Kwanini Rais Samia hajawahi kumjulia hali Mzee Lowassa?

Kwanini Rais Samia hajawahi kumjulia hali Mzee Lowassa?

Mheshimiwa Rais Samia ameonekana mara kadhaa akiwatembelea viongozi wakuu wastaafu mbalimbali majumbani mwao au kukutana nao ikulu kwa mazungumzo na kubadilishana uzoefu wa maswala kadhaa ya uongozi.

Ila sijawahi kumuona akikutana au akimjulia hali mzee Edward Ngoyai Lowasa(waziri mkuu mstaafu).

Je, ni lini Rais Samia atamjulia hali mzee Lowasa kama anavyofanya kwa viongozi wengine?

Asanteni
Kama huna taarifa usipende kuongea hasa ktk public. Sasa tumia hii simu uliyoandikia hii hoja fake kuona Mhe. Rais alimtembelea lini Mzee Lowassa.🙏🙏🙏
 
Mheshimiwa Rais Samia ameonekana mara kadhaa akiwatembelea viongozi wakuu wastaafu mbalimbali majumbani mwao au kukutana nao ikulu kwa mazungumzo na kubadilishana uzoefu wa maswala kadhaa ya uongozi.

Ila sijawahi kumuona akikutana au akimjulia hali mzee Edward Ngoyai Lowasa(waziri mkuu mstaafu).

Je, ni lini Rais Samia atamjulia hali mzee Lowasa kama anavyofanya kwa viongozi wengine?

Asanteni
MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA KUMJULIA HALI LOWASSA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu Afrika ya Kusini.

Akizungumza na wanafamilia kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia, Waziri Mkuu amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais na kusema Mheshimiwa Rais anafuatilia hali ya Mheshimiwa Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.

Waziri Mkuu ametoa salamu hizo leo (Jumatano, Desemba 28, 2022) jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambako alienda kumjulia hali Mheshimiwa Lowassa.

Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao.

Naye mtoto mkubwa wa Mheshimiwa Lowassa na Mbunge wa Monduli, Bw. Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.

View attachment 2461149
Natumaini umejibiwa!.
P
 
Mheshimiwa Rais Samia ameonekana mara kadhaa akiwatembelea viongozi wakuu wastaafu mbalimbali majumbani mwao au kukutana nao ikulu kwa mazungumzo na kubadilishana uzoefu wa maswala kadhaa ya uongozi.

Ila sijawahi kumuona akikutana au akimjulia hali mzee Edward Ngoyai Lowasa(waziri mkuu mstaafu).

Je, ni lini Rais Samia atamjulia hali mzee Lowasa kama anavyofanya kwa viongozi wengine?

Asanteni
Jibu unalo.....alishaenda na juzi PM kamuwakilisha
 
Wanamchukulia poa lowasa kwa sababu wanaamini watamuwin rostam aziz. Kwa mfano wamempa uwaziri kijana wa Rostam bwana Bashe.

Rostam ni Lowasa na Lowasa ni Rostam.

Wasichojua ni kuwa Lowasa ana mizizi mirefu mno ndani ya CCM. Je mmesahau ukumbi mzima ulipoinuka na kuimba tuna imani na Lowasa? Je mmesahau mafuriko ya Lowasa ya 2015?

Hata JPM aliijua nguvu ya Lowasa ndio maana alitoka ikulu akaenda Lumumba kumlaki na 2020 alipata kura nyingi tu zilitoka kwa watu wa Lowasa. Aliamua kuzika tofauti zake na Lowasa.

Huyu mama kwa sababu ni timu JK kwa hiyo anaogopa kumuudhi JK na Kinana & Co, ila JK mwenyewe anaijua nguvu ya Lowasa sema amekaza shingo na ana kisasi kwa alivyochanwa chanwa 2015.

Anachofanya ni kulipiza kisasi kwa watu wa Lowasa maana wanajuana vizuri sana. Kwa sasa hutosikia kina Nchimbi au Sophia Simba wakila shavu kwenye hii serikali ya JK kwa mwamvuli wa Samia. Na hutoona JK na Rostam wakikaa meza moja. Hawa ni mahasimu haswa. Ikumbukwe Rostam Aziz alijivua ubunge na kujitoa kwenye siasa kwa sababu ya JK. Aliamua kujikita kwenye biashara zake.

Rostam anajua CCM ya kina JK wanataka kampani yake 2025 sababu wanaijua nguvu yake. Anajua fika hawa ni waswahili tu na anaishi nao kwa akili mno. Ndio maana humuoni Rostam wala kumsikia hata kwenye shughuli zao mbalimbali za uzinduzi. Hata hii ya Makamba kubeba mitungi ya Taifa gesi ni hadaa tu ya kumsogeza huyu mwamba. Ila jamaa yupo smart mno ku deal na hizi takataka.

Bado kuna nguvu kubwa ya Lowasa kuliko ya JK ndani ya CCM. Na katika hili kuna uwezekano mkubwa 2025 huyu maza akakosa kura nyingi za watu wa Lowasa na pengine wa JPM.

JK hajawahi kuwa na siasa za kimkakati. Ndio maana hata upigaji wao huwa unaonekana waziwazi.

Upinzani wakijipanga vizuri watakuwa na nafasi nzuri. Hata wabunge wa JK wanaweza wakakosa kura za wanaccm wengi na kura zikaenda kwa wapinzani. Na kuna uwezekano wa wabunge wengi wa JPM kutolewa kwa hila na hapa pia utakuwa mpasuko mwingine ambao ni faida kwa upinzani.

Tuendelee kuchochea kuni.View attachment 2461843
images%20(7).jpg
 
Why,
Kwa sasa hana madhara yoyote.
Madhara ya Lowasa ni base aliyoitengeneza na atakayoiacha ndani ya CCM. Hii itaisumbua CCM muda wote. Lowasa alienda UKAWA na wafuasi, sio wanachama. Kina nchimbi ni wafuasi wa Lowasa ila ni wanachama wa ccm.

Hata Kingunge na kina Sumaye walikuwa ni wafuasi wa Lowasa ila ni wanaccm. Imagine ana wafuasi kiasi gani. Ule mtikisiko na mafuriko 60% ilikuwa CCM na 40% ilikuwa ukawa.
 
LOWASA NA FAMILIA YAKE HAWATAKI MTU KUMTEMBELEA LOWASA, HALI YAKE MBAYA NA SIO VIZURI KWA STARA YAKE
 
Mheshimiwa Rais Samia ameonekana mara kadhaa akiwatembelea viongozi wakuu wastaafu mbalimbali majumbani mwao au kukutana nao ikulu kwa mazungumzo na kubadilishana uzoefu wa maswala kadhaa ya uongozi.

Ila sijawahi kumuona akikutana au akimjulia hali mzee Edward Ngoyai Lowasa(waziri mkuu mstaafu).

Je, ni lini Rais Samia atamjulia hali mzee Lowasa kama anavyofanya kwa viongozi wengine?

Asanteni
Wahafidhina mpo?
 
Back
Top Bottom