Haiwezekani unazuia mikutano ya kisiasa wakati katiba inaruhusu, huwezi kuzuia watu kujadili katiba ya nchi wakati siyo uhaini wala hakuna katiba iliyovunjwa. Hivi kwani Uchamungu umekua ni msamiati mzito sana kwa watawala wetu?
Unaweka makatazo batili maana yake nini? Yaani tusubiri ujenge uchumi wakati mambo mengine hayasubiri? Haya makatazo ni kwa mujibu wa sheria ipi?
Marais wote toka ccm watakaofuata baada ya Magufuli, watafanya kazi kwa kubanwa sana.
1) Kulazimika kuendeleza miradi ya Magufuli iliyoungua bila kuiva, ambayo inagharimu kuliko uwezo wa nchi, iliyokuwa inategemea fedha za "Dhulma".
2) Kwa kuwa ccm ni chama mfu kinachojiegemeza kwenye Dola, watalazimika kuvibana vyama vya upinzani visifurukute. Wataoneshwa mfano wa Kikwete aliyejaribu kuwapa wapinzani mwanya kidogo tu, wakachukua nchi uchaguzi wa 2015, sema tu ilibidi mbinu za ziada zitumike kupindua meza.
3) Kutokana na rushwa kushamiri, mipango mibovu, historia mbaya, ccm imeshindwa kuleta ufumbuzi wa Kweli wa matatizo ya nchi. Imeishiwa pumzi. Ubabe ni muhimu, na suala la Katiba mpya litaleta matatizo zaidi kwa ccm.
4) suala la Muungano ni bomu linalongoja kulipuka muda wowote. Angalau ccm inahitaji kuwepo madarakani ili ilikalie bomu hilo. Chama kingine kikiingia madarakani, kitalitegua na kuufumua Muungano. Wachawi wa ccm hawataki kusikia habari hiyo. Wako radhi kuficha kichwa mchangani kama mbuni