Kwanini Rais Magufuli alimfunga Kabendera?

Kwahiyo unataka kusema Pascal Mayalla alikuwa ànamzuia kabendera asiendelee kufichua ufisadi wa serikali uliokuwa unawekwa wazi na kabendera?
 
Je mafisadi na majizi wanatokea wapi?,,
 
Bahati nzuri Pascal Mayalla yupo humu na ni active member. Kuna ukweli hapa?
 
Sswa mimi mjinga ila jibu swali. Kabendera angepindua vipi hii nchi ilihali hata jeshi hana? Au ndo insecurities za jpm baada ya Kabendera kuhoji mambo ya ndnai ya familia ya JPM?
Kumbe wwe bado mtoto, hujuwi nguvu ya kalamu!? Ukitaka kujua nguvu ya kalamu ya mwandishi nenda kawaulize Rwanda kuhusu yale mauwaji ya kwao! The Rwanda genocide!!
 
Achafue kitu kilichokuwa kimechafuka

Mbona ilikuwa wazi kuwa Magufuli hakujali kuhusu uhusiano wa kidiplomasia na nchi kubwa hususani nchi za magharibi

Yeye mwenyewe mara zote alitoa kauli controversial kwa kushutumu kuanzia viongozi wa ndani hadi mabeberu kwa matatizo yote.

Au kuweka bunge lote kuwa la kijani katika uchaguzi wa 2020, nalo kasingiziwa

Mara ngapi yeye mwenyewe alienda kinyume na makubaliano au mikataba iliyopelekea ndege za nchi kuzuiwa na billions of money serikali kulipa baada ya kifo chake ili kurudisha hayo mahusiano na nchi za kimataifa na wawekezaji.

Vitu ambavyo Tindu alivipigia kelele siku zote na vitu vilivyokuja kutokea.

Magufuli alikuwa ni Rais Mtendaji ndio maana kwenye physical infrastructures ameacha legacy kubwa Ila tukiongelea katika diplomasia, intellect, utawala wa sheria, na Demokrasia. Toka vyama vingi vianze anaweza kuwa the worst president

Na ubaya wa nchi hii ni wanachi kutetea vyama na viongozi kuliko kutetea nchi yao. Hii ndio sababu tumefika hapa
 
Watu wengi sana wanaponda alilofanyiwa huyu ndugu yetu ila amini nawaambia hakuna mtu anayempenda mmbea anayeichunguza na kuisema familia yake mitaani.

Hivyo ndivyo ilivyo na stahiki zake.
 
Ukitaka kujua ni kwa nini kabendera alikamatwa. Kwanza lazima ujue kabendera ni mwandishi wa habari za kichunguzi. Na habari zake alikuwa anayatumia makampuni ya kigeni hasa wingereza. Fikiria mwandishi achunguze na kupata habari nyeti na kuzituma nje ya nchi si hatari hiyo?
Ukizingatia kipindi cha magufuli kuna watu walikuwa wamejipanga kuhakikisha wanampa wakati mgumu katika kuiongoza hii nchi.

Hata hivyo nadhan kabendera ana mtandao mkubwa ndani ya serhkali unaomlinda maana mara nyingi mtu ukijua siri za ikulu usalama wako ni mdogo.
 
umeandika maoni mazuri kabisa yasiyo na chembe ya unafiki. Kuhusu mabeberu nadhani alikuwa anasema ukweli japo wenyewe hawapendi kuambiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…