kuwa hakina hata chembe yoyote ya uchunguzi. Nilisoma makala yake kwenye jarida la Economist ambayo ndiyo iliyomtia matatani, ilijaaa udaku mtrupu na hata lugha aliyokuwa ametumia kumweleza Magufuli ilikuwa siyo ya mtu professional; huwezi kuandika kwenye jarida kubwa na kusema "...the presidents stupid decision" halafu ukaita hiyo ni investigative journalizma. Kusema mtu magufuli ni stupid ilikuwa ni opnion yake binafsi ambazo ziko below journalizma standards.

Sikuwahi kusoma makala za Azory lakini Stan ndiye alikuwa anaandika Invesitgative articles sawasawa bila kuweka maoni yake binafsi. Kuna mwingine nimesahahu jina lake naye alikuwa mwandishi mzuri sana wa investigative report; mara ya mwisho nilisafri naye kwenda Harare mwaka 1988 alikokuwa anafuatilia habari fulani kuhusu mauaji ya Gukurahundi na kuyumba kwa Unity Accord baina ya Mugabe na Nkomo
 
Asiyefunzwa na makosa ya watangulizi wake atayarudia makosa ya watangulizi wake.
 
Mkuu asante sana! Hiki ndo nilichokuwa nakitafuta. Chanzo hasa cha ugomvi wake na JPM ni kipi? Hii artcles nataka niisome alafu niitafsiri kwa kiswahili alafu tuipitie tena kwa pamoja tuone Kabendera alikosewai na je alichokisema kuhusu JPM kilikuwa ni sahihi?

ARTICLE yenyewe ni hii hapa

 
Kumbe usnitch ulianzia kwa baba hadi mtoto?
Like father like son.
 
Huko kuchafua inchi kukoje,ebu tuelezee alivyokuwa anachafua
 
Siyo hiyo; Nikiipata nitaileta. Hiyo uliyoleta ni baada ya kuwa amekamatwa. Article iliyomtia matatatani ilikuwa analysis mojawapo ya miradi mikubwa ya Magufuli nadhani ama ule wa bwawa la Nyerere au wa SGR na kutumia maneno “the president’s stupid decision”!! Ndipo Magufuli akaamua kumbana mipira.
 

kumbe na Baba yake mzazi pia alikuwa na maisha ya mlengo huo? na akaishia 'kujiua' kwenye Ziwa Victoria mwaka 2000 ?!
Duuh hatari !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…