Kwanini Rais Samia amesema hataki mabango, Je hii ndiyo demokrasia?

Mkuu tunazungumzia li nchi hili la tanzania sio office hii mkuu hii nchi kubwa mno,,
rais hawez kufika kila sehemu,
Lazma tujenge utamaduni wa kila mtendaji kuwajibika eneo alipo.
Wewe t apo mkuu unaweza ukawa upo dar unaish magomeni gongolamboto hujakanyaga mwaka mzima.
lazma tujenge utamaduni wa uwajibikaji kila mtu katika eneo lake atimize majukumu yake.
Hili suala hata hayati magufuli amelisemea sana wat wawajibike katka maeneo yao,
Sio kila jambo mpaka rais ndo aje alishughulikie.
Kama wewe ni mtendaji uko kakonko kigoma jiulize niko huku kwa ajili gani,lazma ujihis natakiwa kutatua kero za watu.

Tukienda ivo kwamba kila kitu ad rais hatutafika popote milele.
Mkuu nakubaliana na wewe 100% na hayati Magufuli alishawahi sema. Issue yangu ni kwamba je Tuwazuie wanchi wasibebe Mabango au tuwaache ili ikitokea mkuu wa Nchi kapita hapo apate ujumbe wake na ajue nini kero au matatizo ya eneo husika au pia apokee mabango yanayomsifu na kumtia Moyo?

Mimi naona tuwaache watu wawe huru ila Watendji wapige kazi aisee. Mkuu ni rais kusema ila ukweli mambo bado sana hapa kwetu.
 
Mimi nilimsikiliza na nikamuelewa. Alisema hataki kuona mabango akifanya ziara wilayani au mikoani kwa sababu kero za wananchi wa mkoa au wilaya husika zinatakiwa zishugulikiwe na wanaosimamia jukumu hilo kwa niyaba yake ambao ni Mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa.

Hivyo aliyasema hayo ili kuwahamasisha watendaji husika kusimamia ktk kutatua kero za wananchi, kwani kuibuka kwa mabango ya kero za wananchi kunaashiria wahusika hawajitumi ipasavyo ktk kusimamia lero zao.
Kama Rais; anawajibika kutatua kero za wananchi.
 
Mimi nilimsikiliza na nikamuelewa. Alisema hataki kuona mabango akifanya ziara wilayani au mikoani kwa sababu kero za wananchi wa mkoa au wilaya husika zinatakiwa zishugulikiwe na wanaosimamia jukumu hilo kwa niyaba yake ambao ni Mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa.

Hivyo aliyasema hayo ili kuwahamasisha watendaji husika kusimamia ktk kutatua kero za wananchi, kwani kuibuka kwa mabango ya kero za wananchi kunaashiria wahusika hawajitumi ipasavyo ktk kusimamia lero zao.

Mkuu mi Nikuulize kitu!
Kwani Kero Huwa Zinaisha?
Kamwe haziwezi Kawisha hata Kidogo!Kukiwa hamna Kero basi Haina Haja ya Kuwepo watu Ofisini!
Wewe unahudumia watu say 500,000 tuu Unadhanibwote wataridhika mahitaji yao Kutekelezwa 100%?
Kipimo kipi unaweza tumia Kusema Hapa Tumepunguza Kero?
Uchache wa mabango?
Mwingine atakuja Mara kadhulumiwa kiwanja,Wakati unaendelea nalo Kuna Mwingine Hawajapatiwa Afya,Maji nk nk!
Ok Kipimo cha Ufanisi nadhani kungekuwa na KPI ambazo kila Mtu Ofisni mwake anazijua ili aweze kuzipunguza in Quantity!
Amepokea Kero 50 Kwa mwezi,Ametatua 20,Zilizobaki zipo on Progress!
Lakini Tukisema Mabango tuu...Mtaumiza hao watu na Kuchukia Kazi au Kufanya Kwa woga,Na woga huondoa Ufanisi!
 
Mimi nilimsikiliza na nikamuelewa. Alisema hataki kuona mabango akifanya ziara wilayani au mikoani kwa sababu kero za wananchi wa mkoa au wilaya husika zinatakiwa zishugulikiwe na wanaosimamia jukumu hilo kwa niyaba yake ambao ni Mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa.

Hivyo aliyasema hayo ili kuwahamasisha watendaji husika kusimamia ktk kutatua kero za wananchi, kwani kuibuka kwa mabango ya kero za wananchi kunaashiria wahusika hawajitumi ipasavyo ktk kusimamia lero zao.

Kunung’unika ni hulka ya binadamu. Kufikiria kwamba kila mwenye manung’uniko ana hoja ya msingi ambayo ni lazima itatuliwe kwa namna ambayo mnung’unikaji ataridhika ni unrealistic. Kama sio kuweka mwanya wa RC au DC kuanza kutoa vitisho kwa watu wa aina hiyo, RC au DC afanye nini ili kuhakikisha kuwa mtu kama huyo hazuki na bango siku Rais akija?
 
Cc: Godo
 
Mama la mama Rais wetu yupo sahihi 100% ✔️ alisema kwanini watendaji wasi wajibika kwa wana Nchi wakati ndio kazi zao! yeye ana kazi zingine hataki mama movie kama mwenda zake haramia
 
Kiongozi mbona kauli ya rais Samia Suluhu iko wazi. Uwepo wa mabango tafsiri yake ni kwamba wateule wake hawawajibiki.
Kwa mantiki ya kwamba viongozi wa ngazi za chini wapige kazi kutatua kero za wananchi. Ndo maana akasema kila bango litaondoka na mtu/kiongozi.
 
Mkuu nakubaliana na wewe 100% na hayati Magufuli alishawahi sema. Issue yangu ni kwamba je Tuwazuie wanchi wasibebe Mabango au tuwaache ili ikitokea mkuu wa Nchi kapita hapo apate ujumbe wake na ajue nini kero au matatizo ya eneo husika au pia apokee mabango yanayomsifu na kumtia Moyo?

Mimi naona tuwaache watu wawe huru ila Watendji wapige kazi aisee. Mkuu ni rais kusema ila ukweli mambo bado sana hapa kwetu.
Ndo tunataka tuelekee uko ambapo mfumo ndo uwe unafanya kazi na sio mtu mmoja,,
Tutafkaje uko kama hatujapigana mikwara tukajenga hayo mazoea.
Mtu mmoja hawez kumaliza matatzo yote ya watu mil.60.
Kila mtu awajibike katka eneo lake.
Kuanzia mtu mmoja mmoja mpaka kwa watendaji na wateule wa rais.
Na hapo ndo tutakapopata maendeleo ya kweli.
Mimi sio muumin wa mtu mmoja kupita uko mabrbrn kusmamisha gari et unatatua kero za wananchi then what,
Zile kwangu ni siasa tu.
Ukipita ushaondoka then kero zinazofuata anatatua nan.
Rais samia akazie hapo hapo ili tujenge nidhamu kwanza ya ki utendaji kwa hawa wateule na watendaji wa chini.
 
Back
Top Bottom