Kwanini Rais Magufuli alimfunga Kabendera?

Kwanini Rais Magufuli alimfunga Kabendera?

Mimi naona wengi mnaliongelea hili suala kama vile Magufuli aliongoza nchi kwa utulivu pasipo YEYE MWENYEWE kufanya Declaration ya kwenda kinyume na makubaliano au mikataba ya umoja wa mataifa. Kiufupi HAKUJALI

Mfano mdogo tu ni issue ya mabinti wa shule waliopata mimba kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

Alikuwa ni kiongozi ambaye negative news zilikuwa zinatoka kila mara kutokana na kauli zake au actions zake YEYE MWENYEWE

Yes kabendera yawezekana alikuwa akitumika na wazungu kwa sababu tu anapokea pesa zao lakini ni wanaharakati, mashirika na miradi mingapi hadi sasa inategemea pesa za wahisani?....

Nachokiona tu hapa watu mnatetea mtu au watu na sio hoja. Natamani mjadala kama huu ungejawa facts na sio hisia
Waliokupeleka shule hawakukosea!
 
Unaweza kuniambia kwa nini magufuli alienda kuchukua mikopo kwenye bank ya Exim ambayo ina interests za kibiashara na kuacha nchi za wahisani na mashirika ya fedha za kimataifa yenye riba maalum kwa nchi ??...

Unadhani ni nchi ngapi ziliondoa funds zake kwenye miradi mbalimbali ya serikali na hata NGOs kuja Tanzania ikiwemo USA ambaye alipata guts za kumpiga ban mkuu wa mkoa wa nchi asiingie marekani kwa kuhusishwa na utishiaji wa maisha na uhuru wa watu..

Articles zoteee zipo mtandaoni au unadhani uhusiano wa kidiplomasia ni kuingia katika vita mkuu.

Mbona vitu vipo wazi...

Najua wengi mlimpenda Magufuli kama dini na mnaumia mkisikia kasemwa kwa lolote na hata Mimi kuna baadhi ya vitu naona anaonewa sometimes Ila kuna vitu vingi alivifanya ambavyo vitakuwa doa katika utawala wake kama ambavyo Nyerere na Mkapa walikiri baadae kuwa kuna pahali walikosea. Kwa hiyo hamuwezi kugeuza nyeupe kuwa nyeusi, historia ya Magufuli itamuhukumu kama inavyopasa
Hata Mimi nilimkubali sana Magufuli kwa mengi, lakini kuna maeneo alikuwa anakosea mpaka unashangaa kiongozi mkubwa kama yeye anawezaje kufanya hayo?

Mfano:
1. Kutangaza hadharani kutokumwelewa mkurugenzi yeyote atakayemtangazia ushindi wa ubunge mgombea wa upinzani ilhali analipwa na kuhudumiwa na Serikali!

2. Kutangaza waziwazi nia yake ya kuufuta upinzani nchini wakati ni Serikali ndiyo iliyouruhusu mfumo wa vyama vingi!

3. Kuwanunua wapinzani kwa kisingizio cha kuungwa mkono!

4. Kuwapeleka kibabe bungeni wabunge 19 wa viti maalum kinyume cha utaratibu baada ya kujizolea nafasi zote za ubunge na hivyo kukosekana kwa wabunge wa upinzani bungeni!

5. Kutangaza kutoyapa kipaumbele cha maendeleo maeneo yanayoongozwa na wapinzani!
 
Ndio ujue kwamba huyo mkimbizi Kibendera Hana nia njema na taifa hili Kwa hicho kitabu chake kukiandika Kwa lugha ambayo zaidi ya 80% ya watanzania hawaielewi.

Kwa ufupi tu amewalenga watu wa mataifa ya magharibi huko walikompa hifadhi... Na huu ni mwendelezo wa ukibaraka(kazi ambayo amekuwa akiifanya Kwa muda mrefu sana).
Mafanikio mojawapo ya kitabu ni kusomwa na watu wengi. Naamini hajawaandikia Watanzania pekee, bali ulimwengu. Na Watanzania wanapenda kusoma vitabu, wengi wao wanajua English pia. Kwa hiyo bado lengo la mwandishi litakuwa limetimia endapo kitapata wasomaji wengi.
 
Huwa Kuna mentality fulani ya kuiga na ya kinafiki ipo Kwa watanzania wengi hasa hawa middle class ambao wanajiona Wana akili na vi-exposure uchwara walivyonavyo.

Kwamba kufanya chochote au kusema chochote hata kama ni hatarishi Kwa umma ni haki yake ya kidemokrasia.

Unakuta mtu anafanya ufisadi/wizi halafu akishughulikiwa vilivyo, wanatokea watu WA kumtetea kwamba adhabu aliyopewa ni ukiukwaji WA haki.... Na blah...blah kama hizo

Imagine huyo Kabendera kipindi kile jeshi letu limefanikiwa kuthibiti kile kikundi Cha kigaidi kule Kibiti, eti akaanza kuandika makala za kuwatetea wale magaidi kwamba wameonewa sijui wamevunjiwa haki zao za kibinadamu seriously?

Yaani mtu kuisnitch serikali dhidi ya mataifa ya nje eti ndio demokrasia hiyo, SI upumbavu huo?

Haya leo hii Kuna watu wanaamini eti wale wahanga wa vyeti feki walionewa.... Yaani mtu katumia udanganyifu kujipatia ajira serikalini, wakati huo Kuna watu kibao tu wenye sifa wako mitaaan... Haya leo hii ameshtukiwa na kisha akaondolewa kazini na nafasi yake kuchukuliwa na mtu mwenye elimu na sifa hii, mara ghafla tunakuja kuambiwa eti huyo mdanganyifu alionewa na anapaswa kulipwa stahiki zake... just imagine?

Hakika watanzania wanahitaji mtu ambaye ni mara tatu ya jinsi alivyokuwa Magufuli hili akili zao ziwakae sawa.

Kuna self-entitlement ya kipumbavu mno
Watanzania wakisome kitabu cha kabendera kilichoandikwa kwa kingereza wakati katiba ya nchi yao wenyewe ambayo ipo kwa kiswahili hawajawahi kufungua hata ukurasa mmoja?
 
Makosa ya Kabendera ni Kama ya baba yake Kabendera Shinan alipobanwa na SERIKALI ya Mkapa akaamua kujiua Ziwa Victoria Mwaka 2000,

Alionekana kutumiwa na majirani na bbc kufifisha Juhudi za Mkapa !

Mzee Kabendera ni Mnyarwanda aliyeishi katoMa bukoba , hata msiba wake Rwanda Ulitikisa aliacha baadhi ya ndugu zake Erik huko Rwanda

View attachment 3193545View attachment 3193546View attachment 3193547View attachment 3193548
Ungetoa na muhutasari wake alau ingesaidia.
 
Kabendera alikuwa anatumika na watu wa nje kumhujumu Magufuli alitaka kupindua utawala wa Magu.
Mwandishi wa habari unaandika artcles 4 kwa mwezi kwenye akaunt yako unalipwa million 300. Unachomoa pesa unazitawanya kwa wakosoaji wa serikali mitandaoni. Hiyo investigative journalism kilikuwa kichaka cha money laundering alikuwa anatumika kwa kazi maalum kazi chafu.
Acha porojo za ccm lumumba humu,mwandishi apindue nch,ugoro sio nzuri kwa afya ya akili
 
Hata Mimi nilimkubali sana Magufuli kwa mengi, lakini kuna maeneo alikuwa anakosea mpaka unashangaa kiongozi mkubwa kama yeye anawezaje kufanya hayo?

Mfano:
1. Kutangaza hadharani kutokumwelewa mkurugenzi yeyote atakayemtangazia ushindi wa ubunge mgombea wa upinzani ilhali analipwa na kuhudumiwa na Serikali!

2. Kutangaza waziwazi nia yake ya kuufuta upinzani nchini wakati ni Serikali ndiyo iliyouruhusu mfumo wa vyama vingi!

3. Kuwanunua wapinzani kwa kisingizio cha kuungwa mkono!

4. Kuwapeleka kibabe bungeni wabunge 19 wa viti maalum kinyume cha utaratibu baada ya kujizolea nafasi zote za ubunge na hivyo kukosekana kwa wabunge wa upinzani bungeni!

5. Kutangaza kutoyapa kipaumbele cha maendeleo maeneo yanayoongozwa na wapinzani!
Hiyo ya kutowapa maendeleo sehemu zilizochagua upinzani ilikuwa ni turning point mbaya sana. Hata ile ya bukoba kwa wahanga wa tetemeko. Alionesha ubaguzi wa wazi

Ila tutasemaje mkuu, ukiongea kitu negative unaonekana mpinga legacy. Tunaishia kukaa kimya tu
 
Ndugu wanajamvi,

Tumesikia kuhusu kitabu kipya cha Erick Kabendera kinachoitwa "In the Name of the President: The Memoirs of a Jailed Journalist". Kabendera amefunguka kwa kina juu ya utawala wa Magufuli na madai ya udikteta. Hii inatufanya tujiulize maswali mengi kuhusu sababu halisi za kufungwa kwake.

Ni wazi kuwa Kabendera alikuwa mwandishi wa habari shupavu, lakini je, hatua za kumkamata na kumfungia zilikuwa za haki? Au zilikuwa juhudi za kumnyamazisha kwa sababu ya uandishi wake?

Kwa vile tunafahamu kwamba baadhi ya wanachama wetu hapa ni wafanyakazi wa idara za usalama, jeshi, na ulinzi, wafanyakazi wa ikulu na watumishi wa inner circle tunapenda kupata mitazamo yenu juu ya suala hili:

1. Je, ni nini hasa kilichosababisha Kabendera kuonekana tishio kwa utawala wa Magufuli?

2. Kuna ukweli wowote katika madai kuwa utawala huo ulitumia nguvu za dola kuzima uhuru wa vyombo vya habari?

3. Kwa maoni yenu, je, kufungwa kwa Kabendera kulikuwa na athari gani kwa tasnia ya uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania?

4. Kwa nini utawala wa Magufuli ulikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya waandishi wa habari huru kama Kabendera?

Tunaomba mjadala huu uwe wa kistaarabu, wa kina, na wa kuheshimu maoni tofauti. Ikiwezekana, tusaidiane kupata ukweli ili kuangazia mustakabali wa uhuru wa vyombo vya habari nchini mwetu. Jambo zuri ni kwmaba mzee hayupo tena kwa sababu kipindi cha utawala wake hadi hili jukwaa la siasa lilikuwa compromised. Niliwahi kupost threads zenye hoja na zilifutwa na maadmin bila sababu hali hii ikasababisha nilichukie sana hili jukwaa la siasa.

Karibuni kwa mjadala.

View attachment 3191541
Magu alisema "money laundering "
 
Kabendera ni mwandishi wa habari za kiuchunguzi [Investigative Journalism] ni watu wanaokuwa katika hatari ya kupoteza maisha au kufungwa maana muda mwingine huingia katika anga za hatari.

Azory Gwanda akichunguza masuala ya Kibiti alipotea hadi leo.

Stan Katabaro akichunguza kashfa ya uuzwaji wa Loliondo[ Loliondo gate ] aliuwawa.

Nakuwekea hapa makala ya Gold Mafia kutoka Al Jazeera uone wandishi wa namna hiyo wanavyoingia kupekenyua data katika mazingira magumu.

Gold Mafia ni skendo iliyomuhusisha rais wa Zimbabwe na wasaidizi wake wakiwemo ndugu kufanya utakatishaji pesa wa mamilioni ya dola kupitia biashara ya dhahabu.

Angalia waandishi walivyokuwa wakiingia anga za hatari kupata data na ukweli juu ya utakatishaji pesa uliohusisha hadi rais wa nchi ya Zimbabwe.

View: https://youtu.be/evWEuVR1XIs?si=tKtDsSzJYBL1Lj_u

Kabendera siyo investigative journalist; ukisoma hata kitabu chake utaona kuwa hakina hata chembe yoyote ya uchunguzi. Nilisoma makala yake kwenye jarida la Economist ambayo ndiyo iliyomtia matatani, ilijaaa udaku mtrupu na hata lugha aliyokuwa ametumia kumweleza Magufuli ilikuwa siyo ya mtu professional; huwezi kuandika kwenye jarida kubwa na kusema "...the presidents stupid decision" halafu ukaita hiyo ni investigative journalizma. Kusema mtu magufuli ni stupid ilikuwa ni opnion yake binafsi ambazo ziko below journalizma standards.

Sikuwahi kusoma makala za Azory lakini Stan ndiye alikuwa anaandika Invesitgative articles sawasawa bila kuweka maoni yake binafsi. Kuna mwingine nimesahahu jina lake naye alikuwa mwandishi mzuri sana wa investigative report; mara ya mwisho nilisafri naye kwenda Harare mwaka 1988 alikokuwa anafuatilia habari fulani kuhusu mauaji ya Gukurahundi na kuyumba kwa Unity Accord baina ya Mugabe na Nkomo
 
Hiyo ya kutowapa maendeleo sehemu zilizochagua upinzani ilikuwa ni turning point mbaya sana. Hata ile ya bukoba kwa wahanga wa tetemeko. Alionesha ubaguzi wa wazi

Ila tutasemaje mkuu, ukiongea kitu negative unaonekana mpinga legacy. Tunaishia kukaa kimya tu
Asiyefunzwa na makosa ya watangulizi wake atayarudia makosa ya watangulizi wake.
 
Kabendera siyo investigative journalist; ukisoma hata kitabu chake utaona kuwa hakina hata chembe yoyote ya uchunguzi. Nilisoma makala yake kwenye jarida la Economist ambayo ndiyo iliyomtia matatani, ilijaaa udaku mtrupu na hata lugha aliyokuwa ametumia kumweleza Magufuli ilikuwa siyo ya mtu professional; huwezi kuandika kwenye jarida kubwa na kusema "...the presidents stupid decision" halafu ukaita hiyo ni investigative journalizma. Kusema mtu magufuli ni stupid ilikuwa ni opnion yake binafsi ambazo ziko below journalizma standards.

Sikuwahi kusoma makala za Azory lakini Stan ndiye alikuwa anaandika Invesitgative articles sawasawa bila kuweka maoni yake binafsi. Kuna mwingine nimesahahu jina lake naye alikuwa mwandishi mzuri sana wa investigative report; mara ya mwisho nilisafri naye kwenda Harare mwaka 1988 alikokuwa anafuatilia habari fulani kuhusu mauaji ya Gukurahundi na kuyumba kwa Unity Accord baina ya Mugabe na Nkomo
Mkuu asante sana! Hiki ndo nilichokuwa nakitafuta. Chanzo hasa cha ugomvi wake na JPM ni kipi? Hii artcles nataka niisome alafu niitafsiri kwa kiswahili alafu tuipitie tena kwa pamoja tuone Kabendera alikosewai na je alichokisema kuhusu JPM kilikuwa ni sahihi?

ARTICLE yenyewe ni hii hapa

Makosa ya Kabendera ni Kama ya baba yake Kabendera Shinan alipobanwa na SERIKALI ya Mkapa akaamua kujiua Ziwa Victoria Mwaka 2000,

Alionekana kutumiwa na majirani na bbc kufifisha Juhudi za Mkapa !

Mzee Kabendera ni Mnyarwanda aliyeishi katoMa bukoba , hata msiba wake Rwanda Ulitikisa aliacha baadhi ya ndugu zake Erik huko Rwanda

View attachment 3193545View attachment 3193546View attachment 3193547View attachment 3193548
Kumbe usnitch ulianzia kwa baba hadi mtoto?
Like father like son.
 
Asiyefunzwa na makosa ya watangulizi wake atayarudia makosa ya watangulizi wake.
images - 2025-01-09T081549.987.jpeg
 
Hàya majibu ànayo Pascal Mayalla , ilisemekana ndo alimchoma kabendera kwa Magufuli. Hii ni inasemekana mimi sina uhakika.
Huyu jamaa alikuwa ànatumia feki I'd huko "gazetini" kuandika màmbo ya "kuçhafua nchi"! Mayalla akamweka wazi kwa home boy wake.
Huko kuchafua inchi kukoje,ebu tuelezee alivyokuwa anachafua
 
Mkuu asante sana! Hiki ndo nilichokuwa nakitafuta. Chanzo hasa cha ugomvi wake na JPM ni kipi? Hii artcles nataka niisome alafu niitafsiri kwa kiswahili alafu tuipitie tena kwa pamoja tuone Kabendera alikosewai na je alichokisema kuhusu JPM kilikuwa ni sahihi?

ARTICLE yenyewe ni hii hapa

Siyo hiyo; Nikiipata nitaileta. Hiyo uliyoleta ni baada ya kuwa amekamatwa. Article iliyomtia matatatani ilikuwa analysis mojawapo ya miradi mikubwa ya Magufuli nadhani ama ule wa bwawa la Nyerere au wa SGR na kutumia maneno “the president’s stupid decision”!! Ndipo Magufuli akaamua kumbana mipira.
 
Makosa ya Kabendera ni Kama ya baba yake Kabendera Shinan alipobanwa na SERIKALI ya Mkapa akaamua kujiua Ziwa Victoria Mwaka 2000,

Alionekana kutumiwa na majirani na bbc kufifisha Juhudi za Mkapa !

Mzee Kabendera ni Mnyarwanda aliyeishi katoMa bukoba , hata msiba wake Rwanda Ulitikisa aliacha baadhi ya ndugu zake Erik huko Rwanda

View attachment 3193545View attachment 3193546View attachment 3193547View attachment 3193548

kumbe na Baba yake mzazi pia alikuwa na maisha ya mlengo huo? na akaishia 'kujiua' kwenye Ziwa Victoria mwaka 2000 ?!
Duuh hatari !
 
Back
Top Bottom